Saturday, February 28, 2015

Captain John Komba Afariki Dunia

 Wadau, Mh. Captain John Komba, Mbunge wa Mbinga amefariki leo katika hospitali ya TMJ. Wanasema alikuwa anasumbuliwa na kisukari (diabetes).

Lazima niseme kuwa nakumbuka marehemu Captain Komba alivyoaanza kupanda chati. Alikuwa Sargent wa Jeshi na alikuwa anaimba katika kikundi cha wasanii. Alimwimbia Mwalimu ule wimbo wa 'We Love Freedom'.  Nimesahau ilikuwa sherehe ya nini. Mwalimu na wote tuliyokwepo tuliblow!  Alipata U-Captain haraka sana na mambo ya TOT ni ya kihistoria.

REST IN PEACE CAPTAIN KOMBA!

Kutoka Twitter:

Rest in peace, Tanzanian singer/politician Captain John Komba. I remember his rise to fame. 
Chama Cha Mapinduzi @ccm_tanzania 7m7 minutes ago
TANZIA:Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar.
0 replies10 retweets0 favorites Reply
Retweeted10



Kutoka EATV
 
East Africa TV
@ eastafricatv
1m
#TANZIA Mbunge wa Mbinga Magharibi
Kapt. John Komba amefariki dunia leo
saa 10 jioni katika hospitali ya TMJ
DSM kwa tatizo la Kisukari


15 comments:

Anonymous said...

R.I.P Captain Komba, pengo lako si rahisi kuliziba.

Anonymous said...

Kwa mtazamo wangu, naamini kifo cha Mh. Komba kimetokea ili AGANO la Mungu litimie ambalo marehemu mwenyewe alijiwekea nadhiri kuwa "CHADEMA haitatawala akiwa HAI". Sasa CHADEMA inajiandaa kutwaa dola huku kukiwa hakuna support ya public dhidi ya notion ya kuingia msituni. Hivyo basi, Komba inabidi atangulie kabla dola haijatwaliwa na CHADEMA.
Mungu akupumzishe salama na milele. RIP Captain.

Anonymous said...

RIP komba . Lakini liwe fundisho kwa vijana wanao wadharau waasisi wetu kama akina Walioba kuwatukana na kuwapiga kuwadhalilisha hadharani LAANA NA MIKOSI nadhani Makonda ajifunze na aombe msamaha LAANA HII IMUEPUKE.

Anonymous said...

Mwaka huu nani atakaengoza choir ya chama chetu kwenye kampen jamani?kutakuwa hakuna wahudhuriaji,any way Mungu amlaze pema.

Anonymous said...

Nyimbo za uchaguzi zitakuwa na ladhà tofàuti.

Anonymous said...


Nenda taratibu,hivi sasa bado tunaomboleza,hata kuzikwa tu bado,maneno chungu zima,Hoo! mara Komba kafanya hivi ,hoo! kafanya vile,haitatusaidia watanzania wenzangu,miaka hii bwana ni majanga tu ya kimaadili,miaka ya zamani mambo hayo ni mpaka siku ya kuanua matanga lakini sasa hivi ni balaa,yaan ukianza kukata Roho tu! magazeti yanaanza,sijui ni kukosa kazi au kukosa utu? tutumie muda huu kufariji wafiwa;wanafamilia na wana Nyasa kwa ujumla.

JC said...


“Mwanadamu, aliyezaliwa na mwanamke, ana maisha mafupi na yenye kujaa msukosuko.” (Ayubu 14:1)

Anonymous said...

Kwakweli alipenda Sana mababez na alikuwa muhongaji/mtunzaji mzuri sana..... Akikupenda shida ndogo ndogo zimeikuishia.... RIP Komba

Anonymous said...

Acha huyu kiumbe asiyekuwa na haya AFE. hana maana alitaka kwenda msituni sasa mungu kampeleke zaidi ya msitu. yy alimuona Mzee Warioba ndo kuchoka a nakaribia kufa kumbe hajui mipango ya Mungu ikoje. Na AZIKWE HARAKA KABLA MUNGU HAJABABADILI ADHABU JAMAA AKAFUFUFKA. NA AZIKWE TU

Anonymous said...

Nimekumbuka hizo enzi za huo wimbo dah,Ila all in all alikua na kipaji cha kuimba . Mwaka 1999 tena zile nyimbo za maombolezo ya mwalimu hasa ule wimbo anaotaja awamu ya kwanza....... Hakuna ubishi alikua na talent ya uimbaji. R.I.P Komba

Anonymous said...

Jamani Watanzania tunaishi katika utani ...Nadhani watani Za wangoniiiii ...Leo WATAKUA na mengi ya kutaniana ...
Wangoniiiii ni Kina Zuma ...kwa Hiyo he can do anything to win a woman ....so tusimlaumu please ...!!, ni Kama Umlaum MZARAMO ngomani ...

Kwa Kweli kwa namna alivyokitetea chama hasa kampeni Za Rais Kikwete ...Mkapa ..Mwinyi ..wabunge wengi ..chama kwa ujumla....walimkubali kwa mema yake ..ingetakiwa wamkubali na kwa madhaifu yake ........
Wewe fikiria anawaambia nini watoto wake .....pale ambapo Mali zote alizochuma zinapigwaaaa Mnada ...na wezake wanashindwa angalau kumsaidia watoto wake wasimlaumu.....
Inauma Sana Kama Mzazi Mali zinauZwa Watoto wamekuwa wakubwa ...wanakughasi kwa nini Mali Za familia zinauzwa ..na marafiki uliowasaidia wakitambua madhaifu yako ....wana kuacha kwa kuwa tu katoa msimamo tofauti

Anonymous said...

Tunaposubiri hiyo siku ambayo hatuijui tuwe waadilifu/waaminifu kwa taifa hili na Mungu. Daima matendo na maneno yetu yadhihirishe haki na kweli kwa manufaa ya watanzania.

Enyi wanasiasa na wananchi wote kwa jumla mwaka huu nchi inapotakiwa kutekeleza uandikishaji wa wapiga kura, kura ya maamuzi kuhusu katiba mpya na uchaguzi mkuu tutende haki. Hakuna haja ya kufanya udanganyifu maana hata tukipata madaraka na utajiri tutakufa na kuviacha vyote hivyo. Ni afadhali ufe masikini kama Nyerere lakini ukakumbukwa kwa kutenda haki.

RIP Komba

Anonymous said...

Ukitaka kujua makundi ndani ya ccm yamefika pabaya wakati kuna wanaoomboleza wapo miongoni mwao wanasherekea kifo cha capt komba ...eti tu kwakuwa hakuwa akiwaunga mkono .....waanaona ni kama askari wa adui kafa .......

Sasa sijui tuseme rip nani .......

Ila kwa wastaarabu ...tunaungana kuomboleza msiba huuu

Anonymous said...

R.I.P captain. kazi ya Mungu haina makosa. umeacha pengo ccm, nyimbo zako zingehitajika sana kipindi si kirefu kijacho. Mtunzi hodari, nitakukumbuka tu kwa ule wimbo wa mwalimu. Bila shaka wasanii watakuaga kwa heshima unayostahili.

Anonymous said...

Jamani jamvi hamskitiki hata kdogo! Yaan mawe kwa kwenda na mngaliambiwa achomwe na taili mngalikuwa wa kwanza kuleta mafuta.La msingi watawala wawe na matendo mema badala ya kujijali wenyewe tu