Showing posts with label Tanganyika. Show all posts
Showing posts with label Tanganyika. Show all posts

Saturday, September 17, 2016

Mwenge wa Uhuru Wawasili Mkoani Singida na Ishara ya Uhuru wa Tanganyika

MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo

Saturday, June 11, 2016

Ni Ngoma ya Kabila Gani Hii?

Wasdau, hebu nisaidie kujua hii ni ngoma ya kabila gani? Picha imepigwa mwaka 1907 miaka mia moja iliyopita. Ilipigwa enzi za Mjerumani wakati Tanzania ni German East Africa.




Saturday, April 26, 2014

Sherehe za Miaka 50 ya Muungano Mjini Dar es Salaam

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.

Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.

-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.


Picha na Freddy Maro wa Ikulu

Tuesday, June 11, 2013

Wednesday, March 06, 2013

Wazaramo, Wanyamwezi na Wagogo 1864


Hizi picha zilitoka kwenye gazetii huko Ufaransa mwaka 1864.  Ni wakati Speke alivyoenda kutafuta chanzo cha mto Nile.  Picha zinapatikana: http://www.123rf.com/photo_15155982_old-illustration-of-ouzaramo-region-natives-tanzania-created-by-bayard-published-on-le-tour-du-monde.html

Wazaramo 1864

Picha imechorwa 1864.  Wazungu waliwaita Ouzaramo.

Old illustration of Ouzaramo region natives, Tanzania. Created by Bayard, published on Le Tour du Monde, Paris, 1864

                                               Wagogo 1864
Old illustration of Ougogo encampment during Captain Speke expedition towards Nile river source, Tanzania. Created by De Bar, published on Le Tour du Monde, Paris, 1864


Wanymwezi  wakipika pombe 1864
Old illustration of beer making in Unyamwezi region, Tanzania. Created by Bayard, published on Le Tour du Monde, Paris, 1864

Friday, July 06, 2012

Bayume Mohamed Hussein (1904-1944) Aliuwawa na Hitler


Bayume Mohamed Husen 1904-1944
Je, mmewahi kumsikia Bayume Mohamed Husen/Hussein? Alikuwa ni mcheza sinema na askari wakati wa Vita Kuu ya dunia ya kwanza. Enzi zile za Ukoloni wa Mjerumani watoto waliruhusiwa kuwa askari. Aliondoka Tanganyika kwenda Ujerumani. kule alifundisha Kiswahili  na pia aliigiza kama Askari katika sinema kadhaa za kijerumani. Aliuwawa katika kambi ya meteso (Concentration Camp). Hitler alizijenga maaluma kwa ajili ya kuangamiza wayehudi, wasio wazungu na viwete. Weusi wengi walitolewa vizazi ili wasizae enzi za Hitler.  Walikuwa wanaamini mtu mweusi si binadamu kamili

***************************************************************
Bayume Mohamed Husen was born (Feb 22 1904) in Dar es Salaam, German East Africa, now Tanzania, and died (Nov 24th 1944) in Sachsenhausen concentration camp. (birth name: Mahjub bin Adam Mohamed). He was an African-German Askari and actor. Husen served in World War I in the protection force of German East Africa as a child soldier. After the war and the end of German colonial rule, he could not seem to connect to the service of Great Britain, which had Tanganyika as a "mandate". Temporarily Husen worked in Zanzibar as a teacher and as a "boy", as a servant to British and German ships. In 1925 he was hired on to a ship of the German East African line as a waiter.


In 1929 he went to Berlin to demand unpaid wages of his father's and his. The request was rejected by the Foreign Office on the grounds that the fund had already been settled. Attempting to return him to Africa, Husen opposed and instead he settled in Berlin. He worked as a waiter in the "Wild West Bar" at Potsdamer Platz in Berlin from April 1930 until his dismissal in 1935.

From 1931 to 1941 Husen was also at the "foreign studies department," of the University of Berlin as a Swahili Language instructer/assistant. He instructed officials who were to be prepared for the planned subsequent recovery of the German colonies by the German Reich. For a relatively low salary, he worked under the founder of the German African Studies, a former missionary Diedrich Westermann.

In April 1941 he resigned his duties at the university, apparently because of the humiliating treatment by a professor. In January 1933, three days before the appointment of Hitler as Chancellor, he married Mary Schwandner. In March 1933 they bore a son, Ahmed Adam Mohamed Husen. Another daughter, Anne Marie Husen, was born in September 1936. Both of the children died during childhood.

Between 1934 and 1941, Bayume Mohamed Husen had starred in at least 23 German film productions. He had his first role in the movie titled "The Riders of German East Africa". In the movie "To New Shores" Husen 1937 stood alongside the main actors as an extra and also with small speaking roles. He occasionally took on the role of a consultant in the language of Swahili. His biggest role was also his last: Between August 1940 and February 1941 Husen played in the Nazi propaganda film, "Carl Peters" as Ramadan, a guide and interpreter of the "colonial pioneer," Carl Peters.

In August 1941 he was arrested by the Gestapo( "Secret State Police") because of a relationship with a white woman (Aryan). Since there was no legal basis for a conviction - for blacks, there was indeed a ban on marriage, but no sex ban was with "Aryan women" - he transferred to the Sachsenhausen concentration camp. Shortly thereafter, his wife filed for divorce, probably under pressure from the Nazi authorities. After 3 years in the camp Husen died in November 1944 as a result of bad prison conditions. (ref: Bechhaus-Gerst. 2007)

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

http://www.dw.de/dw/article/0,,5065360,00.html

Friday, February 24, 2012

Sikummaliza Jumbe – " Maalim Seif"

Maalim Seif Sharif Hamad

 Mh. Aboud Jumbe Mwinyi




















Sikummaliza Jumbe – "Maalim Seif"


22 Februari 2012

Na Seif Sharif Hamad

Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Makamo wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aboud Jumbe Mwinyi, alilazimishwa kujiuzulu katika Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma akishutumiwa kutaka kuvunja Muungano. Kitendo hiki kimekuwa kikichukuliwa na Wazanzibari kama udhalilishaji mkubwa kwa nchi na heshima yao, na msimamo wa serikali tatu, ambao Jumbe anasemekana kuutetea umekuwa ndio msimamo wa Wazanzibari. Kujiuzulu kwa Jumbe kunaunganishwa na tafauti za kimtazamo baina yake na Katibu Mkuu wa sasa wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye hata hivyo anasisitiza katika makala hii kwamba hajawahi kutafautiana na Jumbe kuhusu mtazamo wa Muungano.

Kwanza niweke kumbukumbu sawa. Mwaka 1984 wakati Mzee Aboud Jumbe anajiuzulu nyadhifa zake zote, mimi ni kweli nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa [NEC] ya CCM, na hivyo kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi. Hata hivyo wakati huo sikuwa miongoni mwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi. Kwani nilikuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1980. Nikateuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar na Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeteuliwa kuwa Rais wa Muda wa Zanzibar mara baada ya Mzee Aboud Jumbe kujiuzulu mwaka 1984. Hivyo kuanzia mwishoni mwa 1980 hadi mwanzoni mwa 1984 sikuwa kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi.

Pili, tangu Chama cha Wananchi CUF kiasisiwe hapo 1992, sera yake rasmi ni kuwepo kwa Muungano wa serikali tatu: yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.

Pengine itakumbukwa kuwa hata Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa Chama cha Siasa chochote kile kina haki ya kuwa na sera yake juu ya Muungano. Akasema kuwa kama vile ni haki ya CCM kuwa na sera ya serikali mbili kuelekea serikali moja, CUF wanayo haki hiyo hiyo ya kuwa na sera ya serikali tatu katika Muungano. Mwalimu Nyerere akamalizia kwa kusema kuwa na sera juu Muungano inayotafautiana na sera ya CCM si uhaini. Waachiwe wananchi waamue!

Hivyo basi msimamo wangu tangu kuasisiwa kwa Chama cha Wananchi, CUF haujapata kubadilika. Ni msimamo na sera ya Chama changu cha CUF. Sera ya kuwepo kwa serikali tatu katika Muungano wetu.

Hivyo niseme, kama nilivyokuwa nikisema kila nilipopata nafasi, kuwa bila ya kuubadili muundo wa Muungano wetu kutoka muundo wa sasa wa serikali mbili kwenda kwenye muundo wa serikali tatu, matatizo ya Muungano yataendelea kuutafuna Muungano wetu. Badala ya kuuimarisha tutakuwa tunaendelea kuudhoofisha. Kuimarisha Muungano sio kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano katika Katiba. Hili linadhoofisha Muungano. Kwani nguvu za Muungano zitatokana na wananchi wa pande mbili kuukubali kwa dhati Muungano wenyewe. Kuhakikisha kuwa wananchi wa pande zote mbili wanaridhika na muundo wake, mamlaka na madaraka ya kila upande na serikali yake. Na zaidi kuliko yote, wananchi wa pande zote mbili kuridhika kuwa wanatendewa haki katika Muungano.

Vyenginevyo tutakuwa tukibadili misamiati tu: mara tutayaita matatizo ya Muungano; mara tuziite kero za Muungano, pengine tutakuja kuyaita mapungufu ya Muungano, au hata bughdha za Muungano, na kadhalika.

Suala la kutoka serikali mbili kwenda serikali moja hilo halitakubalika. Mimi silikubali. CUF hailikubali, na Mzanzibari mzalendo yeyote halikubali. Siamini kuwa Serikali ya Muungano itakuwa tayari kutumia vifaru, mizinga na madege ya kivita kulazimisha muundo wa serikali moja.

Baada ya kuweka msimamo huo, sasa nigeukie mambo mengine uliyoniuliza.

Kwamba Mzee Aboud Jumbe alituhumiwa kutaka kuwepo kwa muundo wa Muungano wa serikali tatu na akalazimishwa kujiuzulu. Wakati huo mimi nilitetea muundo wa sasa wa serikali mbili.

Ili hili lifahamike vyema na wananchi ni vyema kwanza kuelezea mazingira yaliyomfikisha Mzee Aboud Jumbe kujiuzulu.

Nitangulie kueleza kuwa mimi binafsi na kwa dhati ya nafsi yangu namuheshimu na namthamini sana Mzee Aboud Jumbe. Kwanza ni mwalimu wangu nilipokuwa nasoma katika skuli ambayo wakati huo ikiitwa The King George VI Secondary School (sasa Lumumba College).

Pili, ni Mzee Aboud Jumbe ambaye alisababisha mimi kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya yeye kuwa Rais wa Zanzibar mwaka 1972, baada ya kukaa kwa miaka minane (8) tangu nilipomaliza masomo ya Kidatu cha Sita (Form VI) hapo 1963 na kuzuiwa na Serikali ya Mapinduzi kujiunga na masomo ya Chuo Kikuu, pamoja na kuwa kila mwaka nilikuwa napata nafasi katika vyuo mbali mbali duniani.

Tatu ni Mzee Aboud Jumbe huyo huyo aliyesababisha mimi kuwa kiongozi katika Serikali ya Mapinduzi na kuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa CCM. Hivyo namshukuru na katu siwezi kumsahau kwa mchango wake mkubwa ulionifanya nilivyo.

Sasa nirejee kuelezea mazingira ya wakati huo ambayo yalikuwa kama ifuatavyo:

Nianzie mwaka 1982 ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa CCM. Katika kipindi kilichotangulia Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM wa 1982 wa kuchagua viongozi wa kitaifa, kulijitokeza makundi mawili miongoni mwa viongozi wa CCM kutoka Zanzibar yaliyokuwa yakikinzana. Kundi la kwanza likijulikana kama Liberators, na la pili likijulikana kama Frontliners. Kundi la Liberators kimsingi lilikuwa na viongozi ambao walikuwa wanapinga mabadiliko ya aina yoyote yale katika uendeshaji wa mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Zanzibar.

Kwa lugha ya sasa unaweza ukaliita kundi la Wahafidhina. Kundi la Frontliners lilikuwa na vijana, damu mpya iliyoingia katika uongozi wa Chama na SMZ. Kundi hili lilitaka mabadiliko katika uendeshaji wa mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Unaweza ukaliita kundi la Reformers.

Uchaguzi wa viongozi wa kitaifa (Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa) wa 1982 ulishuhudia msuguano mkali kati ya makundi hayo mawili. Nia ya Liberators ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Frontliners hawaingii katika Halmashauri Kuu ya Taifa. Nia ya Frontliners ilikuwa ni kuhakikisha damu mpya inaingia katika kikao hicho kikuu cha maamuzi cha Chama ambacho wakati huo kilikuwa ndio kimeshika hatamu zote za uongozi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bahati njema Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, kwa busara zake, uliwaingiza watu kutoka makundi yote mawili katika NEC na, baadaye, NEC ikawaingiza watu kutoka makundi yote mawili katika Kamati Kuu.. Frontliners walishukuru kuona kuwa miongoni mwao walifanikiwa kuchaguliwa kuingia katika vikao vyote viwili vikuu vya maamuzi vya Chama.

Kwa upande mwengine, Liberators hawakufurahi. Liberators hao walishaweka shinikizo kwa Mzee Aboud Jumbe (ambaye ndiye chanzo cha kuingiza damu mpya katika CCM ya wakati huo) kuwa vijana aliowaingiza watakujamgeukia na kuwaondoa wao, Liberators, na yeye mwenyewe katika uongozi. Inaelekea Mzee Aboud Jumbe alishawishika na shinikizo hilo, na hivyo naye, kwa njia zake (nyuma ya pazia), alitaka kuona kuwa Frontliners hawaingii katika NEC na Kamati Kuu ya Chama ambako pengine wangekuwa na ushawishi katika maamuzi ya sera za Chama. Frontliners walipoingia, ikawalazimu Liberators na Mzee Aboud Jumbe kutafuta njia nyengine ya kuweza kuwazingira ili, ikiwezekana, waweze kuondolewa katika ramani ya uongozi wa Chama na Serikali.

Hivyo basi, mara baada ya kikao cha Mkutano Mkuu wa Taifa kumalizika mwezi Novemba, 1982, Mzee Aboud Jumbe aliwataka Wajumbe wote wa NEC kutoka Unguja akutane nao Unguja, na Wajumbe wote wa NEC kutoka Pemba akutane nao Pemba. Katika mikutano hiyo, hotuba ya mwalimu wangu, Mzee Aboud Jumbe, ilitushtua wengi. Mzee Aboud Jumbe alishtumu kuwa kuna watu wanaoleta uchochezi kutaka kuvigawa visiwa vya Unguja na Pemba; kutaka kuigawa mikoa, yaani mkoa mmoja dhidi ya mwengine katika kila kisiwa; kutaka kuzigawa wilaya, yaani wilaya moja dhidi ya nyengine katika kila mkoa; na kutaka kuvigawa vijiji, yaani kijiji kimoja dhidi ya chengine katika kila wilaya. Akamalizia kwa kusema kuwa watu hao watahukumiwa na kuonja kile alichokiita “Revolutionary Justice”

Hili lilitushtua wengi, hasa sisi vijana wa wakati huo. Tukakumbuka historia ya Zanzibar tangu Mapinduzi ambapo watu walioshukiwa kuwa wapinzani wa serikali, na hasa wasomi, walivyoshughulikiwa kwa kuhakikisha kuwa wanatoweka kabisa. Khofu yetu ikawa jee, hawa wazee si wamekusudia kuturudisha huko huko tulikotoka? Tukasema kama hatukuchukua hatua za kichama kulizuia hili, basi kuna uwezekano wa historia kujirudia na watu wasiokuwa na hatia kupotea kwa kile kinachodaiwa kusimamisha “Revolutionary Justice”

Hivyo baadhi yetu tuliokuwa Wajumbe wa Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama, hasa sisi kutoka Zanzibar, tukamfuata Mzee Rashid Kawawa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM na Mwenyekiti wa Sekretarieti na kumueleza khofu yetu hiyo. Mzee Kawawa akatuelewa na akaamua iletwe agenda juu ya suala hilo katika kikao kilichofuata katika Sekretarieti. Agenda ikaletwa. Ikajadiliwa kwa mapana yake, kisha ikawasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu. Kamati Kuu ikaamua kuunda timu mbili kwenda kuchunguza madai yaliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Aboud Jumbe. Timu moja ikaagizwa kufanya uchunguzi katika kisiwa cha Unguja, na timu ya pili ikaagizwa kufanya uchunguzi katika kisiwa cha Pemba. Timu moja iliongozwa na Marehemu Moses Nnauye na ya pili iliongozwa na Mheshimiwa Alfred Tandau.

Baada ya uchunguzi, timu zote mbili zikawasilisha taarifa zao katika kikao cha Kamati Kuu. Timu zote mbili ziliona kuwa madai ya Mzee Aboud Jumbe hayakuwa na msingi. Hivyo Kamati Kuu ikamsihi Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Mwenyekiti wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Aboud Jumbe, kuzuia kuchukua hatua zozote zile ambazo zingeweza kusababisha ukiukwaji na uvunjaji wa haki za binadamu dhidi ya raia.

Inavyoonekana, hili halikumpendeza mwalimu wangu, Mzee Aboud Jumbe. Alihisi kuwa Chama, na Muungano unamuingilia katika kutekeleza azma yake na ile ya Liberators ya kuisafisha safu ya uongozi wa Chama Zanzibar kwa kuwaondoa kwa njia yo yote ile Frontliners na vijana wenye mawazo mapya .

Kipindi hicho kulikuwa na mjadala ulioanzishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba. Mzee Aboud Jumbe na timu yake wakaona kuwa waitumie nafasi hiyo kufanya kampeni kabambe kutaka muundo wa Muungano ubadilishwe. Sisi wa Frontliners tulitafsiri kuwa kampeni hiyo madhumuni yake ni kutaka kubadili muundo wa Muungano ili kundi la Liberators lipate uhuru zaidi, nguvu zaidi, na madaraka zaidi, ambayo, kwa mawazo yetu, yangetumika dhidi ya watu wenye mawazo mapya na ambao walionekana kama ni tishio kwa Liberators. Tulitafsiri kampeni hiyo kuwa na agenda iliyojificha ya kutaka kujiimarisha na kujichimbia katika madaraka kundi la Liberators ili kulinda “status quo.”

Ni kwa msingi huo ndipo mimi na wenzangu wa Frontliners tulimpinga Mzee Aboud Jumbe. Ifahamike kuwa hatukupinga dhana ya serikali tatu! Tulipinga nia iliyojificha ya Mzee Aboud Jumbe na wenzake ya kuibua agenda hiyo. Tulipinga njia zilizotumika katika kuisimamia na kuiendesha agenda hiyo. Ndio maana mara baada ya Chama cha Wananchi, CUF, kuundwa, tukabuni sera ya muundo wa Muungano wa serikali tatu. Ikumbukwe kuwa wengi wa waasisi wa CUF walitokana na kundi la Frontliners.

Ingalikuwa kulikuwa na nia njema, Mzee Aboud Jumbe angetuita, walau baadhi yetu na kutaka mawazo yetu. Nina hakika wengi tungekubaliana naye na tungezungumzia mkakati wa kulikabili suala hilo. Mimi nina hakika tungekwenda Kamati Kuu na baadaye Halmashauri Kuu kama uongozi wa Zanzibar ulioungana, wenzetu wa Bara wasingeweza kutupuuza. Na hapa niseme, tena kwa masikitiko makubwa, kwamba hili ndio limekuwa tatizo letu Wazanzibari. Wazanzibari tuna madai ya msingi katika Muungano. Lakini tunashindwa kuyasimamia madai yetu hayo hadi kupatikana mafanikio kwa kuwa tumekubali kugawiwa na tumegawika. Kugawika huko hakuyanufaishi maslahi ya Zanzibar.

Nitoe wito, kupitia gazeti lenu, kwamba wakati umefika kwa Wazanzibari bila kujali tafauti zetu za kiitikadi, kuungana ili kusimamia, kutetea na kuendeleza masilahi ya Zanzibar na watu wake katika Muungano.

