![]() | ||
Haya jamani, kwa nini mnapoteza kununua nguo za harusi wakati mnaweza kusevu pesa kwa kufunga mkiwa uchi? Hao wazungu walisema hela ya nguo watatumia kwa ajili ya kulipa mortgage ya nyumba! Ingekuwa safi kama wageni nao wangekuwa uchi. Kutoka https://www.facebook.com/pages/Ijebu-News-Xtra/121224847988714?fref=photo |
Tuesday, September 07, 2010
Dr. Slaa Afunguliwa Mashitaka Mahakama Kuu!
Jamani, sasa badala ya kuwa kampeni ya siasa, ugombea rais wa Dr. Wilbrod Slaa wa chama cha CHADEMA, unageuka kuwa Soap Opera (Tamthiliya)! Majuzi huko Babati walimwuliza Dr. Slaa ana wake wangapi(BOFYA HAPA kupata maelezo zaidi), leo eti mume halali wa mke wa Dr. Slaa, kaenda mahakamani na kusema kuwa Dk. Slaa kamwibia mke wake! Kusoma habari zaidi za kesi BOFYA HAPA.
Huo mchezo wa kukuchunguza mpaka umevaa chupi gani kama ni mwanasiasa ni mchezo mkuu hapa Marekani. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe msafi. Kwa maana hiyo usitembee nje ya ndoa, usiwe na kimada, usizae nje, usifanye ngono na malaya... listi ni ndefu. Bado wanafanya na wakigundulika wengi wanalazimishwa kujiuzulu.
Enzi za Mwalimu ulikuwa husikii kwenye vyombo vya habari kiongozi fulani anatembea na fulani! Sasa ni jambo la kawaida, sijui ndo uhuru wa vyombo vya habari au nchi kukua kisiasa. Wangekuwa wanasema mambo ya watu enzi za Mwalimu mbona yangesemwa mengi. Ungesikia fulani kazaa katika kila mkoa wa Tanzania, fulani ana familia nyingine sehemu fulani, binti fulani katoa mimba ya kiongozi fulani n.k. Sidhani kama kuna kiongozi 'msafi', hata kwa upande wa wanawake! Kiongozi fulani kazaa sehemu fulani, kiongozi huo kapata ugonjwa fulani mahala fulani.....Doh! Tunaelekea wapi?
Mwisho nauliza kwa nini wanamsakama Dk. Slaa sasa? Naona kampeni yake imepamba moto kweli halafu ndo jamaa anataka alipe eti mabilioni!
Friday, June 19, 2009
Arusi Inapovunjika Dakika Za Mwisho

Kutoka ippmedia.com
Na Da Flora Wingia
Zipo harusi zingine ukisimuliwa mikasa yake utadhani ni sinema za kuigiza. Pilikapilika nyingi tokea uchumba, maandalizi ya harusi zenyewe lakini katika kuhitimisha ndoa hazifungwi. Kulikoni?
Hivi majuzi nilikuwa sehemu katika kikao fulani cha harusi. Ni eneo linalotizamana na barabara kubwa iendayo Bagamoyo. Kabla ya kikao, ukapita msafara ambao tulidokezwa kuwa ni wa Kitchen Party.
Kitchen Party ni tafrija ndogo inayotangulia send-off kisha baadaye harusi. Tafrija hiyo inalenga kumfunda bibi harusi mtarajiwa kabla ya kuanza maisha ya ndoa na mumewe.
Naam. Mimi nikasema, “hayo ni maandalizi ya harusi bila shaka…siku hizi upo msemo kwamba wanaooa au kuolewa miaka hii wanapeleka matatizo nyumbani”.
Baba mmoja aliyeketi pamoja nami akadakiza; “umesema ukweli, harusi za siku hizi si lolote si chochote, gharama kibao lakini muda si mrefu wanaachana”.
Baba mwingine bila kuchelea akasema, “Ngoja niwasimulie ndoa moja iliyovunjika dakika za mwisho na kuacha wengi midomo wazi. Ilihusu jamaa yangu mmoja.
Katika simulizi yake akasema kuwa yupo kaka mmoja ambaye ni jamaa yake alipania kumuoa mwanamama fulani. Maandalizi yakafanyika kuanzia kitchen Party, na send-off vyote vikafanyika.
“Maandalizi ya harusi yenyewe yaligharimu shilingi milioni 18,” kwa mujibu wa baba huyu. Kila kitu kikawa tayari ikabakia kwenda kanisani ili ndoa ifungwe.
Siku ya harusi, bibi harusi akapelekwa saluni kutengenezwa na kuvalishwa.
Bwana harusi naye akapelekwa kuandaliwa. Wageni waalikwa, ndugu na marafiki wakawahi kanisani.
Alivyoeleza baba yule ni kwamba muda wa kwenda kanisani ulipokaribia, ilitakiwa bwana harusi na mpambe wake waenda kumfuata bibi harusi ili kwa pamoja waweze kwenda kanisani.
Lakini ajabu ni kwamba bwana harusi alijaribu kumsaka aliko mkewe mtarajiwa bila mafanikio. Walipokwenda saluni alikopambiwa aliambiwa kuwa yuko jamaa aliyekuja kumchukua na gari lililokuwa limepambwa vilivyo.
Kule kanisani wageni waalikwa pamoja na mtumishi wa Mungu aliyejiandaa kufungisha ndoa ile wakawa wanasubiri kwa muda mrefu wasijue kilichotokea.
Mwishoni wote wakakata tamaa na kutawanyika kurejea kwenye sherehe za harusi kujua kulikoni.
Kumbe baadaye akabainika kuwa yule jamaa aliyekwenda kumchukua bibie pale saluni alikuwa mpenzi wake wa zamani na hivyo kwa pamoja walitorokea kusikojulikana. Inaonekana bibi alikuwa anampenda aliyemtorosha kuliko yule waliyetaka kufunga ndoa naye.
Swali ni je, kwanini mwanamama huyu hakuwa wazi mapema kwa kueleza bayana kwamba bwana harusi yule mtarajiwa hakumpenda bali alikuwa na mwandani wake mwingine?
Hiyo ingesaidia mambo mengi pamoja na kuzuia gharama za maandalizi, usumbufu wa watu waliochanga fedha zao, wakaenda hata kanisani lakini harusi haikufungwa. Ama kwa hakika Maisha Ndivyo Yalivyo.
Ndoa zingine ni vurugu tupu. Usione watu wamesimama mbele ya mashekhe au pale madhabahuni huku maneno mazuri yaliyojaa upendo na matumaini yakiwatoka vinywani. Wengine ni usanii mtupu kama siyo unafiki.
Katika nafsi zao bado wanawakumbuka wapenzi wao wa zamani. Pale altareni inakuwa ni kuthibitisha tu kwamba eti nao wameoa au wameolewa kwa kufunga ndoa takatifu. Kumbe wakishatoka pale, mawasiliano na wachuchu wa zamani yanaendelea kama kawaida.
Matokeo yake ndiyo hayo tunashuhudia kuchipuka kwa nyumba ndogo au wengine wakikufuru zaidi huachana na wenzi wao au kutafuta visingizio ili ndoa zivunjikie mbali.
Haya siyo maisha bali ni kuongeza majanga ya kifamilia. Nyumba moja inakushinda sembuse nyumba mbili au tatu? Sijui labda niseme ‘mwenye nguvu mpishe’ lakini madhara yake hayako mbali.
Msomaji wangu nikuachie nawe uchangie mawazo tuweze kusonga mbele kwa pamoja. Kama unacho kisa unadhani tunaweza kujadili kwa pamoja usisite kuniandikia kupitia email hii hapa chini.
fwingia@yahoo.com
Wasalaam

Wednesday, September 10, 2008
Ajali ya Gari Dar - Wapambe wa wanaarusi wafariki!
Jamani mmetoka kusherekea arusi halaffu kitu kama hii kinatokea. Mungu awape nguvu hao wanaarusi maana lazima marehemu ni ndugu au marafiki wa karibu. Nawapa pole maana ni njia mbaya sana ya kuanza maisha ya ndoa. Leo mnasherekea arusi kesho kilio. Jamani!
*******************************************************
Kutoka IPPMEDIA.com
Ajali mbaya Dar!
2008-09-10
Na Moshi Lusonzo, Jijini
Watu wawili wanaotajwa kuwa ni wapambe wa maharusi wamefariki dunia huku wengine kadhaa wakiwemo bwana na bibi harusi kuumia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuvaana na lori la mizigo.
Tukio hilo la kusikitisha, limetokea hivi karibuni, katika eneo la Ubungo ambapo gari lililobeba maharusi na wapambe wao lilipoteza muelekeo na kulivaa lori la mizigo kwa mbele kabla ya kupinduka.
Wakizungumza na Alasiri, baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo dereva wa lori la mizigo lililogongwa kwa mbele, Bw. Juma Gwao, 38, wamesema tukio hilo lilijiri mishale ya saa 7:00 usiku.
Wameeleza mashuhuda hao kuwa mara tu baada ya ajali hiyo, bwana na bibi harusi walijeruhiwa na kukimbiziwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, huku wapambe wawili kati ya wale walioambatana nao wakifariki dunia papo hapo.
Akisimulia zaidi ajali hiyo, dereva Gwao ambaye bado amelazwa wodi 17 ya Jengo la Sewahaji pale katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili, MOI, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari lililobeba maharusi na wapambe wao kushindwa kuumiliki vyema usukani wa gari na kusababisha aajali ya kugongana uso kwa uso.
Akiasema Gwao kuwa wakati ajali hiyo ikitokea, yeye alikuwa akiendesha gari lake lenye namba T 908 aina ya Fuso, akitokea Ubungo kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuchukua shehena za mizigo.
Akasema wakati akiwa ndio kwanza anaianza safari hiyo eneo la Ubungo, ghafla likatokea gari aina ya Canter ambayo ilibeba maharusi pamoja na wapambe wao kibao.
Akasimulia dereva Gwao kuwa pamoja na kujitahidi kukwepa, bado gari hilo lilimfuata aliko na kuigonga gari yake kwa mbele na kisha kupinduka.
``Nadhani dereva mwenzangu alishindwa kuhimili usukani... kwani licha ya kujitahidi kumkwepa, bado alinifuata niliko na kuigonga gari yangu kwa mbele,`` akasema Gwao.
Shuhuda mwingine akasema mara tu baada ya ajali hiyo, wapambe wawili waliokuwa wakiwasindikiza maharusi hao wakapoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa na kukimbiziwa Muhimbili.
Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Almas Jumaa, amesema ukiacha dereva Gwao, majeruhi wengine wote wa ajali hiyo walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi makwao.
Akaeleza vilevile kuwa hadi sasa, majeruhi Gwao ambaye ni pekee aliyelazwa hadi sasa, angali akiendelea vyema na matibabu na tayari ameanza kupata nafuu kubwa, ukilinganisha na hali aliyokuwa nayo wakati akifikishwa hospitalini hapo.
SOURCE: Alasiri

Wednesday, September 03, 2008
Bibi Arusi ni....Khadija Kopa! Anameremeta!

Malkia wa mipasho, Khadija Kopa ameolewa!
Hebu wapashe dada! Ulipendeza sana siku ya arusi.
Picha kutoka Michuzi Blog.
Tuesday, September 02, 2008
Bwana Arusi achinjwa Dar
Jamani, mbona mauaji yanazidi Dar? Wivu kitu kibaya sana. Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.
***************************************************
Kutoka ippmedia.com
Bwana harusi Dar achinjwa!
2008-09-02
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa mbioni kufunga ndoa wiki hii ameuawa kinyama baada ya kuchomwa kisu na kisha mwili wake kukutwa kandoni mwa barabara.
Taarifa ambazo Alasiri imezipata toka kwa baadhi ya waliodai kuwa ni mashuhuda wa tukio hilo, zinadai kuwa tukio hilo limejiri mishale ya saa 4:00, usiku wa kuamkia jana na kwamba marehemu ametambuliwa kwa jina la Nassoro Shomari.
Taarifa hizo zinadai kuwa bwanaharusi ni dereva taksi aliyekuwa akifanya shughuli zake katika Kituo cha Sinza Madukani Jijini.
Wanadai mashuhuda hao kuwa mwili wa bwanaharusi huyo mtarajiwa ulikutwa katika eneo la Tandale, kandoni mwa njia ya kuelekea Kijitonyama.
Aidha, taarifa hizo zinadai kuwa mmoja wa wale wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya dereva taksi huyo ni mwanamke mmoja aitwaye Aisha, anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa zamani wa marehemu.
Wakieleza zaidi, wanadai wasimuliaji kuwa chanzo cha kuuawa kinyama kwa dereva taksi huyo ni kisa cha kimapenzi, hasa kutokana na ukweli kuwa wiki hii alikuwa afunge pingu za maisha na mwanamke mwingine na kuwatosa wengine aliowahi kuwa nao hapo kabla.
Wanadai wasimuliaji kuwa kabla ya uamuzi wake wa kutangaza ndoa, marehemu aliwahi kuwa na uhusiano na mwanamke mmoja pale Tandale, jirani na njia ya kuelekea Kijitonyama.
Wanadai kutokana na utamu wa penzi lao, marehemu akafikia mahala pa kujifunga mbele ya mwanamke huyo, kwa ahadi kwamba atamuoa.
``Na tena ndiye aliyempangia chumba hapo Tandale... na alikuwa akimhudumia kwa kila kitu kiasi kwamba mwanamke wa wenyewe alijua kuwa yeye ndiye yeye tu... hakuna mwingine zaidi yake,`` akadai mmoja wa wasimuliaji.
Inadaiwa kuwa licha ya kuwa na ahadi ya kumuoa mwanamke huyo, marehemu alikuja kughairi na badala yake akatangaza kufanya mipango ya ndoa na mwanamke mwingine.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa zikiwa zimebaki siku chache kabla ya harusi yake wiki hii, ndipo marehemu alipochepuka kidogo na kwenda nyumbani kwa mpenziwe wa zamani.
``Akiwa huko, haieleweki ni kitu gani hasa kilimkuta... lakini mwili wake ukakutwa kandoni mwa njia ukiwa umechomwa visu,`` akadai mmoja wa watu waliodai kuwa ni mashuhuda.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni hakupatikana ili kuzungumzia tukio hilo la kusikitisha.
Baadhi ya maaskari polisi wameiambia Alasiri kuwa ni kweli kuna tukio la mwanaume kuuawa kwa kuchomwa visu, na ambalo limejiri mishale ya saa 4:00, usiku wa kuamkia jana.
Hata hivyo, wamesema mwanaume huyo ni dereva wa daladala aina ya DCM linalofanya safari kati ya Mbagala na Sinza, likiwa na namba za usajili T 223 AUS.
Wanadai askari hao kuwa juhudi za kumsaka mtuhumiwa Aisha zinaendelea, kwani anadaiwa kutimka baada ya kujiri kwa tukio hilo.

Thursday, July 24, 2008
Tuesday, June 17, 2008
Mr. Sulu anaoa!

Wapenzi wa Star Trek, hatimaye mcheza sinema, George Takei, (71) maarufu kwa kuigiza kama Mr. Sulu anaoa...bibi arusi ni mwanaume mwenzake! Anamwoa mpenzi wake wa siku nyingi Brad Altman (54).
Kama hamkujua Takei alijitokeza mwaka juzi na kusema yeye ni shoga. Tangu leo asubuhi huko California ni ruksa kwa wapenda jinsia moja (wasenge na mashoga) kufunga ndoa. Wanasema yeye alikuwa wa kwanza kuchukua kibali kwenye mji anayokaa, West Hollywood.
Jimbo la California sasa ni la pili nyuma ya Massachusetts nchini Marekeni kuruhusu mashoga kufunga ndoa.
Kwa habari zaidi someni:
Subscribe to:
Posts (Atom)