Thursday, February 18, 2010

Tanzia - Reginald Mhango (Reggie) Bosi wangu Daily News

Reggie na copy yake ya sinema Bongoland II. Sehemu ya hiyo sinema ilipigwa nyumbani kwa Reggie huko Magomeni Mikumi. Nilipomwomba kupiga sehemu ya sinema hapo allikubali bila kusita na pia alifurahi kuona jinsi wanavyotengeneza sinema. Alifurahi uchapa kazi wa crew waliotoka Marekani.
Mimi, Reggie Jr. (katikati) na Mzee Reggie Mhango. Picha hii tulipiga siku ya October 27, 2009 nyumbani kwa Reggie. Nilisikia kutoka kwa kaka Michuzi kuwa alipata stroke lakini hajambo. Nilimpigia Reggie simu kutoka Marekani mwezi wa saba na kumwaidi kuwa nitafika siku hiyo na nilifika. Alifurahi sana.
************************************
Wadau, nimepokea kwa majonzi habari ya kifo cha bosi wangu mpendwa nilipokuwa Daily News, Reginald Mhango (Reggie). Reggie alikuwa na utu, uvumilivu, na upendo kwa kila mtu. Nakumbuka nilikuwa napata shida nikiwa na mimba mwaka 1989. Tumbo ilianza kuwa kubwa na kutembea ilikuwa shida. Reggie aliniambia nikae nyumbani mpaka nijifungue na kumaliza maternity leave. Si hiyo tu lakini kwa kweli sikumbuki kumwona akiwa na hasira au akigombana na mtu. Alitufundisha sisi waandishi chipukizi uandishi wa habari hasa, na kutusaidia katika kuandika habari safi...to the point! Nje ya kazi, ilikuwa hata kama una shida binafsi alikuwa tayari kusikia na kutoa mawaidha.
Mnakumbuka ile kesi ya Mzee Athumani Ali Maumba. Yule babu wa Magomeni aliyekuwa analawiti watoto wa kike wa primary, Reggie alisaidia hizo habari zichapishwe. Hamwezi kuamini lakini mpaka hiyo kesi ya Maumba ilikuwa kama mwiko kuandika habari hizi. Hata waandishi wa habari wengine walikataa kuripoti. Mimi ndo nilikubali kwenda huko kwenye hiyo shule Kisutu na kuchunguza. Baada ya ripoti kukamilika wakuu walitaka kuzuia, Reggie aliongea. Kesho yake walitoa para mbili tena kwa kificho. Baada ya kuona si mwisho wa dunia, habari za Maumba zikawa front page. Msishangae na kusema najiona,lakini mkumbuke kuwa wakati huo kulikuwa na magazeti machache nchini. Daily News (serikali) Uhuru (Chama) na Mfanyakazi, Kiongozi (Wakatoliki). Redio ilikuwa RTD tu. TV ilikuja baadaye.
REST IN ETERNAL PEACE REGGIE. WE WILL MISS YOU DEARLY BUT YOU IMPARTED GREAT KNOWLEDGE AND WISDOM IN US AND WE WILL PASS IT ON!
Mnaweza kusoma habari zaidi kwa Kaka Michuzi.
Na pia someni Daily News:

5 comments:

John Mwaipopo said...

hakika alikuwa mwalimu bora kwenu. mungu amrehemu, apumzike kwa amani. amen.

Anonymous said...

Pole sana Da Chemi. Kweli Mzee Mhango alikuwa mtu poa sana.

SIMON KITURURU said...

R.I.P!

Anonymous said...

Kati ya waandishi wa habari pale "Daily News" aliofanya kazi nao ni mwandishi wa vitabu, Godfrey Mwakikagile, ambaye ameandika pia kuhusu Reginald Mhango katika kitabu chake "Nyerere and Africa: End of an Era."

Nilimaliza kusoma kitabu hicho mwezi uliopita na Godfrey Mwakikagile ameandika mengi mazuri kuhusu Reginald Mhango katika kitabu hicho.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Anonymous said...

Oh my God yaani inasikitisha sana kwani hakuwa mhariri tu bali alikuwa kama baba pale "The Guardian".Alinifundisha sana jisi ya kufanya mahojiano na mabalazi wa nje au kuandika maswali kwa ujumla. Kusema kweli sina la kusema kwani ni kazi ya Mungu haina makosa. Njia ya wote yeye ametangulia nasi tutafatia.

ZK