Renowned Kenyan Lawyer, PLO Lumumba set to receive an African Luminary Award in Lowell, USA |
(AJABU AFRICAN NEWS, JAN, 26, 2018) LOWELL, Mass.__Professor PLO Lumumba, a popular Kenyan lawyer, who shot to even more limelight recently when he animated proceedings at Kenya Supreme court while defending the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC)---during the reelection battle between president Uhuru Kenyatta of the Jubilee coalition and Raila Odinga of the Opposition's NASA coalition---is set to arrive in Boston this week where he will receive an award for his works that have caused ripples in many corners of the African continent.
Lumumba, who just recently stepped down as the director of the Kenya School of Law to pursue other interests and pave way for fresh leadership will receive the Africa Luminary Award conferred by the African Cultural Association, organizers of the wildly popular Lowell African Festival. (watch Lowell African festival Video Recap here >>)
The unique ceremony will take place this Saturday, January 27th 2018 at the Lodge of Elks hall located at 40 Old Ferry Road in Lowell, approximately 35 miles north of Boston starting at 6pm to around midnight. FULL STORY HERE >>> |
Showing posts with label Tuzo. Show all posts

Sunday, January 28, 2018
Kenyan Lawyer Receives Award in Massachusetts, USA!
Saturday, January 07, 2017
Bodi ya Filamu Nchini Yawaomba WaTanzania Kuzipigania Kura Filamu za Kitanzania Kwenye Tuzo za AMV
BMGHabari
Bodi ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.
Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo (pichani juu) ametoa hamasa hiyo hii leo, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.
“Filamu hizo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu bora na Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili. Niwaase Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu ambao wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi waweze kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili nafasi zote tuzo zije Tanzania”. Amesisitiza Fissoo.
Naye Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards ikiwemo filamu yake ya "Naomba Niseme" inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.
Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.

Bonyeza Hapa Au play hapo chini kusikiliza sauti
Credit: Clouds Fm
Monday, May 25, 2015
Tuzo za Filamu 2015
Tuzo za Filamu 2015 zafana, Serikali Yahaidi Neema
Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015 jana
Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye filamu aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA) kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.
Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Mama yake na Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa ampokelee tuzo mwanaye/
Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Irene Paul (Best Actress) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
John Kalage (Best Director) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.[/caption]
[caption id="attachment_57745" align="aligncenter" width="800"]
Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipeana mkono na viongozi wa meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.[/caption]
[caption id="attachment_57743" align="aligncenter" width="800"]
Grace Mapunda Best Actress Supporting Role) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.[/caption]
[caption id="attachment_57744" align="aligncenter" width="620"]
Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipokea tuzo kwa niaba ya msanii mwenzake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.[/caption]
[caption id="attachment_57749" align="aligncenter" width="800"]
Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za Filamu 2015 jana.[/caption]
[caption id="attachment_57753" align="aligncenter" width="800"]
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Saturday, July 05, 2014
Mahojiano ya Kwanza na Diamond Platinumz Baada ya BET Awards
![]() |
| Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page |
Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo.
Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO.
Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi.
SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini
Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini.
KARIBU
Labels:
BET Awards,
Diamond Platinumz,
singers,
Tuzo
Wednesday, April 09, 2014
Ras Kikwete Achaguliwa Kiongozi Boara Afrika
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya Africa’s
Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo leo.
PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani
Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima
hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African
Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya kesho,
Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St.
Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo
hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye tayari amewasili
mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo
hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango
mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa
Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa
kwa masuala ya utawala bora.
Jarida
hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa
sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo
cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera
na mifumo ya uchumi.
Jarida
hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji
wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za
jarida hilo.
Linasema
Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni
hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali
hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika
uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi
ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”
Sherehe za kesho, miongoni mwa mambo mengine,
zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa
Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa ya
Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine zenye ushawishi mkubwa katika
medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya
jirani.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
Labels:
Award,
President Jakaya Kikwete,
Tanzania,
Tuzo
Saturday, June 15, 2013
Mama Kikwete Atunukuniwa Tuzo ya MDGs nchini Marekani
Mke Wa Rais Mama Salma Kikwete Atunukuniwa Tuzo ya MDGs nchini Marekani
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards,2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement Foundation la nchini Marekani. Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.
*******************
Na Anna Nkinda – New York
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Malengo ya Maendeleo ya Milinia ya mwaka 2013 kwa wanawake na Shirika la Voices of African Mothers (VAM) la nchini Marekani kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kusaidia jamii wakiwemo wanawake na watoto.
Sherehe ya kukabidhi tuzo hizo zimefanyika jana katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amekabidiwa tuzo hiyo kutokana na uongozi wake madhubuti, mafanikio na mchango wake na kujitoa kwake kuwasaidia wanawake na watoto wa Tanzania.
Akikabidhi tuzo hizo Nana – Fosu Randall ambaye ni Rais na mwanzilishi wa shirika hilo alisema kuwa tathimini ilitofanyika kwa mwaka 2012 juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia wametambua kwamba malengo matatu yamefikiwa nchini Tanzania kabla ya muda uliowekwa wa kikomo wa mwaka 2015.
Alisema kuwa wake wa Marais wa Afrika wanamajukumu mbalimbali katika nchi zao ili kufikia Malengo hayo, Taasisi ya VAM imekuwa ikifanya tathimini juu ya hatua zilizofikiwa na Taasisi za wake wa Marais kupitia taarifa za mwaka na zingine zinazowasilishwa.
“Wanawake hawa wanastahili kutuzwa kwani wamefanya kazi kubwa pamoja na kufanya shughuli zao katika mazingira yenye changamoto nyingi ukilinganisha na wenzao katika nchi zingine.
Hafla ya tuzo hizi siyo tu inasherehekea mafanikio ya wake wa marais wa Afrika bali pia inawahamasisha na kuwatia moyo wakati huu ambapo mwaka 2015 unakaribia”, alisema .
Alimalizia kwa kusema kuwa mara nyingi vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari zisizokuwa sahihi kutokana na kazi zinazofanywa na wake wa marais lakini vinasahau kuandika mambo mazuri na kazi kubwa wanayoifanya ya kuwasaidia wananchi na kuviomba vyombo hivyo kubadilika na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya.
Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mama Kikwete alishukuru kwa tuzo aliyopewa na kusema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa sana katika kufikia malengo ya milinia kwani vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 45 na 49 kwa watoto wachanga.
Alisema kuwa haya ni mafanikio makubwa sana japokuwa lengo ni kuondoa kabisa vifo ambavyo vinatokana na sababu ambazo zinazuilika na katika malengo mengine maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanaendelea kupungua kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011.
Mama Kikwete alisema, “Elimu ya msingi inatolewa bure kwa watoto wote walio na umri unaostahili na hatua kubwa imepigwa katika kupunguza ugonjwa wa maralia na vifo vya akina mama vinavyotokana na tatizo la uzazi”
Kwa upande wa harakati za kumkomboa mtoto wa kike alisema kuwa ni lazima ziendelee na zizingatie changamoto mpya za mazingira mapya kwani unapompatia elimu unampunguzia changamoto za ujinsia na kumpatia huduma ya afya ikiwemo uzazi wa mpango, unamuwezesha kushiriki zaidi shughuli za maendeleo ya kiuchumi, unasaidia familia yake na jamii kuweza kuendelea.
Kwa upande wake Dk. Judy Kuriansky ambaye ni mwakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali zilizo chini ya UN alisema kuwa wake wa marais wanafanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuwaunga mkono na kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milinia.
Dk. Kuriansky alisema kuwa ili kufikia malengo ya milinia inatakiwa kuimarisha miundombinu iliyopo jambo ambalo litasababisha kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.
Tuzo hizo zimetolewa kwa mara ya kwanza na shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya The reed for Hope (RFHF) na Bethesda Counsel kwa wake wa marais wa Afrika akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Dk. Denice Nkurunziza, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Mama Mintou Doucoure Epse Traore na Mke wa Rais wa Mali Mama Dk. Malika Issoufou.

Tuesday, March 13, 2012
Mtandao wa Filamu za Tanzania
Karibu katika mtandao wetu unaongelea habari za filamu za Tanzania unaojulikana kwa jina www.filamucentral.co.tz, ! Sasa tupo katika mchakato wa kuandaa tuzo za filamu zitakazojulikana kama Swahili film awards (SFA) Tuzo hizi zinakuja baada ya mafanikio ya tuzo tulizotoa mwaka 2010 zikijulikana kama BORA ZA 2010.
Tuesday, March 30, 2010
Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010 - Mshindi kupata kitita cha Dola elfu 5
Tuzo ya Ousmane Sembene katika ZIFF 2010,Mshindi kupata kitita cha Dola $5,000
Shirika la GTZ likishirikiana na Tamasha la nchi za Jahazi (ZIFF) kwa mara ya tatu tena mwaka huu 2010 watatoa tuzo ya Filamu ya Ousmane Sembene, tuzo hii italenga hasa katika filamu fupi ambazo hazijazidi dakika 20 na ambazo zitakua zimezungumzia au kugusia masuala yanayoikabili jamii ya kitanzania hasa katika mambo ya Ukimwi, Jinsia, Elimu na umasikini.Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 taslimu papo hapo kwaajili ya kumsaidia katika kutengeneza filamu nyingine ama kuboresha kazi zake.Wale wote watakaotaka kushiriki katika tuzo hii wawasilishe filamu zao kabla ya tarehe 30/04/2010 kwa kujaza fomu za kawaida zinazopatikana katika tovuti yetu www.ziff.or.tz
Daniel Nyalusi
Events and Film Program Coordinator
Zanzibar International Film Festival

Subscribe to:
Posts (Atom)