Kwa kumalizia basi, kwa maoni yangu, Zanzibar ni nchi. Zanzibar ni taifa. Zanzibar ni dola.

Zanzibar ni nchi kwa sababu ni eneo lenye mipaka inayotambulikana na Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia ina watu wanaotambulika.

Zanzibar ni taifa kwa vile Wazanzibari kwa ujumla wao wanatambulikana kuwa na mila na utamaduni wao. Wazanzibari wanaweza kutafautishwa na watu wa sehemu yoyote nyengine duniani. Taifa la Wazanzibari lina uhai na ni taifa endelevu.

Zanzibar ni dola kwa vile kuna mamlaka iliyowekwa na Katiba zote mbili, yaani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar [SMZ] yenye madaraka yasiyoweza kuingiliwa na chombo chochote chengine katika mambo yasiyo kuwa ya Muungano katika nchi ya Zanzibar. Ni kweli kuwa Zanzibar haina jeshi lake wala polisi yake. Lakini ni kweli pia kuwa Zanzibar ina vyombo vyake vyengine vya maguvu vilivyoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Katiba inayotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sheria za Zanzibar. Hivyo ni vyombo vya maguvu vilivyo halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Ni kweli kuwa suala la Mambo ya Nje ni jambo lililomo katika orodha ya Mambo ya Muungano. Lakini ni kweli pia kuwa suala la mahusiano ya kimataifa halijawahi kuingizwa katika orodha ya Mambo ya Muungano. Hivyo Zanzibar ina uwezo kamili wa kushirikiana na mataifa na mashirika ya kimataifa katika kuwaletea maendeleo Wazanzibari. Ni bahati mbaya kuwa Serikali ya Muungano imejaribu na inaendelea kuiminya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusimamia ushirikiano wa kimataifa. Mambo kama haya ndio yanaoudhoofisha Muungano wetu.

Kama kuna watu wanasema kuwa Zanzibar sio nchi, basi wasiishie hapo. Waeleze jee Zanzibar ni Mkoa, au ni Wilaya, au ni kijiji au ni kitongoji?
--

Saturday, December 10, 2011

New Africa Hotel 1936

New Africa Hotel, Dar es Salaam,Tanganyika
Wadau hebu cheki New Africa Hotel ilivyokuwa mwaka 1936 enzi za Ukoloni!

Sunday, December 04, 2011

Ni lini tuta sherehekea Uhuru wa Tanganyika?

Bendera ya Tanganyika

Imeandikwa na Mdau VM

Ni lini tuta sherehekea Uhuru wa Tanganyika?
Kila mwaka utasikia sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara!!!!!
Ni lini sasa tutasherehekea Uhuru wa Tanganyika? Hivi kweli huu ni umbumbumbu wa Historia kwa miongoni mwetu watanganyika au ni unyanyapaa wa Tanganyika, na ustaarabu kwa Z'bar? Mimi Sipendi!

Mapinduzi ya Z'bar yapo kila Januari 12 tena kwa mbwembwe zote, sherehe za kumbukumbu ya Muungano zipo kila Aprili 26 kwa kwa kila hamasa, lakini Uhuru wa  Tanganyika ni lini??? Mimi sipendi!!!

Tunaambiwa eti Uhuru wa Tanzania Bara! Sipendi!!!
Ok. Potelea mbali. Sasa hivi Tanzania Bara imefikisha umri gani? Miaka 47 au 50? Hivi Tanzania Bara haikuzaliwa Aprili 26, 1964. Sasa hiyo ni miaka mingapi, 50 au 47? Mi sipendi kabisa kuvuruga na kuchanganya historia.

Sipendi watoto wetu, wadogo zetu, kupotoshwa kwa makusudi kuhusu Uhuru wa Tanganyika! Tunawadanganya ili iweje? Sipendi kabisa!!!.
Siendi kwenye sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara wala siangalii televisheni kuhusu uhuru huo, hadi ntakapo sikia tunaazimisha miaka kadhaa ya Uhuru wa Tanganyika! Labda mnisaidie kuelewa, vinginevyo hakuna. Asante.

Vins

Tuesday, March 08, 2011

Wafungwa wa Kike Tanganyika

Hii picha ya Wafungwa wa Kike, ulipigwa mwaka 1895, Dar es Salaam, Tanganyika. Sijui walikosa nini maskini!

Mnaweza kuiona hapa:
http://www.zazzle.com/women_convicts_tanganyika_1895_poster-228015262999522213

Waganga wa Kienyeji wa Tanganyika



Hii picha imepigwa Tanganyika mwaka 1936. Sijui ni waganga wa kienyeji wa kabi la gani. Picha inapatikana hapa:http://www.fotosearch.com/IST515/1631353/

Tuesday, December 09, 2008

Uhuru 9-12-61

Bendera ya Tanganyika


Uhuru wa Tanganyika ulikuwa Disemba 9, 1961. Ni miaka 47 iliyopita. Pichani ni mezi kadhaa kabla ya uhuru mwaka 1961, Mwalimu akiwa na Mama Barbro Johansson nyumbani kwake Kahororo, Bukoba. ( Picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa Blog)

Friday, December 05, 2008

Askari




Bila shaka wengi wenu mna ndugu ambao walikuwepo vikosi vya askari. Hii picha ya kikosi cha askari kilipigwa enzi za mkoloni (mjerumani) mwaka 1914. Sijui ni Mirambo Barracks, Tabora hapo?

Tuesday, May 20, 2008

Polisi Enzi za Tanganyika


6th February 1963: The Tanganyika Police Guard of Honour line up beneath Mount Kilimanjaro, during the Afro-Asian Solidarity Conference in Moshi, in modern Tanzania. (Photo by Keystone/Getty Images)

Saturday, April 26, 2008

Miaka 44 ya Muungano

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya muungano rasmi, April 26, 1964. Siku hiyo Tanzania ilizaliwa.

*****************************************
Wadau nawauliza hivi - huo udongo uko wapi?

Mnahabari kuwa jina la Tanzania ilipatikana katika mashindano. Watu waliombwa wapeleka majina ya nchi mpya. Tanganyika + Zanzibar. Karibu tuitwe TANGIBAR!

Leo namwomba Mungu kuwa tuendelee kujivunia uTanzania wetu. Tuendelee kukaa kwa amani na utulivu na tuendelee kuwa mfano na nyota barani Afrika. AMEN

Thursday, March 06, 2008

Hapo zamani za Kale

Hao ni waarusha
Hii picha ilipigwa Mikindani, Tanganyika. Wanasema eti kabili yake ni Makonki. Wanamaana Makonde? Hiyo fesheni ya kupanua mdomo umepitwa na wakati.

Kuna picha kibao za Afrika toka miaka ya 1880's hapa:
old-photos.blogspot.com/2007_03_01_archive.html

Tuesday, February 26, 2008

Binti Daria Adamu Juma


Hii habari inatoka kwa mdau aliyeona hii picha ya 'Mzungu na mke wake 1905' . Bado hatujajua ni akina nani hao katika picha hii. Lakini Bwana Komba Muhili ameniletea habari za mzaa babu yake aliyelazimishwa kuolewa na mjerumani wakati huo huko Songea.
********************************************************************************

Binti Daria Adamu Juma


Imeandikwa na Komba Muhili

Hii picha inanikumbusha marehemu Mama mkubwa yaani Bibi yake Baba. Alikuwa anaitwa daria Binti Adamu alifariki mwaka 1981. Tulikuwa tunahisi alifariki akiwa na miaka 107. Alikuwa akitusimulia Habari za wajerumani wakati akisimulia alikuwa analia sana mpaka tunamwambia asilie kwani atatupa majonzi sana.

Yeye na familia yake waliishi katika Kijiji kimoja kiitwacho Rumecha, Songea wakati wa vita ya Maji maji alikuwa na miaka kama kumi na sita alikuwa amewekwa ndani si kama amefungwa amewekwa ili achezwe unyago pune vita ikaanza na wajerumani wakvamia kijiji chao.

Klichotokea ni cha kusikitisha baadhi walitekwa na wengine walikimbia cha kusikitisha zaidi yeye alikuwa mwali ndani akuweza kukumbia pamoja na familia yake ilibidi wakamatwe kilichotokea wazazi wake na nduguzake wote walipigwa Risasi na kufa papo hapo. Huku akiwaona wazazi wake wakiuliwa na wajerumani.

Kilichotokea yeye alichukuliwa na kamanda mmoja wakijerumani akawa mke wake bila ridhaa yake mwenyewe. Alikuwa aklia sana akikumbuka wazazi wake na nduguze alikaa na yule mjerumani zaidi ya miaka kumi na tano kama mke na mume kwani akuweza kufanya kitu chochote. Kilichotokea vita ilivyoisha tu yule mzungu akaenda nae Ujerumani na wakaishi huko na kubahatika kupata watoto wawili wakiwa na asili ya kizungu.

Baada ya kuzaa mtoto wa pili alilia sana na akaanza kususa hata kula akiulizwa shida nini akasema nakumbuka sana nyumbani hasa ndugu zangu. Basi yule mjerumani alichofanya alikuja nae mpaka Tanganyika akamuacha Bandari salama mwaka 1918 wakati vita ya kwanza ya Dunia ilivyokwisha.

Alivyofika hapa nyumbani alibusu ardhi ya Tanganyika huku akilia sana kwa uchungu alikuwa anafikilia watoto wake aliowaacha Ujerumani. Basi alifanikiwa kufika kijiji kwao kule Rumecha,Songea lakini akumfahamu mtu yeyote kilichotokea pale alipokewa na kukaribishwa kwa furaha.

Sasa kuna Mtu mmoja alitokea kumpenda sana Daria kilicho tokea pale alikubali kuolewa na yule mzee alikuwa anaitwa muhili komba na hatimae wakabahatika kupata watoto watano. Kati ya hao mmoja wapo ndio babu yangu mzaa baba na bahati nzuri niliishi nae. Mama mkubwa takribani miaka mitatu nikiwa na akili chakushangaza alikuwa mzee sana lakini meno yake yote yaliku meupe na hajang`oa hata moja.
Kwa kusema ukweli alikuwa mzuri sana nafikiri hata yule Mjurumani alimpenda kwa uzuri wake .Nimeona niwape kisa hiki ili nanji muone huko tilikotoka.

Monday, November 19, 2007

Tanganyika Enzi Za Mjerumani 1885-1918

Mjerumani asema "Tulia niwapige picha!"
Tumetoka mbali!


Hospitali ya Tanga 1914.

Tanga kulikuwa na mapigano makali 1914.
Hao wanawake walifungwa kama watumwa. Sikuweza kupata maelezo ya kisa cha wao kunfungwa na mnyororo.

Ocean Road Hospital ilijengwa na Mjerumani 1897.


Zamani ilikuwa kawaida kwa mabibi zetu kutembea vifua wazi. Hii picha ilipigwa maeneo ya Bukoba



" WHITE HUNTER" Waindaji wa kizungu waliua wanyama wengi kweli bila huruma!


Mjerumani alivyowakuta waCHAGGA

Kwa habari zaidi someni:


Thursday, November 15, 2007

Enzi za Mjerumani Tanganyika 1885-1918

Hii picha ilipigwa 1903. Sijui ni shule gani Dar. Je, ni shule ya Uhuru? Hakuna msichana hata moja darasani!
Mjerumani alivyowakuta mabibi na mababu zetu.

Hii picha ilipigwa 1910. Hotel zu Stadt - Sijui ilikuwa mtaa gani Dar?

Nani kasema Mjerumani mbaguzi! Huyo njemba alifanikiwa kwenda Ujerumani na kujiunga na jeshi lao huko huko!

Waafrika walikuwa wanabeba wazungu bila wasiwasi. Wazungu hawakupenda punda kwa sababu walikuwa wana jamba ovyo.

Kabla ya King's African Rifles (Mwingereza) kulikuwa na German Native Infantry (Mjerumani). Hao native infantry walipgana katika vitu kuu ya dunia ya kwanza (World War I).

Kwa habari na picha zaidi someni:

http://germanhistorydocs.ghi-dc.org/sub_image.cfm?image_id=1433&language=english