Saturday, October 08, 2016

Christopher Mtikila, Bado Hajapatikana Mbadala Wako

 
The Late Reverend Christopher Mtikila
CHRISTOPHER MTIKILA BADO HAJAPATIKANA MBADALA WAKO
 
Na Happiness Katabazi

LEO Oktoba 4 Mwaka 2016 , naadhimisha  Mwaka mmoja kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic ( DP) , Mchungaji Christopher Mtikila  tangu alipofariki  kwa ajali ya gari Katika Kijiji cha Msolwa ,Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani ,Barabara Kuu ya Morogoro ,saa 11 alfajiri ya kuamkia Oktoba 4 Mwaka 2015 akitokea Mkoani Njombe Kwenye shughuli za siasa akirejea Dar Es Salaam.

Binafsi urafiki wangu na marehemu Mtikila ulianzia alipoanza kusoma makala na habari zinazohusu habari za mahakamani,siasa nilizokuwa naziandika NA kuchapishwa Katika magazeti Kadhaa nchini.

Mtikila ,Mkewe Georgia na viongozi wa Chama Chake DP, walinipenda sana na Mtikila na Mkewe walinigeuza Kuwa kama binti Yao. 

 Muda  wowote nilikuwa nakwenda nyumbani Kwa Mtikila Enzi zile akiishi lla la Mchikini na hadi alipoamia Katika nyumba Yao Mikocheni nilikuwa nikifika hapo kwake naenda kupiga story na Mtikila na Mkewe tunacheka na Mtikila alipachika jina la ' Mpambanaji' .

Nakumbuka Mtikila yeye alikuwa aogopi mtu Akiamua kuandika Waraka wa kumkosoa,kiongozi yoyote Yule anaingia ofisini kwake ambapo Mikocheni na Ilala alipokuwa akiishi alitenga chumba kimoja kama ofisi ya nyumbani kwake na akawema kompyuta kwaajili ya kufanya kazi zake awapo nyumbani kwake  anaandika waraka mrefu Una maneno makali sana ananiiita niusambaze nami nilikuwa nafanya hivyo .Nilimpenda sana Mzee wangu Mtikila ambaye bado pengo lake halijazibwa  na uenda itatuchukua Miaka Mingi kama  Taifa kumpata mtu wa aina ya Mtikila .

Nikiupeleka waraka wa Mtikila kwa Mhariri ,hataki kuchapisha eti Waraka huo Una matusi hivyo hawezi kuchapa Kwani Gazeti litashitakiwa.Na kweli Mtikila alikuwa aliandika maneno makali Katika Waraka alizokuwa akiziandika.

Kesho yake Mtikila  akiona hakuna gazeti halijachapisha habari yake ,Mtikila ananipigia simu na alikuwa akianza kwa kunisalimia hivi ( Saa ya Ukombozi) minamjibu ni ( Sasa), ananiuliza Hao " wahariri Njaa" kwanini wamekataa kuchapa Habari yake  namweleza Sababu .Mtikila ananiombia  wahariri Hao ni weu wanaho gwa hela na CCM wasitoe Habari zake Kwani eti yeye Mtikila ni Kiboko ya CCM,CCM ina muogopa sana.


Mtikila alikuwa ni mwanasiasa wa aina yake kwani licha ya Kuwa mwanasiasaia alikuwa ni kiongozi wa Kanisa na hakuwa Mwoga alikuwa akisimamia anachokiamini hadi mwisho na hata siku Moja hakuwahi na tabia kama za baadhi ya Vyanzo Vya Habari vingine ambavyo vinakupa  taarifa Fulani ukaandike Kwenye magazeti ,halafu akiona taarifa hiyo amebanwa ,Chanzo hicho kinaibuka na kumkana Mwandishi wa Habari Kuwa hakumpa hiyo Mwandishi wa Habari.Nilimpenda sasa .

Mtikila alikuwa akishavamiwa na polisi nyumbani kwake Ilala mchikichini, Mikocheni  alikuwa akimtaka Mkewe ( GORGIA )  anipigie simu haraka mimi ( Happiness ) ili nifikie eneo la tukio niandike Habari.Na kweli nilikuwa nikifika haraka na kushuhudia Polisi wakiwa wamezingira nyumba yake na Kisha kumkamata kwenda naye Kituo Cha Polisi Kati.

Ndiyo maana nililia sana Mtikila alivyofariki  na ninavyoandika makala hii nakumbuka  vile  vituko vyake,harakati alizokuwa akizifanya za kukuza Utawala wa Sheria ikiwa ni kwa yeye  Kufungua mahakamani Kesi mbalimbali alizoana Haki na Sheria za nchi zimevunjwa ,kufanya mikutano na waandishi wa Habari  kujadili mambo  mbalimbali ya Kitaifa Hali iliyosababisha umma nao kuacha woga nakuanza kuwakosoa viongozi bila woga.

Kama siyo Mtikila na baadhi ya wana mageuzi wengine  kama marehemu Dk.Sengondo Mvungi,James Mapalala, Augustine Mrema,  na wengine Leo hii sisi vijana Tusingekuwa na lakusimulia,au uenda Leo hii  tungekuwa na uwoga kwa Kudai Haki zetu kuikosoa serikali.

Hata hivyo Leo wakati tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo Chako ( Mtikila ) ,Yale maneno yako kuhusu baadhi ya viongozi wenzio Vya vya upinzani Kuwa siyo wapinzani wa kweli ,wanasalitiana na ndiyo maana hukutaka kabisa kujiunga na Umoja wa UKAWA kwasababu unafahamu vyema viongozi Hao wanaounda UKAWA ni wahuni na wasaliti umethibitika Kwani Tayari ndani ya CUF Hali Si shwari wanatimuana ovyo ovyo na hawaamini  tena baadhi ya viongozi kila mmoja anamuita mwenzio ni msaliti.Pia viongozi wa UKAWA wametangaza rasmi kumtenga Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye mara kadhaa ulikuwa ukimpinga Lipumba kuwa siyo mpinzani wa kweli.Hatari sana.

Kwa Sisi wasomi wa Sheria ,Wadau wa Utawala wa Sheria tutamkumbuka sana Mtikila na kuenzi na kuthamini mchango wake wa kushiriki kukuza Demokrasia na utawala wa sheria nchini ikiwa ni pamoja ya yeye Enzi za Baba waTaifa, Julias Nyerere yupo hai ,Mtikila alikuwa akitumia ujasiri wake kumkosoa Myerere,Rais Benjamin Mkapa,Jakaya Kikwete. Enzi walipokuwa madarakani.

Na wakati akiwakosoa,watawala walidai anatoa maneno ya uchochezi serikali ikawa ina mfungulia Kesi za uchochezi pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni.

Enzi za Utawala wa Rais Mkapa, Serikali ilimfungulia kesi za kutoa maneno ya uchochezi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  mfano Kesi maarufu ambazo sisi waandishi wa Habari za mahakamani tuli zibatiza Kesi ya Nyerere. Katika Kesi hiyo Mtikila alipokuwa akihutubia mkutano wake Uwanja wa Jangwani Dar Es Salaam, alisema maneno yafutatayo ( Rais Nyerere ambaye hivi sasa ni marehemu ni Nyamafu na amekwenda Kuzimu).Mtikila alikuwa akitetewa na Marehemu Wakili maarufu Moses Maira. Hii Kesi mwisho wa siku Mtikila aliachiwa huru baada ya Mahakama kuamua kuifuata .

Kesi nyingine ni Mtikila alisema Rais Mkapa siyo Raia wa Tanzania ,Ana ushahidi Kuwa Mkapa ni Raia wa Msumbiji. Mwisho wa siku Mtikila alikuja Kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu.

Ila Kesi ya Kusema CCM ndiyo ilimua aliyekuwa Katibu wa Mkuu wa CCM'  iliyokuwa imefunguliwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Hakimu Gabriel Mirumbe ambaye Kwa sasa ni marehemu mwaka 1999 alimfunga Mtikila Kifungo cha Mwaka mmoja gerezani. Ni Kesi Moja tu Kati ya zote aliziwahi kushitakiwa ndiyo aliyofungwa gerezani Mwaka mmoja .


Enzi za Utawala wa Rais Kikwete ,Mtikila alishitakiwa Mahakama ya Kisutu kwa Kesi ya kumuita Rais Kikwete anagandamiza Ukristo anakumbatia ugaidi ' Kesi hii Mtikila alishinda na hivyo kuachiliwa huru na Mahakama.

Mtikila alifungua Kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kuomba Mahakama hiyo I mpunguzie madaraka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ,aliyopewa katika Kifungu cha 91 ( 1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002. Ambapo Kifungu hicho kinampa mamlaka DPP Kufuta Kesi ya jinai na Hakuna mtu anayepaswa kumhoji.


Septemba 8 Mwaka 2011,  Mtikila, alifungua  kesi ya Kikatiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ,akiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia jengo la Mahakama ya Rufaa lililopo eneo la Kivukoni Front, lisiuzwe kwa mmiliki wa Hoteli ya Kempinski.

Kwa mujibu wa hati ya madai ambayo tayari imeshapewa namba 23 /2011 , Mtikila anamshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria na Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuruhusu jengo hilo la mahakama ya juu nchini liuzwe.

Mtikila amefungua kesi hiyo chini ya ibara ya 27(1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inayosomeka: “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Anadai kuwa amefikia uamuzi wa kuwashtaki walalamikaji hao kwa sababu wadaiwa hao wana dhamana ya kulinda mali za umma zisifujwe lakini cha kushangaza ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kwa kushindwa kulinda jengo hilo ambalo ni mali ya umma na matokeo yake wameshiriki kuharibu mali hiyo ambayo ni jengo la kihistoria.

Hatua hiyo ya Mtikila kufungua kesi, imekuja ikiwa ni siku chache toka Waziri wa Katika na Sheria, Celina Kombani, kuueleza umma kuwa taratibu za kisheria zimefuatwa za kuliuza jengo hilo. Hadi sasa jengo Hilo la Mahakama ya Rufaa halijauzwa.

Mtikila alifungulia Kesi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Aliyekuwa  Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ,Askofu Dk.Valentino Mokiwa kwa kumpapasa Makalio ,Kesi ambayo hadi umauti unamkuta ilikuwa bado haijamalizika.

Mtikila alifungua kesi ya Kikatiba Na.14/2015 Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, kupinga serikali isiwasilishe bungeni muswaada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.Hadi anafariki Dunia  Kesi ilikuwa haijamaliwa na serikali mwisho wa siku serikali ikafuta uamuzi wake wa  muswaada huo bungeni.


Mwaka  2011 , Mtikila  alifungua Kesi ya Kikatiba Katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,Arusha kupinga hukumu Na.45/2009 iliyotolewa na Jopo la Majaji saba wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Katika rufaa hiyo iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza na Mpare Mpoki ambapo Mahakama hiyo ya juu kabisa nchini ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya  Dar Es Salaam Na. 10/2005 iliyokuwa imeruhusu uwepo wa mgombea binafsi  Tanzania.

Hukumu hiyo ya kihistoria ilitolewa na Mahakama ya Haki za Binadamu ,Juni 2013 , Mahakama hiyo ilisema Tanzania inakiuka haki za binadamu kakuzuia uwepo wa mgombea binafsi.

Hakuna  ubishi kwamba hadi Leo tukiazimisha Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mtikila Hajapatikana Mbadala wa Mtikila.Mtikila alikuwa ni Mwanasiasa  wa vitendo yaani Anachukua Hatua za kisheria pindi anapoona au kudhani kuna Sheria na Haki zinavunjwa kwa kwenda Kufungua Kesi mahakamani siyo Kulalamika majukwaani.

