Showing posts with label Oscars. Show all posts
Showing posts with label Oscars. Show all posts

Saturday, February 28, 2015

Gauni ya Lupita Nyong'o Iliyoibiwa Hollywood Imepatikana - Ina thamani ya dola $150,000!


Mcheza sinema Lupita Nyong'o

Wadau, jumapili iliyopita, mceheza sinema na mrembo, Lupita Nyong'o,  alivaa gauni enye thamani ya dola za kiMarekani $150,000 kwenye Oscars.  Hiyo gaumi imepambwa na lulu 6,000 (ameivaa pichani) na imeshonwa na mwanafesheni maarufu, Calvin Klein.  Baada ya Oscars Lupita aliiacha kwenye chumba chake kwenye hoteli ya kifahari The London West Hollywood na alitoka.  Alivyorudi alikuta gauni imeibiwa.

Sasa indaiwa kuwa aliyeiiba, kariudisha baada ya kugundua kuwa hizo lulu ni feki.  Mwizi alinyofoa lulu mbili na kuzipeleka kwenda kuuza kwa sonara, ndo kaambiwa ni feki.
 
Lupita Nyong'o ni mcheza sinema kutoka Kenya aliyepata umaarufu baada ya kushinda Oscar mwaka jana, Aliigiza kama mtumwa katika sinema,  12 Years a Slave.  Pia, alipendwa kwa urembo wake hasa baada ya wanafesheni kugundua kuwa anaweza kuvaa nguo vizuri  na kupendeza kuliko Model!

Kwa habari kamili BOFYA HAPA.

Sunday, March 02, 2014

MKenya Lupita Nyong'o Ashinda Oscars!!!!




Mwigizaji, Lupita Nyong'o kutoka Kenya ameshinda tuzo za Oscar!!!!!! Anakuwa mwafrika mweusi wa kwa kushinda. Mzungu Charlize Theron kutoka Afrika Kusini amewahi kushinda.  Kweli Hollywood inabadilika maana miaka mingi ilikuwa vigumu mwigizaji mweusi kuteuliwa na hasa kushinda! Katika miaka 86 ya historia ya Oscar Lupita, ni mwanamke wa saba mweusi kupokea Tuzo ya Oscar!

HONGERA LUPITA NYONG'O!!!!


Lupita Nyong'o leo kabla ya Tuzo za Oscars Kuanza

Lupita Nyong'o katika sinema  12 Years a Slave

Lupita akicheza na mwimbaji Pharell


Afrika Inawakilishwa Katika Oscars ya Mwaka Huu!

Wadau, tunangojea kwa hamu kuona kama Lupita Nyong'o kutoka Kenya na Barkhad Abdi mwenye asili ya Somalia watashinda katika tuzo za Oscars leo jioni.

Kwa mara ya kwanza Nchi mbili za Afrika zinawakilishwa katika Tuzo za Juu za Oscars.

Lupita Nyong'o  yuko katika Best Supporting Actress (yaani mwigizaji bora wa kike katika sinema si mwigizaji mkuu).  Na Barkhad Abdi anagombea Best Supporting Actor (yaani mwigizaji bora wa kiume - si mwigizaji mkuu).

Jamani, jamani sijui waafrika tukoje, huyo Barkad kasemwa na waSomali wenzake, eti ana sura mbaya na mengine! Khaa! 

Na nisimsahahau Chiwetel  Ejiofor ambaye ni Mwingereza mwenye asili ya Nigeria.  Yeye anagombea Mwigizaji bora wa kiume. (Best Actor).

Kushoto ni Lupita Nyong'o na Kulia ni Barkhad Abdi

Mara nyingi nchi ya Afrika inayopata sifa katika Osars ni Afrika Kusini.  Waigizaji wao wazungu kama Charlize Theron wanatambulika sana.  Charlize alikuwa Msouth Afrika wa kwanza kupata Oscar.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Saturday, January 18, 2014

WaAfrika Wawili Wako Katika Orodha ya Waigizaji Bora Mwaka Huu - OSCARS

Wadau, haijwahi kutokea! Waafrika wawili wako katika mashindano ya Oscars mwaka huu!  Lupita Nyong'o kutoka Kenya ameteuliwa katika kundi la Waigizaji Bora wa Kike (Supporting), na pia Kijana Barkhad Abdi kutoka Somalia amaeteuliwa katika kundi la Waigizaji Boara wa Kiume (Supporting). Je, watashinda?

Bi Lupita aliigiza kama Mtumwa katika sinema 12 Years a Slave.  Alikuwa anaigiza katika television ya Kenya. Pia alisoma Uigizaji hapa Marekani katika Chuo Kikuu cha Yale. Alichaguliwa kuigiza katika sinema 12 Years a Slave mara baada ya kumaliza Yale.

Lupita Nyong'o katika sinema 12 Years a Slave



Barkhad Abdi aligiza katika sinema Captain Phillips. Kabla ya kupata nafasi ya kuigiza katika sinema hiyo, alikuwa anaendesha limo huko Minneanapolis, Minnesota.  Barkhad alienda Open Casting Call na kuchaguliwa.  Wadau nikiwaambia muende Open Call, Nenda!

Barkhad Abdi Katika Sinema Captain Phillips



Kuona Orodha ya wote walioteuliwa kaitka Oscars 2014 BOFYA HAPA:


Wednesday, March 27, 2013

Picha Kutoka Seti ya Sinema Hapa Boston

Wadau, wiki iliyopita nilishiriki katiika sinema inayopigwa hapa Boston. Kwa sasa haina jina lakini mwongoji ana Oscars kadhaa. Siwezi kuwaambia mengi mpaka sinema itoke.  Nguo niliyovaa iko chini ya koti. Na nilivaa wigi enye nywele ndefu.  Lakini sidhani kama nitaonekana, kama nitabahatika kutoka utaniona natongozana na jamaa chuma kweli!

Tuesday, March 09, 2010

Mzungu Am 'Kanye West' Mweusi kwenye Oscars

Umesikia kituko kilichotokea kwenye Oscars juzi? Huyo Roger Ross Williams alikuwa anapokea tuzo kwa ajili ya sinema ya 'Music by Prudence'. Ghafla katokea bibi wa kizungu, Elinor Burkett, na kuanza kusema, "mwache mwanamke aongee" na maneno mengine ambao watu hawakuelewa.

Sisi watazamaji tulishangaa sana inatokea nini. Kumbe huyo mzungu aliwahi kuwa producer wa hiyo sinema lakini waligombana na Williams. Burkett alimpeleka mahakamni lakini walisuluhisha nje ya mahakama. Burkett aklisem hakupenda jinsi sinema ilivyokuwa inaenda. Ajabu, jinsi ilivyoenda ndo ikashinda Oscar!

Lakini wadau , hii kituko kisingetokea tusingekumbuka habari ya hiyo sinema, Music by Prudence. Pia hao Williams nad Burkett wasingejulikana. Sasa hivi Letterman, Leno na wengine wanamtania huyo Burkett. Bila shaka na Saturday Night Live watamtania!

Pia wanamwita Burkett, Lady Kanye! Kumuka mwaka jana Kanye West alivyoingia hotuba ya Taylor Swift kwenye tuzo za MTV.

Wednesday, February 17, 2010

Wateule wa Oscars 2010 Wala Chakula Pamoja!


Wadau, kila mwaka ni kawaida kwa walioteuliwa kupata tuzo ya Oscars kula chakula cha mchana pamoja. Leo walivigida huko Hollywood. Chakula chenyewe kina kuwa cha fahari kweli. Sherehe ya kujua nani kashinda na kutuza wasanii bora, na watengeneza sinema bora itaka siku ya jumapili, March 7, 2010.

Nangojea kwa hamu kumwona dada Mo'nique akishinda Oscar ya Best Supporting Actress. Mo'nique lazima ashinde maana hiyo kazi aliyofanya kwenye sinema Precious ni kiboko. Pia nina hamu ya kumwona Gabourey Sidibe akitembea kwenye Red Carpet. Akishinda Tuzo ya Mcheza sinema bora wa kike itakuwa maajabu. Nasmea hivyo kwa sababu kwanza ni mweusi, tena kwa hapa Marekani mweusi tii, mnene, na ni mara yake ya kwanza kuigiza katika sinema. Akimshinda Meryl Streep nitasema kweli Hollywood imebadilika.

Tuesday, January 22, 2008

Bi Ruby Dee ni mweusi pekee kuteuliwa kupata Oscar mwaka huu!


Leo asubuhi majina ya walioteuliwa kupata Oscar yalitangazwa. Bi Ruby Dee (84) ni mweusi peke yake kuteuliwa mwaka huu. Ameteuliwa katika category ya Best Supporting Actress. (naomba mnisaidie kutafsiri hapo) Mwigizaji Bora wa kike ........
Ametueliwa kwa kazi aliyo fanya katika sinema, American Gangster. Katika sinema hiyo alicheza kama Mama Lucas ambaye ni mama mzazi wa Frank Lucas, mhusika mkuu wa sinema hiyo. Nafasi hiyo ilichezwa na Denzel Washington.
Bi Ruby Dee ameigiza katika sinema nyingi tena vizuri sana lakini hii ndo mara ya kwanza yeye kuteuliwa. Tena ana miaka 84! Nangojea kusikia anasemaje kuhusu kuteuliwa kwake!

Hakuna sinema kutoka Afrika iliyoteuliwa mwaka huu.

Sherehe ya kutuza Oscar itafanyika Februari 24, mwaka huu huko Kodak Theatre, Hollywood.