(kutoka kushoto, Emmuel Myamba, Mimi, Steven Kanumba)
Hii picha nilipiaga mwezi wa saba mwaka jana Bongo. Tulikuwa Magomeni, Dar es Salaam kwenye shoot ya filamu Bongoland II siku ya kwanza. Bongo Superstars Steven Kanumba na Emmanuel Myamba walikuja kututembelea kwenye seti. Sikujua kuwa huyo Emmanuel naye ni actor alielekea mpole kweli.
Nimebahatika kuona sinema ya Fake Pastors. Mle Emmanuel anaigiza kama Evangelist wa kanisa. Kwa kweli ana kipaji cha kuigiza yaani kama kuna tuzo ya Best Supporting Actor Bongo, anastahili yeye. Anaigiza vizuri mno mpaka wewe mtazamaji unasema unataka kumwona zaidi na zaidi. Unaamini kabisa kuwa huyo ni Evangelist anayependa kanisa lake, dini yake na waumini wake. Haonekani kama anaigiza hata kidogo. Natabiri ataenda mbali sana katika fani ya uigizaji na si Bongo tu hata nje ya nchi. Sinema ya Fake Pastors ina kasoro zake lakini huyo jamaa ni nyota!