Saturday, June 04, 2016

City FM Radio Mwanza Kuzindua Kampeni ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

Baadhi ya Wafanyakazi wa 90.2 City Fm Radio ya Jijini Mwanza wakionyesha na vikapu vya asili ambavyo vinapendekezwa zaidi kutumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo mahemezi sokoni ili kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni hatari katika uchafunzi wa mazingira.

Katika kuadhimisha Wiki ya Mazingira ambayo huadhimishwa kila mwaka nchini kuanzia june mosi hadi june 05, City Fm inatarajia kuzindua kampeni ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ijulikanayo kama "My Bag Campaign" ambapo uzinduzi wake utafanywa na maafisa mazingira kutoka halmashauri ya jiji la Mwanza hii leo majira ya saa kumi alasiri katika mtaa wa Market Street uliopo Soko Kuu Jijini Mwanza.

Kulia ni Dj Jakwa wa City Fm akimkabidhi kikapu Mtangazaji wa City Fm katika Kipindi cha The Rock City Rush Hour, Salma Hussein.
Mtangazaji Iman Hezron (kulia) wa City Fm, akimkabidhi kikapu Mtangazaji mwenzake. Wote ni wanatangaza katika kipindi cha The Rock City Rush Hour, Salma Hussein.
Dj Jakwa (kushoto) akiwa pamoja na Iman Hezron (kulia), wote kutoka City Fm Mwanza
City Fm Mwanza imedhamiria kutoa elimu kwa wananchi kuepuka matuzi ya mifuko ya plastiki ambayo yana athari ya kimazingira na badala yake jamii itumie vikapu vya asili na mifuko isiyo hatari katika uchafuzi wa mazingira katika shughuli mbalimbali.
Imeandaliwa na BMG

No comments: