Saturday, October 15, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Asindua Meli Mpya ya Kisasa MV Nyehunge 2

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa (Kivuko) ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.

"Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe". Alisema Mongella na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
Mmoja wa watoto akisalimiana na viongozi waliohudhuria uzinduzi wa meli hiyo
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
Mama  Gertrude Mongella (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha, wakati wa uzinduzi huo.


Mama  Gertrude Mongella (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha (kulia), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonard Masale (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo.
"Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe". Alisema John Mongella (katikati) na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohamed (kushoto), alisema Meli hiyo itakuwa mkombozi kwa wasafiri wa Ukerewe ambapo kutakuwa na Meli tatu kwa siku zitakazokuwa zikifanya safari zake za Jiji la Mwanza na Ukerewe huku nauli ikiwa ni nafuu kabisa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, George Nyamala, akielezea umuhimu wa meli hiyo kwa wakazi wa wilaya yake.
Mmoja wa wakazi wa Ukerewe akielezea furaha yake baada ya uzinduzi wa Meli ya Mv Nyehunge II
Mwonekano wa ndani wa Meli ya Mv Nyehunge II
Abiria wakiingia kwenye Meli ya Mv Nyehunge baada ya uzinduzi kwa ajili ya kusafiri kutoka Jijini Mwanza kuelekea Ukerewe.

No comments: