Sunday, September 14, 2014

Kenny, Mtoto wa Mama Bishanga Aoa!

KENNY MTOTO WA MAMA BISHANGA AOA MZANZIBAR

Hendrich Nambira au Kenny kama anavyojulika kwenye mchezo wa Mambo hayo katika runinga ITV,  alifunga pingu za maisha na mke wake Florence kutoka Visiwani Zanzibar. Harusi ilifanyika kanisa la Anglican UMCA, Upanga DSM tarehe 23/08/2014. Mama Bishanga na mumewe hawakuwahi siku ya harusi hiyo iliopendeza sana na kuhudhuriwa na wazazi wakimwemo wadogo wa mama Bishanga Mack Innocent Hatia na Constancia Innocent Hatia, baba mkubwa mzee John Kamota na shangazi Rehema Kamota, bibi wa Kenny mwalimu Agnes Innocent Hatia na ndugu zetu wengine, pia marafiki na wawakilishi wa wasanii toka Bongo movie. Sherehe ya kukata na shoka ilifanyika Lion Hotel.


Kenny akiwa na mkewe Florence. Auaga ukapera.
Bwana harusi Kenny na mkewe Florence wakiwa pwani Oster Bay mara baada ya kufunga ndoa

Florence na Herry waikikata Keki

Wanaharusi wakikabidhiwa Top Tier ya Keki yao

Wanaharusi wakigonga Champagne Toast na Wageni wao

Dada wa bwana harusi Sizelina ambae ni mtoto wa kwanza wa mama Bishanga akilisakata rumba kwa raha na furaha tele ya harusi ya mdogo wake.

Wayao na Wamakua wakicheza wimbo wao maarufu wa Tilamaundee huku wakiongozwa na aliyekuwa mbunge wao Mzee Ray Mrope

1 comment:

Anonymous said...

Mama Bishanga ndio nani?