Showing posts with label Ray. Show all posts
Showing posts with label Ray. Show all posts

Thursday, March 18, 2010

Ray na Vincent Wanatafuta Waigizaji wa Kike Wapya!

Waigizaji wasichana wanahitajika RJ Company

03/18/2010


Kama unajihisi wewe ni mrembo basi kwa sasa tunatafuta wasanii wapya wa kike katika ofisi za RJ COMPANY zilizoko SINZA MORI. Lengo ni kuwapata wasanii wa kike ambao ni wapya katika tasnia ya filam nchini ili waje kushiriki katika filam mpya itakayoandaliwa na kampuni ya RJ. Umri ni kuanzia miaka 18 mpaka 28. Pia unaweza kutuma picha zako kabla hufika ofisini ili tuweze kukuona jinsi ilivyo.Muda wa ofisi ni saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni kwa siku za Jumatatu mpaka Ijumaa na siku za Jumamosi kuanzia saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 8 mchana. HAKUNA GHARAMA ZOZOTE ZILE UTAKAZOLIPISHWA KWANI KAMPUNI INAJITOSHELEZA.

WASILIANA NA VINCENT aka RAY KUPITIA:Tel: +255 714 082729P.O. Box 11347
Email: vincentkigosi@gmail.com
Website: www.rjtanzania.com

*****************************************

Hapo napingana na Ray. Yaani watu zaidi ya miaka 28 hawawezi kuwa warembo? Angesema anatafuta kuanzia 18+. Katika sinema unahitaji waigizaji wa kila umri. Mambo ya vijana kujifanya wazee haipendezi. - Chemi

Monday, July 14, 2008

Kanumba Bongo


Kaka Michuzi, hivi karibuni alibahatika kukutana na wacheza sinema maarufu wa Bongo, Steven Kanumba na Ray. Alipiga picha hii huko Msasani Club. Cheki Kanumba anavyoonekana sasa...very handsome na hiyo ndevu!
Kuona picha zaidi mtembelee Kaka Michuzi kwa kubofya HAPA.