Saturday, November 11, 2006

Anaomba Urafiki wa Kalamu

Huyu kijana (kulia) ni Corey Brown. Ana miaka 27. Ni mtoto wa rafiki yangu Queenae Mulvihill aliyeko Los Angeles. Kama mnakumbuka, Queenae ni mtunzi wa ile sinema Maangamizi. Kwenye hii picha Corey yuko na binamu yake.

Timu ya Maangamizi walivyokuwa Bagamoyo mwaka 1994, walikuwa na Corey. Alikuwa teenager wakati huu. Huenda kuna wanaomkumbuka.

Kwa sasa, Corey amefungwa gerezani huko California, na anatarajia kutoka baada ya miezi kumi na mbili. Kosa lake ni kughushi cheki ya dola mia ($100). Ameniandikia kuniomba kama naweza kumsaidia kutafuta marafiki wa kalamu. Anapenda sana Afrika na Ulaya.

Kama unataka kumwandikia au kumtumia post card kumsalimia anwani yake ni:

Mr. Corey Brown
coc#T-73384
Dorm 5 - Bunk 8
1150 East Ash Street
Shafter, California 93263

Asanteni

9 comments:

Anonymous said...

Da Chemi,Shkamoo!!!
Nakufahamu tangu Bongo. Wewe unifahamu of koz, nilikuwa nakuja Daily News miaka ya 94 kuwacheki rafiki zangu Zeituni na Monica. Nilikua nakuona mara nyingi. Nimefurahi kufahamu blog yako.Sasa hivi nakaa Michigan.Sasa Da Chemi hatuwezi kublog kuhusu uchaguzi wa Marekani kidogo? au hayatuhusu?

Chemi Che-Mponda said...

Hi Subira,

Marahaba. Habari za Michigan? Nitatoa blogu kuhusu uchaguzi. Nilikuwa busy sana wiki iliyopita na tulikuwa na msiba kazini.

Anonymous said...

Da Chemi tuwekee picha za wanao tuwaone.

Anonymous said...

sasa nani atapenda kuwa rafiki na mtu ambaye si mwaminifu?? Huyu jamaa amechoka kiasi hicho mpaka anagushi shilling mia kweli??

Anonymous said...

Angegushi dola milioni moja ungemwona mtu, na kila mtu angetaka kuwa rafiki yake. Kama hutaki kumwandikia usimwandikie mimi nimemtumia post card.

Anonymous said...

Yaani wewe unawa hook up watu wa kwenu na mtu ambaye clearly ana problem! What up with that Chemi??? Mbona nashindwa kukuelewa? Hivi tuseme unaweza kum-hook up na mmoja wa wadogo zako??? I am very confused!! What you problem?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 10:12AM, I have no problem. Lakini, watu wanabadilika. Huyo kijana hakuua wala kumjerehi mtu. Stats za wanaume weusi (incarceration) kuwa jela USA ni kubwa mno. Kosa dogo na unafungwa mara kumi ya mzungu! Namfahamu tokea ni teenager na si mtu mbaya. Na hakuna ubaya kumtumia kadi hata ukitumia ANONYMOUSLY. Si lazima ajue nani katuma. Huko jela pana bore. Kama hutaki kumwandikia si basi, mwingine ataandika. Asante.

Anonymous said...

bado anahitaji marafiki?maana mimi ndio kwanza leo nafungua hii blog.

Anonymous said...

huyo kijana ni muzungu au mbongo?anaongea swahili language?nahitaji kumuandikia