Monday, January 30, 2012

Je, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe Alipewa Sumu?

Hivi karibuni, Mh. Harrison Mwakyembe alipelekwa kutibiwa nje ya nchi kutokana na ugonjwa wa ajabu aliyopata. Watu wengi walisema kuwa huenda aliwekewa sumu shauri ya maoni yake makali dhidi ya serikali hasa kuhusu mafisadi. Kuna mdau SM ameleta maoni yake.


************************************************
Mh. Harrison Mwakyembe

 NIMESADIKI NA NIMEAMINI MH.DR.MWAKYEMBE ALIWEKEWA SUMU

Ndugu zangu waTz leo hii nimeamini ndugu yetu na mTz mwenzetu Dr. H.Mwakyembe aliwekewa sumu, kutokana na sababu zifuatazo kwa upeo wangu ila simlazimishi mtu yeyote akubaliane na sababu zangu:
A: Mh.Samwel Sitta somo yangu amekuwa akitumia vyombo mbalimbali vya habari km Tv na magazeti kutoa shutuma hizo akiamini ni ukweli bila hata serikali kumunyoshea kidole au kumchukulia hatua yyte huku ikitambua hawa wote ni viongozi waandamizi wa serikali tena katika ngazi za juu za kitaifa, hata leo vyombo vya habari vimemonesha mh.Sitta akisema katika mhadhara wa wakristo mjin Dar, na kwa kujiamini kabisa akitaka mamlaka husika zitoe ripoti ya uchunguzi km  Dr. Mwakyembe hakulishwa sum wamprove wrong.

B: Mh. Samwel Sitta ni rafiki wa karibu sana wa Dr. H. Mwakwembe, hivyo inawezekana kabisa Mwakwembe anamtumia Samwel Sitta na amemwambia ukweli wa tatizo lake ndiyo maana Sitta haogopi kulisemea swala la Mwakwembe kulishwa sumu tena mbele yake yeye Mwakyembe leo alipokuwa anatoa ushuhuda  katika kanisa la ufufuo jijin DSM na Mwakyembe hajakataa kumkanusha Samwel Sitta

C: Dr. Mwakyembe leo amesema katika ushuhuda wake kanisani anatarajia kutembelea makanisa yote nchini ili awaambie wananchi wa kikristo kuwa nguvu za shetani( pengine waliomwekea sumu) zimeshindwa na anazikemea kwa jina Mungu aliye hai, hii inathibitisha kuwa ugojnwa wake haukuwa kwa sabb ya makusudi ya Mungu bali wanadamu mafisadi


D: Leo waheshimiwa kadhaa walikuwa pamoja na Dr. H.Mwakyembe pale kanisani alipomaliza kotoa ushuhuda (testimony) nao wakaanza kusema hawatarudi nyuma katika kutetea wananchi wao waTZ lakini pia hawatakoma kupambana na mafisadi wanaohujumu nchi yetu na rasilimali zake, mh Annakilango Malecela alikuwepo na alisema pamoja na mh.Lembeli

Kwa sababu hizo nimeamini Dr. Hallison Mwakyembe aliwekewa sumu, na ndio chanzo cha matatizo yanayomkabili kamanda wetu mpambanaji, LAKINI kwa nini yeye anatoa habari kwa njia ya mzunguko( indirect) sana? Anyway tuzidi kumwombea naona leo walau ameanza ku-recover taratibu.


Naomba kuwasilisha wadau:

7 comments:

Anonymous said...

Haya mambo ni ruksa kujadiliwa,kwani tayari ameshaweka wazi Dr kuwa alipewa sumu sasa anayezui yasijadiliwe ni nani tena ni mwakyembe ama ni nani huyo?

Anonymous said...

Haya ni maneno ya Mheshimiwa Samweli Sitta aliyoyatoa
kanisani...“Nilishasema na narudia tena alilishwa sumu; mimi nimekuwa
naye muda mrefu akiwa India na madaktari wa kule wanasema alilishwa
sumu, kama wanabisha vyombo vya uchunguzi vitoe majibu haraka,” Chanzo
Tanzaniadaima Jumatatu 30, January 2012.

Kwa kauli hii ya Sitta kama Mwakyembe alikuwa anajua kuwa sitta ana
ongopa kanisani kungekuwa nauwezekano mkubwa wa Mwakyembe kumkanusha
Sitta na kusema ukweli, lakini kwa kuwa alinyamaza na si mara ya
kwanza kwa Sitta kutoa kauli za kwamba Mwakyembe amelishwa sumu basi
kuna jengeka mantiki ya ukweli kwenye vichwa vya wanaofuatilia sakata
lake kuwa ni kweli Mwakyembe kalishwa sumu.

Hii itakuwa ni kashfa nyingine kubwa ambayo itatikisa nchi pale ripoti
ya madaktari itakapo tolewa hasa wafuatiliaji wa mambo watakapo anza
kuunganisha matukio kuanzia pale kwenye mpango wa yeye na viongozi
kadhaa akiwemo Dr Slaa kutegewa mtego wa kuuwawa. Tutashudua mengi
kuelekea 2015

Anonymous said...

Sihamini kama mheshimiwa Sitta anaweza kuongea uongo kanisani, ila namuomba Mheshimiwa Mwakyembe atamke mwenyewe kilicho msibu aki kaa kimya wabaya wake wanaweza kurudia tena mchezo wao mchafu wakihamini kuwa pengine anaogopa kuwataja.
Jimmy.

Anonymous said...

Hakuna kitu cha kuhatarisha usalama kwenye suala la kifo.Wengi wamekufa kwa kupigania haki za watu.Tuna mifano mingi sana katika tanzania hii,eg kifo cha sokoine utata mtupu,kolimba utata mtupu,na wengi wengine.kifo cha sokoine kilitokea baada ya kupambana na walanguzi na wahujumu uchumi,baadae kidogo tukasikia kifo cha ajali,mimi nakumbuka nilikuwa form one,habari hizi zilisika kwa simanzi kubwa kote tanzania.kwa hiyo basi haya sio mageni kwa wenye uchungu na nchii.lakini hata hao wanaofanya haya mabaya wajue yana mwisho wake.

Anonymous said...

Huyu bwana alipewa sumu na waliompa sumu ni mafisadi. Period.

Anonymous said...

matibabu na kubwa maombi yamefanya kazi sio kawaida, Yesu kristo ni kiboko maana biblia inasema hata mkilishwa vitu vya kufisha havitawadhuru, mwakyembe we mshike Yesu sana na maombi kwa sana, maadui zako watajua Yesu ni jina kupita SUMU, UCHAWI, MAJINI n.k

BY MPENDWA

Anonymous said...

Mh! mpaka kufika mwaka 2015 hizi kambi 2 zitatoana roho!