
Leo kuna habari kuwa mwimbaji Billie Joe Armstrong wa bendi Green Day alifukuzwa kwenye ndege ya Southwest Airlines alipokataa kupandisha suruali yake zilizokuwa fesheni GawaKundu. Alikuwa anasafiri kutoka Oakland, California kwenda Burbank, California. Soma habari kamili kwa kubofya HAPA.
Msemaji wa Southwest anasema kuwa Armstrong aliruhusiwa kupanda ndege nyingine. Nadhani kwa vile mzungu.
Kuna kijana mwingine mweusi ambaye alifungwa mwaka huu kwa vile alijaribu kupanada ndege ya US Airways na fesheni GawaKundu. Deshon Marman ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha New Mexico na pia mcheza football alikamatwa na kushitakiwa kwa makosa kadhaa ya jinai.
Lakini ajabu, kuna mwanaume wa kizungu aliyeruhusiwa kupanda ndege ya US Airways akiwa amevaa chupi ya kike na sidiria tu!
Soma habari ya Marman na Bikini Man kwa kubofya HAPA:

Kwa habari zaidi ya kesi ya kijana Marman tembelea:
http://www.sfexaminer.com/local/peninsula/2011/07/deshon-marman-sue-us-airways-after-saggy-pants-arrest
NOTE: Fesheni GawaKundu si mbayawakati mwingine, nimeshaona matako ya vijana wengi wa kizungu, weusi na waAsia baada ya suruali zao kuanguka wakiwa wanatembea!!! LOL!