Showing posts with label Askari. Show all posts
Showing posts with label Askari. Show all posts

Saturday, June 11, 2016

Tukumbuke Askari Wetu Waliopigana kwa Niaba ya Mkoloni



Askari Monument in Dar es Salaam, Tanzania
 Leo nimekumbuka ule wimbo tuliokuwa tunaimba jeshini, JKT, inaenda hivi..... Askari Eh, Vitani yee mama......   

Wadau, mnajua ile sanamu pale City Center Dar. Inaitwa Askari Monument.  Ni kumbukumbu ya Askari waafrika waliopigana katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.  Waafrika walichukuliwa na Mkoloni kuwa Askari katika Majeshi yao, Walifanya kazi ngumu ya kupigana huko wazungu walikaa kwenye viti vyao wanapunga hewa!  Kwa maana hiyo Akari wa nchi fulani, walikuwa wanaua Askari wa nchi nyingine, Kama mchezo vile!  (Gameborad) Askari wengine walipelekwa Ulaya na hawakurudi kwa familia zao, wala familia zao hawajui waliishia wapi!

Nimekusanya picha ya Askari waliopigana katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, wakati huo Tanzania, inaiitwa Deustche Oost Afrika (German East Africa).

Na Mjerumani alikuwa ni msehenzi mkatiki kwa Waafrika..  Waafrika huko vijijini waliuawa wengi sana na Mjerumani eti wazaa au wagonjwa.

Kwa habari zaidi za Vita Kuu ya Kwanza na Dunia na Tanzania (German East Africa) BOFYA HAPA:

Askari Akiaaga Familia Yake kabla ya kwenda Vitani

Askari kwenye Gwaride Dar es Salaam

Askari kwenye Mafunzo 1918










Askari Monument Mwaka 1945

Saturday, August 09, 2014

Kibonde wa Clouds FM Akamatwa na Polisi Leo

Ni mara chache sisi waandishi wa habari, tunakuwa habari!

********************************
 Habari na picha kutoka FACEBOOK:

Askari wa Trafiki Akimkamata Ephraim Kibonde

Ephraim Kibonde ndani ya Lock Up


Mtangazaji Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.

Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

Tuesday, March 01, 2011

Askari Wa Vita Vya Kwanza ya Dunia - German East Africa

Hii ni meli ya kivita Mjerumani SMS Konisberg ikiwa imita nanga bandarini Bagamoyo. Bagamoyo ilikuwa mji mkuu wa Tanganyika enzi za MJerumani
Askari kwenye foleni
Waliopitia JKT wataelewa hii...ROUTE MARCH!

Sijui ni Tanga au Bagamoyo hapo au Itakuwa kwenye Ziwa Victoria au Nyasa

Hao watakuwa wale Asakri wa kwanza kabisa. Hawana viatu!

Askari wakisfisha bunduki zao

Enzi za MJerumani walikuwa wanatumia Rupia siyo Shilingi


Bahati mbaya hatuna majina ya hao Askari pichani



The Force Publique in German East Africa during World War One

Monday, September 28, 2009

Askari Wakisoma Gazeti la Kiongozi 1916

Kumbe gazeti la 'Kiongozi' ilikuwepo tangu enzi za Mjerumani! Hao askari wa enzi za Mjerumani wanaburudika kwa kusoma gazeti la Kiongozi iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Hii Picha ilipigwa wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza (World War I) na Walther Dobbertin.


Askari eh, Vitani eeh Mamaaa!

Friday, December 05, 2008

Askari




Bila shaka wengi wenu mna ndugu ambao walikuwepo vikosi vya askari. Hii picha ya kikosi cha askari kilipigwa enzi za mkoloni (mjerumani) mwaka 1914. Sijui ni Mirambo Barracks, Tabora hapo?

Friday, December 07, 2007

Askari


"Askari eh, vitani yeee mamaaa! "
Mjerumani alipenda sana kupiga posi na askari wao huko Bagamoyo!