Friday, January 03, 2014

Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Kwa Mama Bishanga

HAPPY NEW YEAR FROM MAMA BISHANGA
 
Wapendwa nyumbani TZ natumia nafasi hii kuwatakia heri ya mwaka mpya 2014 uwe wa Baraka na mafanikio kwetu na taifa letu kwa jumla. Nilipenda kuja Tz lakini ndoa imenishika ilibidi mimi na mume wangu tupite juu kwa juu hadi JHB na kurudi Ohio kuchapa kazi, na hali  ya Ohio ndio kama mnavyoiona ni winter kali sana, lakini ndani tulijirusha kama kawaida na mwanangu Kilian na wajukuu Mariam na Lalai Kamota kama mnavyoona,
 
Mwaka uliopita umeisha salama salimini ila tumepoteza watu maarufu akiwemo Tata Mandela baba na babu wa Africa na Tabu ley gwiji katika fani muziki naupenda kule Masasi  mzee Bellim kulikuwa na ile kitu ya kuzungusha mkono na kupiga santuri mama zangu wakicheza na baba yangu aliupenda sana ukawa unaimbwa kila kona na kubakia kichwani kwangu hadi sasa,kwa heshima tuwaombee walale mahali pema peponi, na mwaka uliisha vizuri kwa amani kwa aslimia kubwa ni fahari yetu na haki yetu kudumisha amani na upendo kifamilia na kitaifa. NAWATAKIA KILA LA HERI 2014
 
CHRISTINA I MAROLEN
MAMA BISHANGA
OHIO


Mama Bishanga na Mwanae Kiliana na Wajukuu

No comments: