Friday, October 28, 2016

Wapiga Cheni Walalamikiwa Kwa Kuvizia Magari mjini Mwanza

"Kama kuna watu wanajua kuvizia, basi hawa jamaa wa cheni wanaongoza, wanaweza kukuona unaelekea kuegesha gari eneo lisilo sahihi pengine bila kujua, badala wakuambie, wao hujificha na ukiisha egesha gari utaona wanavyolikimbilia". Amelalamika mmoja wa madereva Jijini Mwanza ambaye gari lake limeviziwa na kufungwa cheni na vijana wanaokusanya ushuru wa maegesho.
Na BMG
Kumekuwepo na malalamiko ya mara kwa mara kwamba huenda wakusanya ushuru hao ni kama wamepewa maagizo ya utendaji kazi ikiwemo kuzingatia kiwango cha kukusanya pesa, hali ambayo husababisha watumie njia za kuvizia ili kufikia lengo hilo.
Hapa ni baada ya dereva kusimamisha gari ili kushusha mzigo wake katika eneo la ofisini, wazee wa cheni wakatimba bila kujua wametokea wapi.
Zoezi likawa gumu kwa wapiga cheni baada ya kulalamikiwa sana.
Mmoja wa watu waliosadikika ni kiongozi wa wakusanya ushuru wa maegesho Jijini Mwanza, akipiga simu kwa mtu ambaye hakujulikana mara moja kufuatia watu wengi kulalamikia utendaji kazi wa wapiga cheni hao.

No comments: