Thursday, November 25, 2010

Happy Thanksgiving!

Leo ni siku ya Shukurani hapa Marekani. Ni sikukuu ambayo inahusu kila mtu, bila kujali dini wala rangi. Karibu maduka na maofisi yote yamefungwa ila watu wawe na familia zao.

Chanzo chake, wazungu walipotua hapa Marekani, walikufa wengi mno kwa vile hawakujua jinsi ya kulima vyakula vitakayostawi hapa. Yaani walikufa shauri ya njaa! Ni wahindi wekundu waliowaonyesha na kuwafundisha jinsi ya kulima vyakula kama mahindi. Sasa ni siku ya watu kuwa na familia zao na kushukuru.




2 comments:

Anonymous said...

Nashukuru Dada kwa elimu hii nzuri.Sikujua kumbe ni siku muhimu sana.Mdau kutoka Morogoro.

Anonymous said...

Da' Chemi, ulivyosema ni kweli kiasi fulani lakini hii sikukuu imepoteza maana yake kwani kwa wazawa (wahindi wekundu) ni siku ya kukumbuka madhila ya mwanzo wa ukoloni ambao umesababisha tamaduni zao kupotea, ardhi yao kuporwa na hao "wakuja" na hata wengi wao kuuawa. Sasa wenye nchi wamekuwa kama wakimbizi kwenye nchi yao na wengi wao hawasherehekei hii sikukuu.