Saturday, September 13, 2014

Msanii Lucy Komba Aolewa!

Kutoka BONGO MOVIES:
Hatimaye yule mwigizaji mkongwe nchini Lucy komba amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi aishie nchini Denmark aliyefahamika kwa jina la Stanley,. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii nchini lucy ameandika
"..Asante Mungu kwa siku hii nzuri na muhimu sana katika maisha yangu, wengi hawakutaka nifikie siku hii, kunawengine walinuna, kunawengine waliniombea mabaya, kuna wengine walichukia na wengine waliambiana wanichunie walifikiri bila wao Mungu hawezi kuifanikisha siku hii, nasema asante Mungu kwa sababu aliifanikisha siku hii kwa nguvu zake wqtu wanaonipenda walisheherekea siku hii vizuri walikunywa na kula na kusaza watu zaidi ya miasita walikuwa ukumbini wakishangilia pamoja nami haleluyaaaaaaaaaaaaaaa anachokiunganisha Mungu binadamu hawezi kukitenganisha hata ieeje.."

Hongera sana lucy.

No comments: