Saturday, October 15, 2016

Safari za Ndege Mpya Aina ya Bombardier Jijini Arusha Kuinua Seukta ya Utallii Nchini

Moja ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier  Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakati maafisa wa Mamlaka ya Anga(TCAA) walipokua wakifanya ukaguzi kabla ya kuanza rasmi safari za kibiashara nchini.
Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)wakilakiwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ukaguzi kabla ya safari kwa ndege hizo kuanza.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ,Ibrahim Mussa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA) akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za utalii zitakazotokana na kukua usafiri wa anga nchini.
  Baadhi ya watumishi wa uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakifurahia ndege aina ya Bombadier baada ya kupata nafasi ya kuingia ndani ya ndege hiyo na kujionea mandhari yake.
  Mkuu wa kitengo cha usalama wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ,John Chaggu akijiandaa kuingia ndani ya  ndege kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi katika viwanja vingine nchini ambavyo ndege hiyo itatoa huduma.
  Baadhi ya wananchi waliokua wakipita kando ya barabara walilazimika kuishudia ndege hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

No comments: