Saturday, February 06, 2010

The Harlem Renaissance Revisited - Mchezo wa Kuigiza

Mother Africa /Mama Afrika
Linda Henderson akimpaka make-up Joe Banks Jr. (Steve Lucky)

Kushelia, Linda na Catrina walioigiza kama watumwa

Muongozaji (Director) Wetu Lee Smith na Oscar feki tuliyomkabidhi kama shukurani kwa kazi nzuri. Lee aliigiza kama Langston Hughes pia.


Mimi na Ruby Hill tukiwa tumevaa costumes kwa ajili ya Party Scene.


Mimi niligiza kama Mother Africa pia, safari hii. Father Africa alikuwa David Bowden. Kwa mara ya kwanza walikuwa na Mother Africa ambaye anaongea lugha ya Afrika. Khanga na vitenge nilinunua nilivyokuwa Dar mwezi Novemba. Ungo nilinunua Ubungo TANESCO. Nilikuwa na nyingine ambaye nilikuwa nafanya mazeozi nayo, ilibiwa pale tulipokuwa tunafanya mazoezi! LOL!


Costume yangu ya awali kama Ms. Thelma anayetafuta mapenzi na ana ndoto ya kushinda bahati nasibu.


Mimi na Charles Jackson aliyeigiza kama Joe the Bartender. Mwanzo Ms. Thelman anamkataa Joe, lakini baadaye anamkubali na wanafunga ndoa.Wadau, jana jioni (Ijumaa) niliigiza katika mchezo wa kuigiza, The Harlem Renaissance Revisited with a Gospel Flavor. Mchezo wa Harlem Renaissance umetungwa na Haywood Fennell Sr.

25 comments:

Anonymous said...

Da Chemi,

Hizi picha zako ziko bomba sana. Hasa hiyo uliyoigiza kama mother afrika. Nzuri sana.

Hongera kwa jitihada zako.

Mdau,
London

Anonymous said...

wewe siumefiwa na mumeo juzi?

Chemi Che-Mponda said...

Mdau wa 6:!2am, Ndio nimefiwa na mume wangu. Lakini Marekani hapa. Kazini walinipa siku tano za kuomboleza, nimerudi kazini. Na katika showbiz wanasema, The Show Must Go On.

Anonymous said...

Nenda kazini dada, umefiwa na mume ndio lakini msiba unao mwenyewe ndani ya nafsi yako, utakaa nyumbani utakula mawe? Ingekuwa Bongo ungechukua hata likizo ya mwezi mzima unajua ndugu na jamaa hata wa mume watakutunza. Sasa huko tamaduni ni tofauti, una watoto wanataka kula na kusoma, eti ukae nyumbani na recession hii unatafuta msiba mwingine?

Anonymous said...

wadau wengine ovyo hata comment zenu hamuwazi kwanza eti unaandika wewe si umefiwa na mumeo inamaana yeye hajui unajua bongo watu wanafanya vitu vingi kwa kuangalia watu si kwa ukweli wa mambo hata serikali za vijiji siku hizi zimekataza watu kukaa misibani siku nyingina tulio wa Mungu tunasema kazi ya Mungu haina makosa ikitokea tunaomba Mungu anatupa nguvu za kuendelea na maisha

Anonymous said...

nimependa picha hizo safi sana ni kumbukumbu nzuri kwa watoto wenu walioko huko kujua japo kidogo utamaduni wa mkwao africa

Admirer said...

Dada Chemi umependeza kweli. Keep it up! Utafika mpaka Hollywood.

Anonymous said...

Dada hongerea sana! lakini mbona hata 40 bado, sababu namfahamu jamaa yangu mmoja kafiwa Mkewe hapa NJ, amepewa siku 7 za mapumziko, mimi nadhani ni mapema mno, lakini sababu ni kazi...

Anonymous said...

Ungeongeza na kaniki kidogo da chemi ungetoka bomba zaidi.....afadhali umewaonyesha uafrika hasa kwani huwa hawajui kama waafrika tunatoka nchi mbalimbali! Wakiigiza watu wakiafrika wanaongea lafudhi ya kinaija...

Anonymous said...

pamoja na kazi nzuri anayoifanya lakini arobaini ya mumewe alishaimaliza?kwa maadili yetu ilibid a-cool kwanza yaani huyo mumewe kashamsahau haraka hivyo?aomboleze kwanza then other things vitafuata baadae,asiwe na haraka hivyo.uchungu wa mume jamani ni muhim.

Anonymous said...

Hongera sana dada yangu Chemi. I feel proud for you! Kwa kweli unatuinua sana Watanzania na hasa Wanawake wa Kitanzania. Mungu akuzidishie uwezo wa kufanya kazi, busara na afya njema ili uweze kuendelea na kazi zako.

Nichukue nafasi hii pia kukupa pole nyingi kwa msiba mzito.POLE SANA DADA. Kila mtu anaelewa kuwa ni lazima uendelee na kazi, hayo ndiyo maisha. Msiba uko moyoni dada yangu, kazi nayo ni muhimu, na zaidi ya yote, maisha ni lazima yaendelee. Mungu wetu mwema aendelee kukulinda na kukutetea.

All the best. We love you. Love from Dar es Salaam and Dodoma.

Chemi Che-Mponda said...

Mdau wa 12:33am, wala sijamsahau mume wangu na arobaini unaendelea. Lakini kumbuka niko Marekani. Ukisema ungonjee arobaini, utakosa mengi! Ubaya zaidi hasa katika usanii, unatupwa kama mtu 'unreliable'. Katika kikundi chetu kuna mtu mwingine kafiwa kabla ya show, lakini aliendelea. Tunakwenda kwenye mazishi jumanne. Miaka ya nyuma nilikuwa kwenye kikundi cha wazungu hapo Harvard Square, mume wangu aliugua kawa intenseive care. Nilichelewa rehearsals kwa vile nilienda kumwona. Hawakuniita tena, ilibidi nitafute kikundi kingine. Kazini, naona nitachukua kalikizo baadaye nikipata siku za kutosha.

Anonymous said...

Chemi, huna haja ya kuclarify mambo yanayohusu maisha yako, kimsingi msiba utakuwa nao tu utake usitake, hayo ya arubaini siku hizi hata nyumbani wengi hawafuati wanakaa ile likizo aliyopewa na mwajiri ya siku 5 basi. Labda itokee bahati iwe bado mtu hajachukua likizo yake ya mwaka ndio anaenda likizo.

Mie ni muislam sisi tuna eda, zamani watu walikuwa wanakaa ndani siku zote za eda mpaka iishe, anatunzwa kwa kila kitu na ndugu za mume hata ndugu zake pia. Maisha sasa yamebadilika nani atakutunza siku zote za eda? Basi hata wanawake wa kiislamu hutoka nje kutafuta rizki midamu wamejistiri.

Ni heri mwanamke anayetoka nje kutafuta maisha lakini anajiheshimu na kumheshimu marehemu mumewe kuliko wale wanafiki wanaokaa ndani lakini humo washikaji/mabwana zao wanawafuata.

Hakuna hata mtu mmoja mwenye haki ya kuingilia maisha yako ya ndani, kwani kati yetu sisi tutaishia kusema tu lakini hakuna atakayetoa senti tano yake kukulipia bills, kodi za nyumba na mengineyo. Ni wewe unayeicheza hiyo ngoma na ndiye unayejua mrindimo na utamu wake sisi ni watazamaji tu. Kwa hiyo comments za kipuuzi kama hizo huna haja ya kuzijibu kujustify unachofanya, dont let them make you feel guilty mpaka uwajibu, wewe nyamaza kimya, na wengi wenye kutoa hizo comments ni wanawake, tena wengine wana waume, waswahili wanasema 'ukiona mwenzio kanyolewa....'

Msiba uko nao wewe mwenyewe tena ndani ya nafsi yako!

Mswahili

Anonymous said...

Nilibahatika kuona dada Chemi anaigiza...Ama kweli kazi anaisweza...Good job..Keep it up!!

Anonymous said...

da chem pole sana hawa wanaokwambia umechukua muda mfupi ku come back ktk activities, after u r husband passed away,mi naona hao wapo bongo hawajui maisha ya nje,to missed even one hour it will course matatizo, na kazi unaikosa na watambue kuwa hauko afrika, hivyo hata tamaduni zinatofautiana,excuse kama hivyo hawazielewi mchongo huo upo afrika

Anonymous said...

Kweli kama angekuwa mume niliyependa sana sijui kama ningerudi kwenye kazi mapema hivyo hata kama ni sababu nipo Marekani, but kama wengine walivyosema hamna haja kuingilia maisha ya mwingine, lakini ni mapema mno.

Anonymous said...

Da Chem upo bomba sana ,naomba weka picha za ujana wako nizione.
Achana na hao wanaotaka ukae siku 40 huo ni ushamba waambie wachagga wanakaa siku hizo?
mdau Bongo.

Anonymous said...

Haata Tanzania likizo ya kufiwa ni wiki 2 tu, sasa wanaokushangaa nasi tunawashangaa.
Nilifiwa na mume na baada ya wiki 2 nilitakiwa kazini, ilibidi niende vinginevyo wanangu watakula nini?

Halil Mnzava said...

Waliiba ungo?ebo!
Basi wakati mwingine ukija Bongo wapelekee nyingi kwa ajili ya zawadi,yaelekea wamezipenda!
Picha nzuri sana.
Hongera!!!!

Anonymous said...

Safi sana Dada Chemi. Kuna siku utafika Broadway na Hollywood!

Anonymous said...

Sasa nyinyi mnapiga kelele za nini? mwenzenu ameishapata papers... endeleeni tu na kelele zenu.

Anonymous said...

Sidhani kama Da Chemi alikuwa na shida ya papers kama mtu mmoja alivyodai kuwa eti yeye keshapata papers. Pamoja ya kuwa Mzee Chemponda ni mtanzania lakini Chemi alizaliwa Marekani, yeye mwenyewe hana makuu ya kutaka kujitangaza. Na isitoshe wakati tuko wadogo bado tunasoma shule, Kina Chemi walikuwa wanakaa Kilimani nyumba za chuo tulikuwa tunaspeculate kuwa mama yao ni Mmarekani. Kwa hiyo justification yenu kuwa eti keshapata papers ni baseless na wivu usio kichwa wala miguu. Sie wengine tunaona kama amerudi kwao tu huko Marekani.

Kama nitakuwa nimekosea Da Chemi utanisamehe!

Anonymous said...

Dada Chemi,

Pole sana na msiba mkubwa uliokukuta, nakuomba sana usiwajibu hao watu hapo juu. Ukifanya hivyo utakuwa umewapa adhabu kali sana.


Frankly speaking, what they are asking is not only too personal but also non of their business. There is no such thing as general way of grieving, we should allow others to grief the way they see it fit. My advice to you Dada Chemi, go ahead with your life by doing those things that would have made your husband happy.

Anonymous said...

Sasa wewe unafikiri dada Chemi amekuomba hili uwe msemaji wake? na huyu aliysema kuwa tayari amepata papers wewe inakuhusu nini? wabongo kwa kufuatiliana bwana...

TOTAL KNOCKOUT!!! said...

Umependeza sasa Chemi!