Monday, January 06, 2014

Freddy Macha Atoa Wimbo Mpya!

WASIFU WA MLIMA  KILIMANJARO NA TANZANIA

Mwandishi na mwanamuziki Mtanzania,  Freddy Macha,  katoa video ya wimbo  unaoyasifia mazingira, mandhari, watu,  asilia na uzuri wa Tanzania kupitia mlima Kilimanjaro. Kibao hiki alichokitunga akiishi Brazil (na kurekodi mjini London 2001) kimeshirikisha wanamuziki wa Ulaya, Afrika Mashariki na Kati ambao wengi ni marafiki zake wa karibu sana.
  "Kilimanjaro" ni kati ya nyimbo zinazotazamiwa kufungua kinywa cha Albam mpya ya Macha, baadaye mwakani.
No comments: