Saturday, August 09, 2014

Kibonde wa Clouds FM Akamatwa na Polisi Leo

Ni mara chache sisi waandishi wa habari, tunakuwa habari!

********************************
 Habari na picha kutoka FACEBOOK:

Askari wa Trafiki Akimkamata Ephraim Kibonde

Ephraim Kibonde ndani ya Lock Up


Mtangazaji Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.

Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

5 comments:

Anonymous said...

Sheria msumeno!

Anonymous said...

DAH! Mpanda viazi huvuna viazi ndivyo nilivyofundwa!

Anonymous said...

Hana maana huyo acha wa mdake, wamemtumia sasa kondomu tupa huko

Anonymous said...

Samahani suala la kulalamikia wawekezaji mimi linanikera kwa kuwa ninajiuliza-nani amekataza matajiri wetu wanaovuma nchini na Africa kuungana na kuwekeza wakatoa na ajira kwa vijana? Au-tajiri kufanya hivyo kama alivyofanya Dangote Mtwara au hao makaburu nchini? nani anakuambia wewe uuze mitumba ya chupi, viatu barabarani halafu utumie hela kwa ulevi, bangi? nani kakukataza usiende kulima nyanya au usilime kijijini ulipo ukaungana na wenzako, mkapata kagari ka kubeba mizigo mkaleta nyanya na matikiti dar, mkanunua lori baadae na kusafirisha vitu nchi jirani na mkakua kibiashara kama Shigongo? mbona matajiri wa zamani watu wazima sasa hawana elimu kubwa? Wasomi wa sasa vipi na benki hutangaza mikopo?
>
>Prof Muhongo alisema-watanzania kuwekeza hamuwezi labda katika soda za rangi tu!! Umeona huu ni uongo? Angalia sera na sheria ya uwekezaji. Google Tanzania National Investment Centre (TIC). Angalia pia mashamba makubwa ya kazati ambayo yana beacons, surveyed wakati wa ukoloni na ni ya GVT baada ya ukoloni. angalia ya Katani tu kuanzia Ubena Zomoni kwenda Kingolwira Morogoro au kuelekea Tanga na kuelekea Korogwe-Same-Mwanga-Moshi.Waliochukua mashamba hawajawekeza mikopo wamejenga magorofa wanapangisha kwa dola DSM na miji mingine. wengine wametoroka nchini (kesi ya Mhindi mtanzania Hale). Ni mishamba hiyo hadi Tongoni-Pangani Tanga. Maeneo yaliyopewa wanakijiji kulima mfano-Vijiji vya ukitoka Segera hadi unamaliza Sisi kwa sisi kuelekea mabwawa ya umeme hale-Pangani 1 and 2 wanalima? wamejenga lodging. nani anamkataza tajiri Mzawa asiwekeze katika ardhi productively akatoa na ajira sio mpaka aje Dangote kutona Nigeria aweke kiwanda cha cement? Si
> wangeungana mfano Hood, Abood, manji, Mengi etc kuunda a multinational company, wakachukua maekari ya former GVT plantation zinazovamiwa na kujengwa majumba kiholela, au mifugo mamilioni kufanya degradation wakaiomba NHC kujenga houses za aina mbali mbali na kujengesha processing industries na kuhamishia omba omba wa mitaani, walio na ulemavu hawana matunzo lakini wanaweza kufanyakazi wakawa wanafanya kazi za uzalishaji. mashamba hayo yakawa yanazalisha vyakula vya kuuza ndani na nje ya nchi, mapambo na vifaa vya katani, maembo na matunda mengine ya muda mfupi. wanaweza wakaanzisha hata fish ponds (nchi kavu na za mikokoni baharini); mifugo ya kisasa kwa kuwapa uwezo wafugaji kufanya hivyo badala ya kuzurura mwaka hadi mwaka kusababisha mapigano vijijini, kuathiri kilimo na food security na kuleta vifo na vilema.
>
Unawawapa uwezo kwa elimu, kuweka extension services wafugaji wajenge maboma na kupanda majani ya malisho; livestock multiplication centres zipo TZ kimkoa zingetumika kutoa elimu hao matajiri wanalipia hizo extension na ufuatiliaji kisha wao wananunua products na kuzichakachua kiwandani. Nyama, maziwa, ngozi bora etc. Mbona hata Tv zao wengine zinaonyesha sineam familia za mashamba na ufugaji? Akija mchina, Mcanada kuchukua mashamba hayo ya former GVt institutions (kahawa, Minazi, katani, Mikorosho, mahindi, Ngano etc) manawavamia na kudai unavyodai hapa. Mbunge au Diwani anadiriki kuwashauri wananchi wasihame mabondeni, wafugaji wahamaji wasibugudhiwe kwani hiyo ndio mila yao (karne hii ya structural adjustment na ya liberal competitive economy kurudi); kiongozi mjinga na mpumbavu anasema hivi wakati tax payers wa ulaya hawataki tena kutupa grants za huduma za maisha yetu wakati kwetu kuna kila kitu ila tumebweteka.

Anonymous said...

I dont believe this, Huyu ni kibonde yule ninayemjua anayehasisha watu wabaki njia kuu au ni kibonde mwingine???