Saturday, December 26, 2015

Mzee Njemba Atoweka Nyumbani kwake Magomeni, Ndugu Zake Wanamtafuta

Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani)  ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015. 
Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.


No comments: