Tuesday, January 10, 2012

Hasira za Mpangaji - Riwaya Mpya

Mpendwa msomaji;


Baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya uhusiano uliopo kati ya mwenye nyumba na mpangaji, nikianzia Songea 2005 na kumalizia Mwanza 2011, sasa nakuletea riwaya ya kisayansi (science fiction).

HASIRA ZA MPANGAJI ni riwaya iliyotungwa na mimi Gabriel Nombo. Inaelezea maisha ya watu kwenye sayari iliyo nje ya mfumo wa jua, extrasolar planet. Sayari yenye watu wanaopanga na wanaopangisha nyumba kama watu wa hapa duniani.

Tofauti ni kwamba, wao wameendelea zaidi kisayansi na kiteknolojia ukilinganisha na sisi wa duniani.Pia, kwa asili binadamu wa huko (aliens) wana hasira sana. Kwenye nyumba wanazoishi mifarakano ipo muda wote. Kitu kidogo tu, kwa wao, chaweza zua hasira kubwa. Tafadhali usiikose riwaya hii ya aina yake. Ipo njiani kukutembelea.

Kwa maoni au maswali, tafadhali nitumie barua pepe mapigaby@yahoo.com

Gabriel Nombo

No comments: