Showing posts with label Martin Mhando. Show all posts
Showing posts with label Martin Mhando. Show all posts

Sunday, July 10, 2016

MAANGAMIZI: THE ANCIENT ONE - Sinema ya Kwanza ya Tanzania Kwenda Oscars!

   Hii ni sinema ya kwanza kutoka Tanzania kushindana katika Academy Awards (Oscars)!

Thursday, June 05, 2014

Lupita Nyong'o atakuwa ZIFF

*Geneviveve Nnaji na John Dumelo nao ndani

*Habib Koite, Didier Awadi kuburudisha

*Filamu ya Mandela kufungua pazia

DSC_0021

Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Tamasha la Filamu la nchi za Majahazi la 17 maarufu kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF). Kulia Msaidizi wa Kitengo cha habari ZIFF, Lara Prieston, Kushoto ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean), Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa "Has T" (wa pili kushoto) na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (katikati). Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog

Na Andrew Chale

DUNIA inatarajia kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ndani Mji Mkongwe wa Stone Town, Unguja, kwa watu wa mataifa yote watakapoungana na kushuhudia ‘Hatma ya Pamoja’ (A common Destiny) Juni 14 hadi 22, 2014, katika Tamasha la Kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF).

Tamasha hilo maarufu kama filamu la nchi za Majahazi ZIFF, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 17, tokea kuanzishwa kwake.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, kwenye halfa maalum ya uzinduzi wa tamasha hilo la 17, kwa wandishi wa habari iliyofanyika Goethe Institut kituo cha utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, alisema tamasha hilo msimu wa mwaka huu linatarajiwa kuwa moto kwani linakuja na mambo mbalimbali yenye kuleta mabadiliko ya hali ya juu.

Ni kutokana na mabadiliko hayo, Profesa Mhando anasema tasnia ya filamu kwa Tanzania inahitaji kubadilika ikiwemo wasanii wenyewe kujituma na hata kuingia darasani ili kufanya kazi zenye uhakika.

Akimaanisha kila msanii wa filamu aweze kufikia malengo yake, hana budi kujifunza na kushirikisha wale waliotangulia katika tasnia hiyo.

Anazungumziaje kaulimbiu ya ‘A Common Destiny’

Prof. Mhando amesema kauli mbiu ya mwaka huu yenye kusema Hatma ya pamoja yenye maana ya ‘A common Destiny’, ina lengo la kuwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja na kufurahia kwa pamoja ikiwemo kubadilishana mawazo kwa pamoja kwa tasnia ya filamu, muziki, kwa mlengo ya kujenga.

“Tukiwa na haja moja, kuishi kwa amani na kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kifikira na maendeleo kwa amani, ZIFF kwa kutumia dira hiyo hasa kupitia filamu zetu za ndani zenye mchanganyiko wa utamaduni na asili yetu.

“Wazanzibari na hata wageni watakaoshuhudia filamu hizi wataweza kuchukua utamaduni huo na kuupeleka nje kwa furaha kubwa katika kufikia hatma ya pamoja” amesema Prof. Mhando.

DSC_0082

Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.

Lupita-Nyong-o-729-620x349

Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba

Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa kwenye viunga vya Zanzibar na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.

Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.

Prof. Mhando amesema tayari wazazi wote wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo huku Lupita mwenyewe akiahidi kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo katika utoaji wa tuzo kama ratiba za shughuli zake hazita mbana.

Prof. Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa kujulikana na baadaye alienda kusoma zaidi masuala hayo ya filamu, ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama Volunteer.

Mara nyingi staa huyo amekua akihudhuria matamasha na halfa mbalimbali za utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku akiwa ameambatana na wazazi wake wote wawili.

Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia filamu ya ‘12 Years a Slave’ pia filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali zikiwemo: tuzo ya Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji bora wa kike aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild Award’, ‘NAACP Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film Critics Association Award’, na nyingine nyingi.

Genevieve-Nnaji-Cover

Genevieve Nnaji.

Mbali na Lupita, katika kuongeza utamu wa tamasha hilo, mastaa wengine nguli wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa kuwapo katika ushuhudiaji wa utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji na mwanamitindo nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji.

Wengine ni Amr Waked (Misri), Faouzi Bensaidi (Morocco), Nadia Buari, Richard Mote Damijo ‘RMD’, John Dumelo, Desmond Eliot na Florence Masebe.

DSC_0067

Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na Filamu iliyopewa jina la "Women with Altitude" iliyoandaliwa na WFP ambapo ndani yake imeshirikisha wanawake wa kitanzania watatu waliofanikiwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa wameambatana na wenzao nane kutoka Nepal na kuzungumzia changamoto mbalimbali wakati wa kupata elimu na maisha kwa ujumla itakayoonyeshwa kwenye tamasha hilo tarehe 17/6/2014 saa 19:15 jioni ukumbi wa Old Fort visiwani Zanzibar.

Filamu ya Mandela kufungua pazia

Jumla ya filamu 79, kutoka mataifa mbalimbali zinatarajiwa kuonyeshwa huku filamu iliyoingia kwenye tuzo za Oscar, ya Mandela: ‘A Long Walk to Freedom’ ndiyo itakayofungua pazia kwenye tamasha hilo, Juni 14.

“Katika filamu hizo 79 za kimataifa zitaoneshwa ZIFF, nyingi zikiwa zinatoka katika nchi za Kiafrika na filamu ya Mandela imepata bahati ya kuwa ya ufunguzi”, amesema Profesa Mhando.

Pia Profesa Mhando amesema kuwa zitakuwepo filamu zinatoka katika nchi 35 zikiwemo filamu fupi 38, filamu ndefu za kuburudisha 24 na makala 17.

DSC_0137

Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi "Dean" akionyesha kitabu chenye ratiba nzima ya tamasha hilo litakalorindima visiwani Zanzibar kuanzia Juni 14 hadi 22 mwaka huu.

Burudani zitakazopamba

Kwa upande wake, Edward Lusala anayeshughulikia muziki kwenye tamasha hilo la 17, anasema kuwa, wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake ambayo itaacha historia kwa mwaka huu.

Lusala amesema jumla ya makundi 18 yanatarajiwa kutumbuiza. Huku kwa wasanii gwiji wakiwemo pia Didier Awadi kutoka nchi ya Senegal na Habib Koite (Mali) wanatarajiwa kuja kuishika Zanzibar na viunga vyake.

“Wasanii Koite na Didier ni miongoni mwa wasanii wakubwa sana na wenye heshima kubwa hasa kwa muziki wao kwani wanapiga kimataifa hasa katika matamasha makubwa na wamekuwa wakipiga miziki ya kipekee. Hivyo watu wote watafurahia” amefafanua Lusala.

Ameongeza kuwa, wasanii wengine ni pamoja na Farid Kubanda ‘Fid Q’, Ambwene Yesaya ‘ Ay’, Sauti Soul, Mzungu Kichaa, Ras Inncent Nganyagwa, Grace Matata na wengine wengi ambao watatoka Tanzania.

Na kuongeza kuwa kwa sasa AY yupo nchini Malawi akijifua na moja bendi maarufu ya muziki wa Live ambapo anatajiwa kukaa jukwaani kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu huku akiimbaLIVE.

Pia vikundi vya muziki nguli toka Tanzania, Egypt, Kenya, Uganda, Malawi na Afrika ya Kusini vitatumbuiza kila siku katika tamasha hilo.

Aidha, Lusala amesema kuwa, kwa mwaka huu wanatarajia kufanya ‘surprise’ kwa kumleta msanii mkubwa ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na msanii huyo kutoka Afrika kusini.

Kwa upande wake Meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi amewataja wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja mdhamini mkuu ZUKU Pay tv, huku wengine ni Ethiopian Airlines, Tanzania Media Fund TMF, ComNet, Cello, Air Uganda, Gina Din, FASTJET and United Petroleum. Wengine ni shirika la Rosa Luzemburg Foundation, Arterial Networking, Steps International, Azam marine, Prime Time Promotions, Goethe Institut na wengine wengi.

ZIFF moja kati ya matamasha ya filamu makubwa duniani hukutanisha wadau katika tasnia ya filamu. Wakiwemo waigizaji wa siku nyingi na maarufu, waongozaji, waigizaji wachanga na wanafunzi kutoka ulimwenguni kote

DSC_0119

Meneja wa Biashara wa shirika la ndege la Fastjet, Jean Uku akizungumzia udhamini wao kwenye tamasha hilo ambapo wametoa tiketi za safari ya washiriki kutoka Afrika Kusini watakaoshiriki kwenye tamasha hilo.

DSC_0084

Msanii wa Hip Hop, Harry Kaale kutoka kundi la One "The Incredible" akielezea namna watakavyotoa burudani na elimu kwa vijana kwenye tamasha hilo.

DSC_0105

Msanii Mzungu Kichaa akiwashukuru ZIFF kwa kutoa nafasi kwa wazalendo kuonyesha vipaji vyao kwenye tamasha la ZIFF.

DSC_0108

DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto rico akisisitiza kutoa burudani ya aina yake kwenye tamasha hilo.

Thursday, July 02, 2009

Danny Glover Awasilli ZIFF

Danny Glover akiongea na Martin Mhando

Kutoka LUKWANGULE BLOG:

Danny Glovver Atua Uwanja wa Zenj

Muigizaji maarufu wa Hollywood na ambaye pia ni balozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Kuhudumia watoto(UNICEF) danny glover amewasili mjini Zanzibar leo majira ya alasiri na kusema ziara yake nchini itasaidia kujenga mahusiano zaidi kati ya Wamarekani weusi na ndugu zao wa Afrika.

Muigizaji huyo alisema hayo akiwa uwanja wa ndege wa zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema pamoja na kuwa balozi wa uNICEF na kupeleka salamu za UNICEF maeneo anayotembelea pia ana shirika lisilo la kiserikali ambalo hushughulikia mahusiano na nchi za Kiafrika hasa kudumisha utamaduni ulipo wa miaka mingi kati ya wamarekani weusi na ndugu zao waliopo bara la Afrika.

Amesema katika kuimarisha uhusiano huo anajikita zaidi katika mawasiliano na kunyambua tamadunia mbzo anaona ndio ufunguao wa mahusiano kati ya Afrika na bara la Amerika.
Glovver ambaye atakuwa nchini kwa siku tano anatarajiwa pia kushiriki katika masuala mbalimbali ya tamasha kuwa na mahojiano na vyombo vya habari na kufanya shughuli za UNICEF ikiwa ni pamoja na kumuona Rais wa Zanzibar, Abeid Aman karume.
Pia akiwa hapa atashiriki katika kongamano la watoto na amani linaloandaliwa na GNRC na na kuzungumza na watengeneza sinema .

Pichani kama nilivyomnyaka akiwa na Mkurugenzi wa tamasha la filamu za zanzibar Dk martin wakikumbushana enzi hizo za nairobi, kenya mara tu baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari ndani ya VIP ya zanzibar.

Monday, July 21, 2008

Orodha ya Washindi wa ZIFF

Dr. Martin Mhando, afisa mtendaji mkuu wa ZIFF akiongea kwenye hafla ya kufunga rasmi tamasha la 11 la ZIFF ngome kongwe, Zanzibar (picha kutoka Michuzi Blog)
Watoto wakitazama filamu kwenye ZIFF
Baadhi ya watazamaji kwenye ZIFF

1. THE GOLDEN DHOW -Awarded to a film that exemplifies excellence in film language and one highlighting Dhow culture.Ezra (2007, Dir: Newton I Aduaka, Nigeria/France)


2. THE SILVER DHOW- Awarded to a film that is a runner up to the Golden Dhow awardee.India Untouched (2007, Dir: Stalin K. India)


3. SHORT/ ANIMATION -Awarded to the best short film in the festival reflecting mastery of the short film structure and aesthetics.Subira (2007, Dir: Ravneet Chadha, Kenya/)


4. EAST AFRICA -Awarded to the best film by an East African filmmaker that shows the greatest commercial aptitude and potential marketabilityAfrican Lens (2008, Dir: Shravan Vidyarthi, India/Kenya)


5. SPECIAL JUROR'S CHOICE -Laya Project (2006, Dir: Harold Monfils, India)SEMBENE OUSMANE PRIZEAwarded to a film that takes a particular look at topics of development coperation.INTO THE LIGHT by Peter Glen, 2007, USA


6. SIGNIS JURY AWARD -Awarded to a film that is deemed to to exemplify universal and spiritual values that enhance human dignity, justice and tolerance.TARTINA CITY by Issa Serge Coelo - (Chad)


7.Special Commendations-Behind this Convent By 2007, Gilbert Ndahayo (Rwanda)African Lens 2008, by Shravan Vidyarthi (Kenya)East African TalentSubira (2007, Dir: Ravneet Chadha, Kenya)


8. VERONA JURY AWARD -Awarded to a film deemed the best African feature film in competition.Behind this Convent 2007, By Gilbert Ndahayo (Rwanda)


9.FIPRESCI JURY PRIZE- Awarded to a feature film from the Dhow Countries that combines cultural astuteness and commercial potential.EZRA directed by Newton I. Adauka, Nigeria/France, 2007


10. THE ZIFF CHAIRMAN'S AWARD -The award is given to a film that reveals an acute reflection on contemporary issues in a balanced manner in these times of polarised perspectives.In The Name of God , Shoaib Mansour, Pakistan, 2007


11.THE AIR TANZANIA AWARD FOR THE BEST EAST AFRICAN FILM- African Lens (2008, Dir: Shravan Vidyarthi)


12. THE UNICEF AWARD -For the Best film that encapsulates issues of children and WomenThe Kadogo Brothers, 2007, Ivory Coast, By Joseph Muganga

Wednesday, July 02, 2008

Bongoland II - Zanzibar

Kwa wale wote mlioko Bongo!!

Tunafurahi kuwatangazia kuwa sinema ya Bongoland II itaonyeshwa katika Tamasha la filamu la Zanzibar (Zanzibar International Film Festival) Sinema ya Bongoland II itaonyeshwa rasmi Jumamosi, July 12 saa moja na dakika 15 jioni.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa tamasha, Bwana Martin Mhando, alisema "ratiba hii imezingatia umuhimu wa kuwapatia watanzania wengi fursa ya kuiona sinema hii, ndo maana ikapangiwa jumamosi". Itaonyeshwa kwanza katika sinema zote zitakazoonyeshwa usiku huo.Kama mnavyokumbuka, Bongoland II ilishutiwa katika jiji la Dar mwaka jana mwezi wa saba.

Wasanii wote katika sinema hii ni wakazi wa Bongo. Hii ni sifa kubwa maana sinema hii itachuana na sinema nyingine nyingi kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni.

Mwezi ujao Bongoland II itaonyeshwa Chicago katika Gene Siskel Film Center katika Black Harvest Film Festival. Soma zaidi hapa. TUTAONANA ZENJ!! - link it to in their own words.