Na jinsi Watanzania Wengi tulivyo wanafki tena wazandiki wakubwa Leo hii Mtikila akiwa anatimiza Mwaka mmoja tangu afariki,Hakuna hata Jukwaa Moja liwe la wasomi wa Sheria ,wanasiasa ,wapenda Mageuzi na hata Ofisi ya Vyama Vya Siasa vilivyoandaa hata mdahalo wa Kumbukumbu ya kifo cha Mtikila ambaye ameacha alama Katika siasa za nchi hii na Utawala wa Sheria .

Mtikila kasaulika utafikiri alifariki Miaka 300 iliyopita na wakati wa msiba wake kuna watu wakiwemo viongozi wa kiserikali walitoa Matamko wakisema ama kwa hakika hawatamsahau Mtikila, Na watambuenzi sana .Unafki mtupu.

Sina cha kukupa rafiki Mtikila zaidi ya mimi rafiki yako,mwanao kuendelea kukuenzi kupitia kalamu yangu kwa kuandika makala ili watu waelewe Kuwa pamoja na Vituko vyako ulivyokuwa ukififanya hapa Duniani Ulipokuwa kama mwanasiasa pia ulitoa mchango mkubwa Katika kukuza utawala wa Sheria kwa kutumia Haki yako ya Msingi iliyoainishwa Katika Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo  inasomeka hivi ;

"Kila mtu Ana Haki ,kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria,kuchukua Hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na Sheria za nchi zinalindwa".

Mtikila ni Mtanzania ambaye Tunaweza Kusema ni kama alikuwa ni kinara wa kuliko wa Watanzania wengi kuitumia haki hiyo ya Ibara ya 26(2) ya Katiba ya Nchi kwenda mahakama mbalimbali hapa nchini kufungua kesi .


Mwaka 1993 ,Mtikila alimfungulia kesi ya Kikatiba Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akitetewa na Wakili wa Serikali Kipenka Mussa ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini ,Kesi  Namba 5 / 1993 ambapo Mtikila alikuwa akipinga uamuzi wa kuzuiwa mgombea urais ngazi ya mgombea urais, Ubunge Katika chaguzi za kisiasa ambalo zuio Hilo lilikuja baada ya kufanyika kwa Mabadiliko ya nane ya Sheria ya Katiba ya Mwaka 1992. 

Ambapo  Mabadiliko hayo yalifanyia marekebisho   Ibara ya 39 ya Katiba ya nchi Ambapo Kabla ya Mabadiliko hayo  Ibara ya 39 Ilikuwa ikimtaka mtu yoyote anayetaka Kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima awe ametimiza umri wa Miaka 40 , pia atakawa na sifa ya Kuwa mbunge mjumbe wa Baraza la wawakilizi (Zanzibar).

Hitaji la kisheria la kutaka kila mgombea urais, Ubunge lazima apitishwe na Chama Chake cha siasa wakati wa uchaguzi  pia kimeanishwa katia Ibara ya 67 na 77 ya Katiba ya nchi pia Local council elections of the Local Authorities (Elections) Act, 1979, 
as amended by the Local Authorities (Elections) (Amendment) Act, _ 
(Act No 7 of 1992). 

Mtikila Mbele ya Jaji Lugakingira ambaye ni marehemu kwa sasa alidai Hitaji la linalotaka wagombea wadhaminiwe na vyama vinavunja Ibara ya 21(1) ya Katiba inatoa Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.

Akitoa hukumu yake Jaji Lugakingila alisema kwa mujibu wa Ibara ya 39,67,77 pamoja na Kifungu cha 39 Local Authorities (Elections) Act 1979,alisema ugombea binafsi siyo uvunjifu wa sheria  kwa ngazi ya rais .Hata hivyo Jaji Lugakingira Katika hukumu yake hiyo hakutamka Vifungo hivyo Vya Sheria ni Batili.

Katika rufaa iliyokatwa na Mtikila Na. 10 /2009, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam Mbele ya jopo la Majaji watatu Amir Manento ( Mstaafu ), Salum Massati ( Sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa) naThomas Mihayo (Mstaafu) .

