Friday, October 17, 2008

Walimu Wanaonewa Tanzania!

Ni miaka mingi Tanzania sasa walimu wazuri wanakimbia shule za serikali kwenda kufundisha kwenye shule za private. Kisa shule za private zinalipa vizuri.

Jamani, nataka mkumbuke kuwa kuna wakati walimu wazuri walikuwa wanafundihswa kwenye shule za serikali na walimu wabaya walikuwa wanafundisha shule za private. Hivi kumetokea nini?

Ni uzembe wa nani mpaka kumekuwa na hali mbaya kiasi kwamba walimu wanaona kuwa mgomo ndo njia pekee ya kudai maslahi yao? Hali umekuwa mbaya mpaka watu hawtaaki kuseomea ualimu kwa sababu wanajua wataumia. Na wanaopoata nafasi wanaacha kabisa ualimu na kuingia fani zingine!

Mdau na mwanablogu John Mwaipopo kasema, "Katika kundi la walimu kuna wasiopata promosheni toka 1981! narudia 1981.achilia mbali wa miaka 10, 9,7 na kadhalika. Wamo ambao hawajawahi kupandisha vyeo wala kwenda likizo toka waanze kazi miaka mingi haisemeki. Ukiuliza utajibiwa ngoja 'upembuzi yakinifu ufanyike. Years go by. Na wanadai jumla ya shilingi biloni 16 tu ambazo fisadi mmoja anaweza anayesemekaka kuficha mapesa uingereza anaweza kuwalipa na akabaki na chenji."

Jamani! Mbona hali hiyo ni jambo la aibu kwa serikali yetu. Huko tunaona wabunge wananunuliwa mashangingi kila siku!

Hebu serikali waaingilie hii suala mara mora na watatue hayo matatizo kaya ya mwaka 2008 kwisha. Na pia waombe msamaha kwa walimu wa Tanzania.

No comments: