Wednesday, April 27, 2011

Mimi katika 'Body of Proof'

(Chemi Che-Mponda (left) as the Police Station Receptionist in the Society Hill episode of Body of Proof)


Wadau, kama mlitazama Body of Proof jana kwenye ABC taifa basi huenda mliona nikiigiza kama Receptionist (Mapokezi) kwenye kituo cha Polisi. Scene ilipita haraka, lakini nimeweka picha hapa. Stelingi wa Body of Proof ni Dana Delany (kashika blackberry) ambaye alikuwa kwenye show Desperate Housewives. Katika show ya jana iitwayo Society Hill, mhariri wa gazeti maarufu inayohusu maisha ya matajiri kauwawa. Polisi wanamshikilia mtu ambaye wanadhani kamwua, ila Dr. Hunt (Dana) anagundua aliyemwua ni mwingine.


Bado kuna episode ambayo nitakuwa mpelelezi (detective). Mimi nilikuwa mwigizaji 'extra/background' hivyo sina maneno. Natumaini kuwa wakitengeneza episode zingine watanipa maneno.

Body of Proof ilishutiwa katika studio huko Rhode Island mwaka jana. Studio ilikuwa ghala ambayo waligeuza studio huko Warwick. Yaani huwezi kuamini mambo waliofanya mle kusudi iwe studio halisi. Hata scene ambazo utadhani zilikuwa nje, zilipigwa ndani!

7 comments:

Anonymous said...

safi sana...soon tutaanza kukufungulia mlango wa limo.

emu-three said...

Nimeipenda hiyo je mikanda yake inapatikana?

Anonymous said...

Hongera Dada Chemi! Karibu tutakuona Hollywood!

Mbele said...

Hongera sana. Kaza buti Da Chemi. Ndo ndo ndo hujaza ndoo.

Anonymous said...

Hongera ila jitahidi kupunguza unene..kwani una kipaji na unaweza kufika mbali zaidi.

Anonymous said...

hata simshauri apunguze uzito kwani wanawake wote wanaofanya vizuri holywood weusi si wembamba mfano queen latifah,oprah, monique,mwigizaji wa precious, jennifer hudson(ila kwa sasa kapungua anaweza akakosa market sasa) hivyo wala usibadilike

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wote. Kuhusu unene, katika sinema wanahitaji watu wa saizi zote.

Nilisahau kusema ile scene tulipiga saa 11 (5:00am) huko Rhode Island mwezi September mwaka jana. Ilikuwa siku yangu ya kwanza kwenye Body of Proof. Kuna siku nilikuwa mpelelezi wa polisi and siku nyingine daktari kwenye ofisi ya Medical Examiner (Ofisi yua kuchunguza vifo). Nidhamu kwenye seti ya Body of Proof ilikuwa kali mno, ukifanya kosa unafukuzwa! Kuns dada wa kizungu alifukuzwa kwa sababu alikuwa anaongea na mtu wakati mastelingi wanapiga scene.