Monday, November 08, 2010

Dr. Aleck Che-Mponda Awania Uspika

Wadau, nimesoma kwenye Michuzi blog kuwa baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda, anawania Uspika wa Bunge. Baba ni mtaalamu wa Political Science na International Relations. Mchango wake katika siasa za vyama vingi Tanzania ni kubwa mno, tuseme watu wamesahau. Katika siasa Tanzania amepitia na kuona mabaya na mazuri. Wishing him all the best.Mhadhiri mstaafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam University na mwanasiasa wa siku nyingi muda mfupi uliopita amechukua fomu za kuwania Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutimiza idadi ya wagombea kuwa 13.

Wengine ni Spika anaemaliza muda wake Mh. Samuel Sitta, Naibu Spika anayemaliza muda wake, Mama Anne Makinda, Mbunge-mteule wa Bariadi-Mashariki, Mh. Andrew Chenge, Mbunge-mteule wa Kongwa, Mh. Job Ndugai, Mbunge wa Afrika Mashariki Mama Kate Kamba, Mbunge wa Viti Maalumu Mama Anna Abdallah na Luteni Mstaafu Benedict Lukwembe.
Wengine ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Saint Augustine University (SAUTI), Bw. Stephen Deya, Mjumbe wa Baraza la vijana mkoa wa Pwani Bw. Mohammed Nyundo, Kada wa CCM Bw. Kazimbaya Makwega, Kepteni Mstaafu Peter Nyalali na Mwalimu wa Shyule ya Sekondari ya Tambaza, Mwl. Salum Kungulilo.

11 comments:

Anonymous said...

Wishing him all the best.

Ali Z. said...

Ehe! Spika itamfaa! Namtakia mafanikio mema.

Malkiory Matiya said...

Tunamtakia kila la kheri Dr. Aleck Che-Mponda katika harakati zake za kuwania uspika. Ni matumaini yetu ya kuwa wasomi watakuwa mstari wa mbele kupiga vita umasikini na ufisadi kwa maslahi ya watanzania wote.

Anonymous said...

Dada Chemi, namfahamu mzee wako miaka mingi. Naona uspika unamfaa sana kama watakuwa fair. Usishangae lakini ukiona wanampuuza maana ndo siasa za Bongo.

Anonymous said...

Kuna kazi kubwa hapo. Hiyo list hasa majina ya awali kiboko pia Old Boys network. Namtakia Mzee Chemponda best wishes.

SIMON KITURURU said...

Kila la Kheri!

emu-three said...

Kazi kweli kweli! Siunajua tena bongo yetu, mzuri anayefaa ni yule 'mwenzetu' ili alinde masilahi `yetu' kwa manufaa `yetu' na watoto 'wetu'. Kama sio mwenzetu hata kama unafaa, utabigwa kikumbo kama hujulikani na hata kutungiwa wimbo wa uwongo kuwa `sio mzawa, au mbongo'
TWAMTAKIA KILA-LAHERI KWANI AKISHINDA NI KWA MANUFAA YA TAIFA KWA UJUMLA!

Anonymous said...

Akishinda itakuwa vizuri sana kwa taifa. Best wishes.

Anonymous said...

nakumbuka alishawahi kuwania tena akapata kura moja, nadhani ilikuwa ya kwake tu. Nadhani kwa sasa atakuwa amejipanga.

Anonymous said...

Chama cha mafisadi kimeshatoa majina 3 ya wanawake tupu Anna Makinda, Cate Kamba Na Anna Msekwa mke wa spika wa zamani.

Anonymous said...

Atawaweza mafisadi?? au naye anataka ajiunge nao?