Monday, February 01, 2010

Tukumbuke Waliovyofanya - Greensboro Four


February ni Black History Month yaani mwezi wa kukumbuka historia ya weusi Marekani. Kwa wakati huu ni muhimu sana tukumbushe vijana wetu historia ya weusi Marekani...utumwa, ubaguzi na vitendo vya uonevu na mauaji.

Wadau, hapa Marekani siku hizi tumezoea kwenda madukani na kwenye migahawa na kuhudumiwa bila matitizo. Haikuwa hivyo siku zote. Mpaka miaka ya 1960's kulikuwa na sehemu ambazo weusi walikuwa hawahudumiwi. Walikuwa hawaruhusiwi kula chakula katika migahawa, kulikuwa na mabango 'Whites Only' (Wazungu Tu). Kama walikuwa wanahudumia weusi basi ilibidi waende nyuma ya jengo na kupewa chakula kwenye mfuko, huko si ajabu wazungu waliitemea mate na kuiweka mikojo, mavi na uchafu mwingine.

Greensboro Four walikuwa vijana weusi wanne waliokuwa wanasoma katika Chuo Kikuu cha North Carolina A & T. Siku ya Februari mosi mwaka 1960, waliamua kwenda kukaa katika sehemu ya wazungu kwenye duka la Woolworth's na kudai wahudumiwe. Walisema kwa nini hapo dukani wanauuzia weusi mahitaji, lakini hawawezi kuwaruhusu kukaa kunywa kahawa na kula chakula hapo. Kwanza weusi wenzao waliwaona wajinga na wapuuzi, lakini wengine walijiunga nao na mwisho migomo iliandaliwa katika miji15! Hatimaye ilibidi rais wa wakati huo Rais Dwight D. Eisenhower aiingilie! Hatimaye Woolworth's waliruhusu weusi kula hapo.

Kusoma habari ya Greensboro Four BOFYA HAPA: http://www.cnn.com/2010/US/02/01/greensboro.four.sitins/index.html?hpt=C1

No comments: