Showing posts with label Bibi Arusi. Show all posts
Showing posts with label Bibi Arusi. Show all posts

Saturday, November 02, 2013

Fesheni Mpya ya Picha za WanaHarusi Bongo

Wadau, naomba maoni yenu kuhusu hii picha. Mimi nasema Tarzan angefurahi sana kuona wanaharisu kwenye miti! Bibi harusi alipandaje na hiyo gauni na heels?

Tuesday, September 17, 2013

Mfalme Mswati Kuoa Mke wa 14!

Huyo Binti akishika mimba ndo ruksa Mfalme kuoa. Duh! Mila zingine.   Mchumba ana miaka 18.

********************************************************

 MBABANE - Swaziland’s King Mswati III has chosen an 18-year-old beauty pageant contestant as his 14th wife, a palace spokesman said Tuesday, days before a much-criticised parliamentary vote. ”I can confirm that the king has introduced to the nation a new liphovela (royal fiancee),” said Ludzidzini palace governor Timothy Mtetwa. Mswati, a 45-year-old who is sub-Saharan Africa’s last absolute monarch, introduced Sindiswa Dlamini at a Reed Dance celebration over the weekend, Mtetwa told AFP. She wore reed feathers on her head — a sign of royalty.

The young woman graduated from Mbabane’s St. Francis High School last year and is a finalist in the Miss Cultural Heritage beauty pageant. The winner will be announced on September 28. The king has come under fire for his household’s lavish lifestyle while the tiny mountain kingdom’s 1.2 million people struggle to make a living. – AFP.

 Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

King Mswati III

Tuesday, May 21, 2013

Kwa Nini Bibi Harusi Hulia Siku ya Harusi?


Swali uliulizwa:

Hawa najiuliza, kwanini mabibi harusi wengi wanapenda kulia siku ya ndoa?

1. Jee! Ni uchungu au furaha kwa kupata mume?

2. Ni uchungu au kufaraha ya kuondoka mazingira ya nyumbani kwao?

3. Ni furaha ya kwenda kuanza kumiliki kitanda na mumewe mfululizo na
kwa muda anao upenda (lile tendo)?

3. Au wanaogopa fedheha kwa kuwa wanaolewa /anaolewa akiwa si bikra?

4. Ni uoga wa kuanza kulala bila nguo ya ndani akiwa kwenye ndoa na mumewe?

Kwa nini mabibi harusi wengi huangua vilio?!
Dada Leila Sheikh kajibu hivi:
Kwetu sisi uswahilini usipolia wafinywa na kungwi.
Seriously huwa tunalia kwa sababu tunaondoka kwa wazazi wetu na kwenda kujiunga na koo jingine.
huwa tunafundwa- "Mama Mkwe ndiyo Mama Yako sasa. Ba Mkwe ndiyo Baba Yako kuanzia leo. Hawa usiwachukulie kama mawifi au mashemeji bali ndiyo ndugu zako kuanzia leo. Mume akiwa kachacha, gongesha vikombe majirani wafikiri munakunywa chai kwa bajia. Chakula kikikosekana, hakikisha unachoma iliki ili majirani waamini unapika pilau. Mume akichelewa kurudi, mlaki mlangoni kwa tabasamu. Akikukaripia, mwimbie wimbo wa mapenzi "Sabalkheir (ishakuwa asubuhi anaporudi) Mpenzi, waonaje hali yako?".
Na kwa nini nisilie baada ya kuambiwa hivyo?Unaondoka kwenu ulipodeka wenda ugenini.
Leila Sheikh

Tuesday, September 27, 2011

Kitchen Party Boston

Wadau, wikiendi iliyopita tulimfanyia 'Kitchen Party' mwali, Musau, mtoto wa Dada Margaret Kabula wa Boston. Anaolewa mwezi ujao hapa Boston.

Kwa vile watu waliomba nyuso zao zisitoke kwenye blog nabandika zilizokuwa blurred.

Hapa tuko kwenye Mdundiko Mwali yuko kwenye stool

Hapo nakatika kidogo

Mwali akifundwa

Hapo mambo nyeti

Mdundiko unakolea

Mwali akipewa somo kiboko