Tuesday, October 26, 2010

Pweza Paulo Afariki Dunia!

Yule pweza maarufu aliyetabiri timu zilizoshinda katika Kombe la Dunia (Kandanda) World Cup huko Afrika Kusini amefariki dunia.

Habari kutoka Ujerumani alipokuwa anatunzwa zinasema kuwa Paulo alifariki leo akiwa na umri wa miaka miwili na nusu. Baada ya World Cup Paulo aliishi maisha ya raha mustarehe katika hifadhi ya viumbe vya bahari huko Ujerumani.

Mipango ya mazishi bado haijakamilika lakini wanasema kutokana na umaarufu wake ni lazima azikwa kwa heshima.

Mnaweza kusoma habari zaidi CNN.Com

http://www.cnn.com/2010/SPORT/10/26/germany.paul.octopus.death/index.html?hpt=Sbin

Najua huko Bongo watu wanasema wamekosa kitoweo kizuri. Hapa USA watu wanasema kuwa badala ya kutangaza kuwa kafa si wangemchukua pweza nyingine na kusema ni Paulo. Watu wasingejua eti.

4 comments:

Anonymous said...

Wazungu bwana eti mazishi kwa ajili ya pweza! Watu wangapi wanapata dishi hapo! Khaa!

emu-three said...

Mhh, mnyama kama huyo kapata sifa na `anazikwa' kwa heshima kubwa, je, najiuliza, je na mimi au wewe utaipata heshima kama au angalau kidogo kama hiyo?

Anonymous said...

MI MWENZENU CJAWAHI KUMLA UYU MNYAMA,NA IVI NNAVOMUONA ALIVO NNA KINYAA NAE CTOMLA,IVI NI MTAMU HUYU AU?

Anonymous said...

Tumekosa kitoweo!