Tuesday, April 12, 2011

Rais Gbagbo wa Ivory Coast Akamatwa!



Wadau, Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na mke wake wamekamatwa na askari wa Upinzani huko Abidjan. Mdau Mobhare Matinyi amekusanya picha za kukamatwa kwao. Zinatia huruma hasa huyo mke wa Gbagbo. Mara nyingi watu wanasherekea kukamatwa kwa viongozi wao, lakini wanajuta wakigundua anayemfuta ni mbaya zaidi. Rais Gbagbo na Mke wake Simone mara baada ya kukamatwa na askari wa Upinzani huko Abidjan. Walikuwa wamekimbilia kwenye hoteli.
Mama Simone Gbagbo, mke wa Rais Gbagbo mara baada ya kukamtwa kwao
Askari wa Kiongzoi wa upinzani Ivory Coast Allasane Ouattara wamemzunguzka Raia Gbagbo akiwa anavaa
Rais Gbagbo akijifuta na taulo huko kwenye hoteli alikokamatwa Abidjan.
Wakazi wa Abidjan wakisherekea kukamatwa kwa Rais Gbagbo
Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na mke wake Simone wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya kugombea urais mwaka jana


*************************************


Kwa habari zaidi za Utawala wa Rais Gbagbo na Kukamatwa kwake someni:




6 comments:

Anonymous said...

Dah! Shida ya kujificha hotelini zimewafanya wakongoroke hivyo? Yaani mke wa Gbagbo kumbe ana mvi kibao na upara. Wigi zinaficha mengi. Halafu huyo Gbaggbo kadhofika nini? Kabadilika sana ukilinganisha na picha zake za zamani.

Anonymous said...

More than 1 million civilians fled their homes and untold numbers were killed in the power struggle between the two rivals that threatened to re-ignite a civil war in the world's largest cocoa producer. Gbagbo's security forces have been accused of using cannons, 60 mm mortars and 50-caliber machine guns to mow down opponents during the standoff.

Anonymous said...

Wanatia huruma lakini tusisahau watu zaidi ya milioni moja wamekufa kwa ajili yao.

Anonymous said...

Hizo picha za Before & After, DUUUH!

Anonymous said...

Kama kuna ulevi mbaya ni ule wa kulewa madaraka! Kupofushwa macho ya kuuona uhalisi! Unashindwa hata kusoma alama za nyakati! Alijua yuko kinyume cha Jumuia za kimataifa! Alijua hata akiongoza lazima atumie mtutu! Hata kama aliamini ameshinda basi ushindi bado ulikuwa na utata! Umri tu ulimtosha kusema sasa basi! Na kutambua kila kila kina mwanzo na mwisho!Ni somo kwa vongozi wetu Africa, ni somo hata katika maisha ya kila siku! Kuna Nyakati za kusema sasa basi! Wakati wangu wa kuondoka na kuendelea mbele umefika wapishe wengine!

Anonymous said...

When i read opinions of individuals who even contemplate showing any sort of sympathy for despots like gbagbo,i lose hope in my continent. completely.No wonder dictators like mugabe find people amongst us to serenade them as if they represent any sort of progress that will set us free from this darkness.misplaced sentimentalism has no place in a continent that seeks to build strong foundations for the future where rule of law,respect of electoral process and human rights as whole are the norm rather than the expception (and even then,after much bloodshed).
there are no "imperialists" other than than our own demented power-clingers!