Friday, November 14, 2014

Rais Kikwete Atoka Hospitalini Baada ya Kupata Nafuu

 PICHA NA HABARI KUTOKA IKULU:Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa
Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya
kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais
Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni
akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya
kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya
mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za
Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia
pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi
mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye
amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya
Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa
mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku
chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete
pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi
(SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu
mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi
wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza  (Picha na
Freddy Maro)

No comments: