Showing posts with label Peter Omari. Show all posts
Showing posts with label Peter Omari. Show all posts
Wednesday, August 13, 2008
Walimu wa sinema 'stunts'
Hao ndo walifundisha akina Peter Omari, Shaffi Abdul na Charles Magali stunts zao kwenye sinema Bongoland II. Nilishangaa waigizaji Bongo walivyoniambia kuwa eti watu wanapigana kweli hadi kuumizana wakiwa kwenye shuti. Hizi sinema za Hollywood hakuna kuumizana ingawa utadhani mtu kapigwa kweli kweli.
Tulivyokuwa Bongo niliwashauri watu wajifunze hizo stunts maana walikuwa wanatoa mafunzo bure. Zaidi ya kipigana aliwaonyesha kidogo defensive driving (yaani kuendesha gari kwa stunt). Hapa Marekani watu wanalipa maelfu ya dola kujifunza.
Mwalimu Jason Hilton alitaka kufundisha wabongo wengi lakini hakuna aliyejitokeza zaidi ya waliokuwa kwenye sinema. Nilivyowauliza vijana fulani kama wanataka kujifunza waliuza eti watalipwa shilingi ngapi. Somo inatolewa bure halafu unataka ulipwe? Si ukachukua huo utalaamu uliyopata na uende ukatengeneza pesa? Au, ni wazo baya kwangu?
Friday, February 22, 2008
Uzinduzi Rasmi - Bongoland II

Habari kutoka Kibira Films International:
Moja kwa moja kutoka mjini Dar-Es-Salaam, tunafurahi kutangaza siku ya uzinduzi maalumu wa sinema ya Bongoland II. Tarehe ya uzinduzi ni mwezi April 5, 2008 hapa mjini Minnepolis, Minnesota katika ukumbi wa sinema wa Oakstreet Cinema.
Sinema hii ilitengenezwa mwaka jana July pale mjini Dar. Vitongoji maarufu vya mji huo kama Manzese na Magomeni vilitumika katika utengenezaji wa sinema hii. Kusema kweli, hii itakuwa ni hadhi kubwa ya wasanii wa ki-Tanzania maana sinema hii itaonyeshwa katika tamasha mbali mbali za sinema za kimataifa.
Sinema hii ni inamhusu Juma Pondamali ambaye baada ya maisha na malengo yake kutofanikiwa nchini Marekani, aliamua kurudi nyumbani. Lakini visakato alivyovikuta nyumbani vilimshangaza sana na hakuna kitu chochote hapa ulimwenguni ambacho kingemtayarisha kupambana na visakato hivyo.ANGALIA TRELA MPYA
Jitayarishe kuwaona wacheza sinema wakongwe wa Tanzania kama Mzee Kipara, Bi Chuma Selemani Mzee na Bi Thecla Mjatta. Vile vile pia kuwaona wachezaji chipukizi kutoka mjini Dar-es-salaam.
Msanii mhusika mkuu ni Peter Omari ambaye anacheza kama Juma. Peter, ambaye kwa sasa anishi Mwanza, aliwahi kucheza katika sinema yetu iliyopita iliyoitwa TUSAMEHE.
Saturday, September 22, 2007
Trailer ya Bongoland II sasa iko You Tube
Labels:
Bongoland II,
Peter Omari,
Thecla Mjatta,
Trailer
Monday, September 10, 2007
Je, wajua hizi Bia?

WaBongo wanapenda sana kunywa bia. Naweza kusema nimeonja hizi mbili na ile Jahazi ni tamu zaidi. Mtapata habari zaidi ya hizi bia kwenye sinema mpya Bongoland II.
Kwenye picha ya juu, Juma (Peter Omari) na mchumba wake Naomi (Sabrina Rupia) wanaburudika na bia ya Swift Kick.
Labels:
Bongoland II,
Bushoke,
Jahazi Ale,
Peter Omari,
Sabrina Rupia,
Swift Kick
Thursday, August 09, 2007
Bongoland II ndani ya Bongo
Labels:
Bongoland II,
Josiah Kibira,
Mikocheni B,
Peter Omari,
Sam Fischer,
UCLA
Baada ya kazi burudika na...
Labels:
Bongoland II,
Makongoro,
Ndovu,
Peter Omari
Friday, July 27, 2007
Picha zaidi za Bongoland II Film Shoot Dar es Salaam
Cameraman and Cinematographer Sam Fischer, akifanya vitu vyake mitaani Dar es Salaam.
Moja wa Interns kutoka kampuni ya Sofia Records akirekodi somo kuhusu film editing kwenye shoot ya Magomeni.
Mama Thecla Mjatta akisome script kabla ya scene huko Tanki Bovu.
Gayle alikuwa in charge kwenye msawala ya chakula. Hapa yuko Manzese.
Bwana Kibira alimdraftio baba yangu kuwa extra kwenye scene. Nyuma ni Mzee Olutu na Mama Thecla Mjatta .
Mbele ni mcheza sinema maarufu wa Bongo, Shafii. anaposi na interns wa UCLA, baba yangu na Peter Omari.
Mama Mjatta na Mzee Olotu wakipata maelezo kutoka kwa Mwuongoza sinema, Josiah Kibira kabla ya kufanya scene Manzese.Kwa kweli nashukuru kuwa nilipata nafasi ya kushiriki katika sinema ya Bongoland II. Ninamshukuru hasa Bwana Josiah Kibira, kwa kuandika script nyingine safi na kufanikisha kutengeneza kwenye sehemu halisi (authentic location) Dar es Salaam. Kwa kweli safari ilikuwa ndefu mpaka kukamilisha lakini yeye na timu yake walikamilisha.
Natumaini sinema ya Bongoland II ikitoka mtaifurahia mno.
Hizi ni picha zaidi na bado sijasafisha mikanda mingine.
Kwa habari zaidi za Bongoland II someni:
Natumaini sinema ya Bongoland II ikitoka mtaifurahia mno.
Hizi ni picha zaidi na bado sijasafisha mikanda mingine.
Kwa habari zaidi za Bongoland II someni:
Labels:
Abdul Thecla Mjatta,
Bongoland II,
Josiah Kibira,
Manzese,
Mzee Olotu,
Peter Omari,
Shaffii
Thursday, July 26, 2007
Utengenezaji wa Sinema ya Bongoland II mjini Dar es Salaam
Msaidizi wa Josiah Kibira, Chris Audet kutoka Minnesota, akipanga mambo ya shoot. Hapa ni Manzese.
Mama Thecla Mjata anayecheza kama Mama yaka Juma, na Mzee Olotu anayecheza kama Uncle, akitoka kwa hasira ndani ya nyumba. Hapo ni eneo la Tenki Bovu.
Cameraman Sam Fischer, wakiandaa kufanya scene barabarani na Thecla Mjatta na Mzee Olotu.
Hapa ni Manzese. Tulipiga sinema kwenye maeneo hayo. Utatuona tunkimbia maeneo la uchochoroni, hapo ni sehemu moja tulipokimbia. Huyo baba ni Baba Saidi, mjumbe wa eneo hilo la Manzese. Pia alikuwa anakaanga samaki safi sana waliotoka freshi Ferry.
Labels:
Bi Hindu,
Bongoland II,
Liz Michael,
Magomeni,
Manzese,
Peter Omari
Subscribe to:
Posts (Atom)















