Thursday, January 26, 2012

Ikulu Yatoa Tamko Kuhusu Ndege ya Rais

Kwa kweli ninapenda jinsi Ikulu inayojitahidi kutoa Press Release siku hizi. Enzi za Mwalimu mtu angepelekwa huko 'MAHALA' na kuminywa mapumbu ili ashike adabu kumsema Rais.

*********************************************************
 *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

Gazeti laTanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wakwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, *“Ndege ya  JK utata: Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.”

Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum ya Rais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa njebaada ya  Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwa ndege
kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuria mkutano wa  dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”.

Limeendelea Gazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege hiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Raisya siku nne kuhudhuria mkutano huo
itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300. Aidha,Gazeti hili linadai  kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikwete amehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwa taifa.

Kwa hakika, maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti  la Tanzania Daima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyo kuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais.

Katika kuuelezea umma ukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuziufuatao:

Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari jana jioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji chaDavos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic; Forum (WEF) unaoanzaleo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa Davous, nchini Sweden kama linavyosema Gazeti hili.  Aidha, Rais Kikwete na ujumbe  wake umesafiri kwa ndegeya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

Pili,Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya  kawaida (routine maintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri  na ipasavyo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan, Paul Mhaiki jana. Isipokuwa nivyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege  hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu,Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (testflight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopitakama linavyodai Tanzania
Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwamiezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama zamatengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

 Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari  kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama  tulivyoeleza jana, ambako atahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu  wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021. Hivyo, si kweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya Mheshimiwa Rais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.

Nne,  Tanzania Daima  linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na wala faida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili.

Tunapenda kukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa Rais Kikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:

 (a) Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana.

Mpango huu utakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma  kwa  kushirikisha Serikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya imataifa unalengakuleta faida zifuatazo:

 (i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekanibilioni 3.4 katika kilimo cha  Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hichomara tatu katika miaka 20 ijayo.

(ii) Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneo ya hekta 350,000.

(iii) Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.

(iv) Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katika umasikini.

(v)Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakula cha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani. 

(vi) Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na  bandari katika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.

(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao,kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na waanzishia
mifumo ya kisasa yaumwagiliaji.

(viii )Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kila mwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50  zinaendelea kuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwa kuanzia  katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa), Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)

(b)  Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dolaza Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dares Salaam unaofanywa  na  Kampuni ya Yara International, moja ya makampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa Kampuni ya Yara International, moja ya makampuni makubwa zaida ya  uzalishaji wa mbolea duniani.

Yara International ni mmoja wa washirika wakubwakatika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hatamajirani wanapata mbolea ya  kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

(c) Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa chikukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa  siasa,  wabiashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake zakuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

Katika siku tatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu; wengine atakutanana Bwana Bill Gates wa Bill& Bellinda Foundation,  Naibu  Waziri wa Uchumi,Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya Dunia Bwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, Mtendaji Mkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra.

Tunapenda kumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni  vyema Gazeti laTanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapishakama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha  uzushi usiokuwa na sababu zozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

*Imetolewa na*:
*Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais*,
Ikulu, *DAR ES SALAAM*.
25 Januari, 2012

3 comments:

Anonymous said...

Tz Daima ni gazeti linalomilikiwa na upinzani. Unategemea wataandika mazuri kuhusu serikali, ili iwe nini? Tatizo lao ni pale wanapotia chumvi sana na kujiweka katika hatua mbaya ya kuitwa wazushi!

Anonymous said...

Lakini ndugu zangu minute za vikao siyo matokeo.
Maazimio ya vikao siyo tija.

Mazungumzo ya kwenye vikao ni tofauti kabisa na matokeo.

Watu wanaweza kuongea mambo matamu kwenye vikao na yakaishia hapo hapo.

Anonymous said...

mimi nashangaa sana Tanzania tuna matatizo mengi hatujayatatua na yanatatulika badala ya kupoteza pesa kwa safari zisizo na msingi nafikiri tunge save pesa kutatua angalau matatizo mengine madogo madogo. 1993 waziri wa mawasiliano kwa wakati huo Pro. Sarungi aliulizwa swali na wafanyakazi waATC wa Engineering nchi yetu ni maskini lakini tuna mashirika matatu ya ndege yote ni ya serikali moja ni ndege za serikali za mizigo za kijeshi na ATC CHA AJABU NI KWAMBA HIZO NDEGE KIUNDESHAJI ZINACOSTI PESA NYINGI LAKINI MUDA MREFU HUWA ZINAPAKI ATC wakikwama hata kama wana shida ya ndege ndogo ya Domestic fliught wanakodi kwehye mashirika hengine ya ndege kwannini wasi kodi ile ya serikali iliyo paki? Kuanzia hapo kukawa na flight nyingine zina fanywa kwa kukodi ndege ya serikali Pia serikali inatakiwa kubana matumizi kwenye hizi ndege za serikali mbone kuna viongozi wengi wa nchi wanatumia National Airline zao? chamuhimu ni kuimarisha National Airlie yenu hata Raisi akitaka kusafiri awe anatumia ndege ya shirika lake kwani ATC ni shirika la serikali.