Saturday, June 25, 2016

Wasanii Payus na Mecras wawashukuru Mashabiki Waz wa Kanda ya Ziwa

Msanii Payus kutoka Jijini mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo
Wasanii Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza ambao wanaunda kundi la “Payus & Mecras”, wametoa shukurani zao za dhati kwa wapenzi wote wa muziki ambao wanahakikisha kwamba muziki wao unaziki kuchanja mbuga kitaifa na kimataifa.

Wakiongea na BMG, wasanii hao ambao hivi sasa wameweka kambi mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko ya mwezi mtukufu, wa Ramadhan, wamewashukuru wapenzi wa muziki wao hususani kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambao wameupokea vyema wimbo wao mpya uitwayo “Chausiku”.

“Baada ya kuachia audio na video ya wimbo wa Chausiku, tumepata conection kubwa sana ambapo mashabiki zetu kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamekuwa wakitupigia simu ili tukapige shows huko waliko jambo ambalo tunalifanyia kazi”. Amesema Mecras.

Kupitia BMG, msanii Payus amewahakikishia mashabiki zao kwamba wategemee kazi nyingine nzuri na bora zaidi kuanzia audio hadi video kama ambavyo wamefanya katika wimbo wao wa Chausiku ambao ni wimbo mpya kutoka Mwanza unaopendwa sana hivi sasa.
Msanii Mecras kutoka Jijini Mwanza

No comments: