Showing posts with label Walimu. Show all posts
Showing posts with label Walimu. Show all posts

Saturday, October 27, 2012

Mwalimu Ajiua Dar Baada ya Hii Picha Kutoka!!!

Mwalimu ni kiungo muhimu sana katika malezi ya wanafunzi hapa nchini.Wao hushinda na watoto wetu kutwa nzima .......
Kwa mantiki hiyo, tabia ya mtoto yeyote aliyewahi kalia madawati ina asilimia zaidi ya 70 ya tabia za walimu wake......
Siku hizi mambo yamebadilika sana.Mwalimu wa miaka ya 90 ni tofauti kabisa na mwalimu wa miaka ya leo.
Walimu wa leo wengi wao ni vijana wadogo ambao wengi wamejawa na tamaa za mapenzi.Wao hawajui kutongoza bali wanajua kulazimisha....
Inashangaza na kusikitisha kuona walimu wetu wakishindana KUTOA BIKRA ZA WATOTO WA KIKE......Mtoto akikataa basi cha motoatakiona ....
Mtandao huu umebahatika kuongea na mwanafunzi mmojaambaye ni mhanga wa tukio hilo la kulazimishwa mapenzi na mwalimu wake..........
HILI NI SIMULIZI LAKE:
--------------------------------------------------------------------
Mwalimu akimbaka mwanafunzi wake darasani. Baada ya picha hii kutoka kwenye gazeti la Udaku Mwalimu huyo mbakaji mshenzi alijiua!

"Mwalimu alianza kunitaka tangu nikuwa form one.Nilipomkataa alianza kunichapa tena bila kosa maalumu na kunipa adhabu kila mara...
Baada ya kufanya hivyo kwa muda, aliamua kuniita ofisini na kuniambia kuwa anatanisaidia kimasomo endapo ntamkubalia.Niliamua kumkubali kwa kwa kuhofia viboko na aliniambia nisimwambie mtu.

Siku ya kwanza kufanya mapenzi alinipeleka gesti na aliniambia kuwa atatumia condom.Kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza hatukuweza kutumia kinga na alifanya hivyohivyo.

Baada ya hapo tuliendelea kufanya hicho kitendo hata tukiwa shule.Wakati wa kutawanyika, mwalimu alikuwa akiniita katika ofisi yake na kunilazimisha tufanye.....

Miezi kadhaa baadaye, nilianza kujihisi tofauti na wazazi wangu waliyagundua mabadiliko hayo.Walinipeleka hospitali na vipimo vilionesha kuwa nna mimba.Waliponibana ilinibidi niwaeleze ukweli.....

AFISA ELIMU AINGILIA KATI:
Baada ya kubaini hali hiyo, baba alinipeleka moja kwa moja mpaka kwa afisa elimu wa mkoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli.Mwalimu aliitwa na kuhojiwa.Mwanzo alikataa kabisa lakini baada ya kubanwa ilibidi akubali.

Mwalimu alisimamishwa kazi kwa muda na kufunguliwa mashitaka.Alikaa polisi kwa siku mbili, siku ya tatu alipata dhamana akatoka.....

Alipotoka, mwalimu aliamua kujiua kwa sumu.Shule niliachishwa.nipo nyumbani na mtoto.

Sunday, February 08, 2009

Translation:

Tanzanian Member of Parliament: "We 'Fat People', I mean we Members of Parliament, are really hurt to see teachers and those who have retired not being paid what they are owed, Ahh!"

Kipanya (Rat Character) - Why don't you start with your driver...

Friday, November 21, 2008

Walimu Wachachamaa Tena!

Walimu wakitafuta majina yao


OFISI za maDC na Maded wa Temeke na Kinondoni leo zilipata matatizo kidogo wakati walimu walipovamia kutaka kujua kulikoni baada ya majina yao kutokuonekana katika karatasi za malipo kwenye mbao.Pichani ni walimu wakiangalia majina yao.Imeelezwa kuwa wilaya ya Kinondoni zaidi ya walimu 200 walijiandikisha kuuliza kulikoni kwingine wakafanya maandamano.

OniSomething is wrong somewhere kwanini taarifa sahihi zisitolewe kuhusu nini kinafanyika mbona watu wanafanya vitu vionekane kama matusi? Na nilipowatafuta jamaa kujazia stori kila mtu akawa anaruka kimanga. Kuna shida kwelikweli na ofisi hizi za umma, utafiti vile wanalinda magunia ya bangi. - Lukwangule
********************************************************
Nami nauliza hivi Tanzania walimu wetu wanadhauruliwa kiasi hicho? Hao walimu wanakazi nzito ya kuelimisha watoto wetu. Kazi wataweza kufanya vizuri kweli kama wanakuwa na wasiwasi wa kulipwa mshahara, tena ambao wamekwishaifanyia kazi? Hii ni aibu sana. Zamani shule za serikali zilikuwa za hakika lakini siku hizi mmmmh!- Chemi

Friday, October 17, 2008

Walimu Wanaonewa Tanzania!

Ni miaka mingi Tanzania sasa walimu wazuri wanakimbia shule za serikali kwenda kufundisha kwenye shule za private. Kisa shule za private zinalipa vizuri.

Jamani, nataka mkumbuke kuwa kuna wakati walimu wazuri walikuwa wanafundihswa kwenye shule za serikali na walimu wabaya walikuwa wanafundisha shule za private. Hivi kumetokea nini?

Ni uzembe wa nani mpaka kumekuwa na hali mbaya kiasi kwamba walimu wanaona kuwa mgomo ndo njia pekee ya kudai maslahi yao? Hali umekuwa mbaya mpaka watu hawtaaki kuseomea ualimu kwa sababu wanajua wataumia. Na wanaopoata nafasi wanaacha kabisa ualimu na kuingia fani zingine!

Mdau na mwanablogu John Mwaipopo kasema, "Katika kundi la walimu kuna wasiopata promosheni toka 1981! narudia 1981.achilia mbali wa miaka 10, 9,7 na kadhalika. Wamo ambao hawajawahi kupandisha vyeo wala kwenda likizo toka waanze kazi miaka mingi haisemeki. Ukiuliza utajibiwa ngoja 'upembuzi yakinifu ufanyike. Years go by. Na wanadai jumla ya shilingi biloni 16 tu ambazo fisadi mmoja anaweza anayesemekaka kuficha mapesa uingereza anaweza kuwalipa na akabaki na chenji."

Jamani! Mbona hali hiyo ni jambo la aibu kwa serikali yetu. Huko tunaona wabunge wananunuliwa mashangingi kila siku!

Hebu serikali waaingilie hii suala mara mora na watatue hayo matatizo kaya ya mwaka 2008 kwisha. Na pia waombe msamaha kwa walimu wa Tanzania.

Wednesday, October 15, 2008

Walimu Wetu Vipi Tena!!!!!

(pichani Mwalimu Mkoba akipigwa na Walimu wenzake! Picha kutoka Haki Ngowi Blog)

Hivi, hao walimu walishikwa na 'mob mentality' nini? Kwanza lazima nisema kuwa naogopa sana maana hao ndio wanaofundisha watoto wetu! Na kwa nini walitaka kumwua kiongozi wao? Waseme tu ni wavivu na wanatafuta kisingizio cha kutokwenda kazini!

Walivyofanya ni vibaya na washukuru kuwa si enzi za Mwalimu Nyerere. Wangesombwa wote hao na kupelekwa Gezaulole kulima kwa muda!

****************************************************************
Walimu wataka kumuua Rais wao

2008-10-15

Na Richard Makore

Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Gratian Mkoba, jana alinusurika kuuawa na walimu wenzake baada ya kuwatangazia uamuzi wa kuahirisha mgomo wao uliopangwa kuanza leo, hali iliyowalazimu polisi kuingilia kati na kumtoa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kupitia mlango wa nyuma.

Kabla ya polisi kumuokoa, viongozi wenzake waliokuwa meza kuu, walimkinga dhidi ya silaha zilizokuwa zikirushwa, zikiwamo viti na chupa za maji.

Walimu hao wakiwa wanawaka hasira walivamia meza kuu na kuzonga huku wakimlaani kuwa amewasaliti kwa kukaa upande wa serikali, hivyo kupoteza heshima na imani aliyojijengea kwao.

Umati wa walimu kutoka manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam, walikutana katika ukumbi huo pamoja na mambo mengine ili kujua hatma ya mgomo huo na madai yao kwa serikali kama ulivyotangazwa na CWT kwa muda mrefu.

Baada ya Mkoba kutangaza kusitishwa mgomo huo, baadhi ya walimu, walianguka kwa mshtuko huku wengine wakiangua vilio, hali iliyosababisha ukumbi kugeuka eneo lililojaa huzuni kubwa na kutawaliwa na kelele za vilio.

Mkoba aliwaambia walimu hao kuwa, mgomo wao umefutwa kwa amri ya Mahakama na kuwataka leo wasigome kama walivyopanga kwa kuwa watakuwa wamekiuka amri hiyo halali.

Kabla ya kumalizia neno `` hakutakuwepo mgomo kesho``, ukumbi huo uligeuka kuwa kama uwanja wa vita kutokana na baadhi ya walimu kumrushia Rais huyo chupa za maji, viti, kuvunja meza kuu, alikokuwa amekaa hali iliyosababisha viongozi wote wa chama hicho waliokuwa wamekaa naye kukimbia.

Hata hivyo, jitihada za baadhi ya viongozi hao, waliojipanga kuwakabili walimu waliokuwa wameanzisha vurugu hizo kwa lengo la kumdhuru Rais huyo zilishindikana hadi walipofika askari wa Jeshi la Polisi kumuokoa kwa kumuondoa ukumbini hapo kwa kupitia mlango wa nyumba.

Wakati hayo yakijiri, walimu wasikika walikisema kuwa: `` Hatukutaki, umenunuliwa na serikali, acha gari letu na ngoja tukufundishe adabu kwani naona hutujui.``

Baada ya walimu kushtuka kwamba mlengwa wao ameondolewa ukumbini hapo kwa kupitishiwa nyuma, walitoka nje na kulizingira gari la polisi kwa lengo la kulizuia kuondoka na Rais huyo wakiwa wamebeba mawe.

Polisi walilazimika kufyatua risasi za moto hewani na kuwatanya walimu hao kisha kuondoa gari lao kwa mwendo wa kasi.

Kufuatia kiongozi huo wa CWT kuokolewa na polisi, baadhi ya walimu walirudi na kumalizia hasira zao kwa kutoa upepo kwenye magurudumu ya gari lake lililokuwa limesimama nje ya ukumbi huo na kutaka kulipasua vioo.

Dalili za kuzuka kwa vurungu hizo, zilianza kuonekana ukumbini hapo baada ya viongozi wa chini wa CWT kugusia habari za kusitishwa mgomo huo ambapo walimu walikuwa wakiguna kuashiria kutokuunga mkono uamuzi huo.

Kabla ya kutokea kwa vurugu hizo wakisubiri mkutano wao uanze, walimu hao waliimba nyimbo za kumsifia Mkoba wakati anaingia ukumbini na wakisema wana imani naye.

Baadhi ya nyimbo hizo ni ``tuna imani na Mkoba oyaa! oyaa!`` na nyingine nyingi, lakini hali ilivyogeuka walimuona kama mtu mbaya na mhalifu wa siku nyingi.

Wakizungumza na Nipashe ukumbini hapo, walimu hao walisisitiza kuwa mgomo wao uko pale pale na kwamba Mkoba hawezi kuwazuia kwani wao ndiyo watendaji.

Walidai mazingira yanaonyesha kwamba Rais wao amenunuliwa na serikali na hivyo amepoteza sifa za kushika wadhifa huo, hivyo ajiuzulu.

Wakati Mkoba akiwa amebana kwenye kona ya ukumbi huo huku akitetemeka, walimu walisikika wakimwambia kuwa kuanzia jana awaachie gari lao ambalo ni la CWT na atafute usafiri mwingine au aondoke kwa miguu.

Rehema Kimweri Mwalimu wa Shule ya msingi Mivinjeni wilayani Temeke alisema, ana miaka 25 kazini, lakini hajawahi kupewa fedha za likizo pamoja na kushindwa kumrekebishia mshahara.

Lyidia Mhina kutoka Shule ya Msingi Mtoni aliangua kilio na kushindwa kuzungumza zaidi ya kutamka jina lake na shule anayofundisha.

Atanas Mwinyi wa shule ya msingi Kimara B, alisema kuwa serikali na CWT ni kitu kimoja kwani anaamini kwamba Mkoba alikwenda ukumbini hapo kuwahadaa.

Alisema anaidai serikali zaidi ya Sh. 600,000, deni ambalo alidai amejibiwa hadi leo linafanyiwa uhakiki.

Rais huyo alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya vurugu zilizoibuka ukumbini hapo aligeuka bubu huku akiwaangalia waandishi wa habari.

Mahakama ya Kuu kitengo cha Kazi, juzi ilizuia kufanyika kwa mgomo huo, uamuzi ambao walimu hao wameupinga na kudai kuwa hawataingia madarasani, isipokuwa watakwenda kazini.

Walimu wameazimia kugoma kwa madai kuwa serikali imeshindwa kuwalipa madai yao licha ya kuipa siku 60 tangu Agosti mwaka huu.

Siku hizo zilimazika jana na leo ilikuwa ni siku iliyopangwa na walimu hao kugoma baada ya kupata baraka za CWT.

SOURCE: Nipashe

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/10/15/124522.html

Tuesday, September 16, 2008

Walimu wasivyoheshimika Bongo!

Kutoka gazeti la MWANANCHI:

Hayo ni makubwa! Nani anaumia hapa? Bongo wanavyodharua walimu ni aibu!
Ndo maana watu hawataki kuwa walimu.

***************************************************************************
Mkurugenzi awakana walimu 200 Dar, Afisa Elimu mkoa ashangaa

Baadhi ya walimu kati ya 200 ambao mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam amedai kuwa hawatambui hivyo wakatafute nafasi mahali pengine.
Gedius Rwiza na Aika Mushi

MKURUGENZI wa Manispaa ya Kinondoni amewakana zaidi ya walimu 200 waliondamana hadi ofisini kwake kudai fedha za kujikimu ambazo hawajapewa tangu waripoti katika vituo vyao vya kazi mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza baada ya kupokea maandamano hayo, mkurugenzi wa manispaa hiyo, Noel Mahyenga alisema, hahusiki na walimu hao na wala hawatambui kama waajiriwa wa manispaa yake.

"Wanatakiwa kurudi ngazi ya mkoa ili kuangalia sehemu watakapowaweka kwa kuwa manispaa yangu haina upungufu wa walimu, ingawa tatizo hili nalifahamu," alisema mkurugenzi huyo.

Alipotakiwa kutoa maelezo kuhusu mshahara waliolipwa mwezi walioanza kufanya kazi, mkurugenzi huyo alidai kuwa, walilipwa kimakosa na kwamba kama watabahatika kupata sehemu za kwenda, ataongea na wizara ili wakatwe mshahara huo.

"Kulipwa mshahara, barua na mkataba wa kazi si hoja. Katika bajeti yangu sina pesa ya kuwalipa walimu hawa. Warudi mkoani. Kama walipangiwa Kinondoni ni makosa yalifanyika bila kujua. Nina walimu wa kutosha," alisema Mahyenga.

Majibu hayo yaliwasikitisha walimu hao.

"Nashindwa kuelewa tunapoambiwa kwamba sisi siyo waajiriwa wa Manispaa wakati tuna barua za kuripoti kazini na mikataba tunayo, na kama walijua sisi siyo waajiriwa kwa nini tumelipwa mshahara wa mwezi Julai?" alihoji Mwalimu Rehema Macha.

Akizungumzia suala hilo, Afisaelimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makali Bernard alikiri kutokea tatizo hilo na kuongeza kuwa hahusiki.

"Nilishamaliza kazi ya kuwapangia vituo vya kufanyia kazi. Nashangaa kusikia kwamba Manispaa haiwatambui kama watumishi wao," alisema. "Kazi yangu ni kugawa vituo kama ninavyoagizwa na wizara. Hilo ni suala la mkurugenzi wa manispaa ambaye ndiye mwajiri wao."

Walimu hao walisema hali yao kifedha ni mbaya na kwamba fedha walizokuwa nazo zilishaisha siku nyingi, lakini bado wanaendelea kufundisha. Walidai kuwa baadhi yao walikuwa wamepanga vyumba, lakini wamefikia hatua wanaona watashindwa kulipia kodi ya pango, huku baadhi wakiwa wameanza kufukuzwa.

Mwanasheria wa Chama cha Walimu (CWT), Leonard Haule, aliwashauri walimu hao kurudi nyumbani na kwamba ataenda nao kwenye ofisi za manispaa hiyo kujua mustakabali wao.

Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba alisema kuwa, hali hii inaonyesha kuwa mgomo wao waliopanga ufanyike Oktoba 15 utakuwa na nguvu.

"Kama wanaona walimu ni lazima waandamane ili wapate haki zao, tutawaonyesha tulivyochoka na usumbufu huo," alisema. "Kama wamefikia kuwakana wafanyakazi wao, hali inasikitisha."