Saturday, January 18, 2014

WaAfrika Wawili Wako Katika Orodha ya Waigizaji Bora Mwaka Huu - OSCARS

Wadau, haijwahi kutokea! Waafrika wawili wako katika mashindano ya Oscars mwaka huu!  Lupita Nyong'o kutoka Kenya ameteuliwa katika kundi la Waigizaji Bora wa Kike (Supporting), na pia Kijana Barkhad Abdi kutoka Somalia amaeteuliwa katika kundi la Waigizaji Boara wa Kiume (Supporting). Je, watashinda?

Bi Lupita aliigiza kama Mtumwa katika sinema 12 Years a Slave.  Alikuwa anaigiza katika television ya Kenya. Pia alisoma Uigizaji hapa Marekani katika Chuo Kikuu cha Yale. Alichaguliwa kuigiza katika sinema 12 Years a Slave mara baada ya kumaliza Yale.

Lupita Nyong'o katika sinema 12 Years a SlaveBarkhad Abdi aligiza katika sinema Captain Phillips. Kabla ya kupata nafasi ya kuigiza katika sinema hiyo, alikuwa anaendesha limo huko Minneanapolis, Minnesota.  Barkhad alienda Open Casting Call na kuchaguliwa.  Wadau nikiwaambia muende Open Call, Nenda!

Barkhad Abdi Katika Sinema Captain PhillipsKuona Orodha ya wote walioteuliwa kaitka Oscars 2014 BOFYA HAPA:


2 comments:

Anonymous said...

Wanampendelea yule mzungu Jennifer Lawrence.

Anonymous said...

Naona hapo ndio mwisho wa safari yao. Wamekuwa-nominated lakini hawatashinda tuzo. Kuna ubaguzi sana kwenye hizo Oscars.