Katika rufaa hiyo Na.10/2009 ,Mtikilia aliwasilisha maombi manne.  Mtikila alikuwa anapinga mabadiliko ya nane ya Katiba ya Katiba na akaomba Mahakama Kuu itamke kuwa marekebisho ya Ibara 39 na 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1979 yaliyoanzisha Sheria Na.34 ya 1994 inavunja Katiba .

Ombi la pili, Mahakama itamke Kuwa mlalamikaji anayo Haki kwa mujibu wa Ibara ya 21(1) ya Katiba ya nchi  Kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mgombea binafsi. Tatu, alipwe gharama za kuendesha rufaa hiyo na mjibu rufaa ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa serikali, Nne, anaomba alipwe nafuu nyingine  ambazo Mahakama itona itafaa.

Hata hivyo  jopo Hilo la Majaji watatu Manento,Massati, Mihayo wakitoa hukumu Yao Walikubali Maombi hayo  ya Mwomba rufaa ( Mtikila ) isipokuwa Mahakama hiyo imelikataa ombi Moja la kutaka alipwe gharama za uendeshwaji wa Kesi hiyo na badala yak e Mahakama ikaamuru kila upande Katika Kesi hiyo ibebe gharama zake.


Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuridhishwa na hukumu hiyo alikataa rufaa Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, na jopo la Majaji saba waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu ambaye kwa sasa ni Mstaafu Augustino Ramadhani , Eusebio  Munuo, January Msoffe ,Nataria Kimaro , Mbarouk Mbarouk, Bernad Luanda, Mjasiri  wasikiliza rufaa hiyo ya Madai 45/2009 dhidi ya Mtikila ambapo Mwanasheria Mkuu wa serikali aliwasilisha hoja Saba za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi Lakini baadae Akaamua kuzifuta Sababu mbili Kati ya Sababu Saba.

Aliyekuwa Mwanasheria wa serikali Katika Kesi hiyo alikuwa George Masaju  ambaye miongoni mwa hizo Sababu alidai  Mahakama Kuu ilikosea kisheria kwasababu ilishindwa kuanisha Yale yanayobishaniwa kwasababu amri ya 15 Kanuni ya 1(5) ya Sheria ya Madai ya Mwaka 2002 inataka  hivyo na kwamba Mahakama ilikosea kuruhusu mgombea binafsi kwasababu kuna mgawanyo wa mamlaka na kwamba Ibara ya 67 (1) (b)  ya Katiba ya nchi inataka mgombea Ubunge yoyote lazima awe ni Mwana Chama aliyependekezwa na Chama cha siasa, hivyo kuruhusu mgombea binafsi wakati Ibara hiyo bado ipo ni kuingilia Mhimili mwingine wa kutunga Sheria ambao ni Bunge.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Ramadhan alisema Mahakama ya rufaa inatengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyoruhusu mgombea binafsi kwasababu Mahakama Kazi yake ni kutafsiri Sheria na siyo kutunga Sheria hivyo suala Bunge ndiyo lenye mamlaka ya kutunga Sheria ya kuruhusu mgombea binafsi na siyo mhimili wa Mahakama.

Nitaendelea kukukumbuka  Mzee wangu Mtikila na kuenzi mazuri uliyoyafanya hapa Duniani na Mabaya sitayafuata. 

Hakika Mtikila pengo Lako bado halijazibwa ,ulikuwa ni mwanasiasa wa vitendo wa kuzungumza unachokiamini  bila woga ,uliipenda Haki na kutetea Utawala wa Sheria ,hukuogopa kushitakiwa ,ukizungumza,ulishitakiwa hukuyumba.Wanafunzi wa Sheria vyuoni  Tunaposoma somo la Constitution Law, Human Rights, International Law basi ni lazima walimu watu take tusome Kesi ya Mtikila One, Mtikila Two na mwisho wa siku wanafunzi wa Sheria wanaishia Kusema Mtikila ameacha alama Katika tasnia ya Utawala Sheria
 

Mungu aiweke roho ya Mtikila Mahali panapostahili .

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
4/10/2016

 

No comments: