Sunday, November 16, 2014

Jaji Mkuu Amjulia Hali Rais Kikwete Marekani

 Picha na habari kutoka Ikulu.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe
Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba
16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins
jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika
hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa
Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi
jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na
marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo
ya mahakama.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake
waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika
hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore,
Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo
alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako
Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na
ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya
Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi
mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia
wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya
rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,
daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Mhe Hussein Katanga.

No comments: