Showing posts with label Hillary Clinton. Show all posts
Showing posts with label Hillary Clinton. Show all posts

Tuesday, June 03, 2008

Obama atakuwa Mgombea wa Democrats!!!!


Leo Senator Barack Obama amefanikiwa kupata kura za kutosha kuwa mgombea wa Democrats katika uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani. Ni jambo la kihistoria kwa mtu mweusi kutwaa ugombea. Senator Hillary Clinton, anasema yuko tayari kuwa makamu wake akitaka.

Mungu amlinde maana wabaguzi bado wako wengi hapa Marekani. Naomba Mungu kuwa January 2009 Rais Obama ataapishwa! Huyo McCain anasema ataendeleza hiyo vita vya Iraq hata miaka 100, ana wazimu nini! Kwa heri Bush na Cheney!

Saturday, May 24, 2008

Obama Hatarini?!

Kava ya mbele la gazeti Roswell Beacon (Georgia) iliyotoka May 15, 2008


Ukiwa mgombea rais mweusi uko hatarini kuuliwa. Kwa kujua hivyo, Secret Service walitoa ulinzi kwa mgombea rais wa chama cha Democrats mapema. Obama amekuwa akilindwa kwa mieza 18 sasa.

Nchi hii kuna wabaguzi hasa. Yaani white supremacists wanaoamini kwamba mtu mweusi si bindamu na hasthili kuwa na chochote. Huwezi kuamini kuwa mwaka 2008 bado wapo. Sehemu zingine hapa Marekani huwezi kwenda na kuwa na uhakika wa kutoka na maisha yako ukiwa mweusi.

Ajabu, mpinzani wa Obama, Senator Hillary Clinton, amesema kuwa si ajabu watu kugombania nafasi ya mgombea hadi mwezi June, na kusema habari ya kuuliwa kwa Senator Robert F. Kennedy mwaka 1968. Sasa watu wameshutuka! Wametafsiri kuwa Clinton aikuwa na maana kuwa wakimwua Obama, yeye yupo kushika nafasi ya mgombea rais. DUH!

Kwa kweli watu wamemkasirikia Hillary kwa maneno yake.

Kwa habari zaidi someni:

http://blogs.abcnews.com/politicalpunch/2008/05/assassination-d.html

http://afp.google.com/article/ALeqM5jbMPoA_wjG3rgLbbsD-mT30oWfZA

http://ap.google.com/article/ALeqM5g-qGLDs-gAnZiUXD2NU51ry3j3dwD90RJVIO0

Thursday, May 08, 2008

Wazungu Wananitaka Mimi - Hilary Clinton


Yaani siku hizi za 'political correctness' si vizuri hata kusema kuwa Senator Obama ni mwanaume mweusi. Watu wanataka kuonekana kuwa si wabaguzi. Leo maneno ambayo watu walikuwa wanangojea kusikia yametamkwa na Hilary Clinton. Kasema kuwa wazungu Marekani wanamtaka yeye kuwa rais siyo mtu mweusi! DUH!

Na bado, sehemu kama Indiana kuwa watu ambao walisema kuwa hawawezi kumpigia mtu mweusi kura. Basi tu, kwa vile ni mweusi. History ya ubaguzi Marekani ni mbaya sana na ingawa siku hizi hali si mbaya kama ulivyokuwa bado upo!
Na Obama akiwa mgombea tutazidi kusikia maneno ya kibaguzi kutoka kwa watu.

Watu watauliza, "Unataka N-iga awe raisi wenu?" Na bado! Pia Hao masekreti service wamlinde maana wapo wale wazungu wabaguzi wenye siasa kali wanaotaka kumtungua, kisa mweusi!


****************************************************************

May 8, 2008

Clinton touts support from 'white Americans'


Posted: 12:03 PM ET


(CNN) — In what appear to be the New York senator's most blunt comments to date regarding a racial division in the Democratic presidential race, Hillary Clinton suggested Wednesday that "White Americans" are increasingly turning away from Barack Obama’s candidacy.

"I have a much broader base to build a winning coalition on," Clinton said in an interview with USA TODAY.

Clinton cited an Associated Press poll "that found how Senator Obama's support among working, hard-working Americans, white Americans, is weakening again, and how whites in both states who had not completed college were supporting me."

"There's a pattern emerging here," she said.

Exit polls from Tuesday's primaries in Indiana and North Carolina show Clinton won about 60 percent of the white vote in both states. That percentage is down from the Ohio primary on March 4, in which Clinton won upwards of 65 percent of the white vote. Meanwhile, Clinton garnered 63 percent of the white vote in Pennsylvania on April 22.

Speaking with the paper, Clinton rejected the notion her comments were racially divisive in any way.

"These are the people you have to win if you're a Democrat in sufficient numbers to actually win the election," she said. "Everybody knows that."

Obama spokesman Bill Burton called Clinton's statements "not true and frankly disappointing."

From: CNN Ticker Producer Alexander Mooney

Wednesday, March 05, 2008

Senator Hillary Clinton Afufuliwa! - Uchaguzi 2008


Majuzi watu walikuwa wansema kuwa ni bora Senator Hillary Clinton, ajitoe katika mashindano ya kugombania urais wa Marekani. Hiyo ni baada ya Senator Barack Obama, kushinda katika states 12 mfululizo.

Jana Senator Clinton alishinda states za Ohio na Texas ambazo zina wajumbe wengi watakao piga kura katika mkutano mkuu wa Democrats mwezi Agosti. Hao ndo wanampitisha mgombea. Pamoja na ushindi wake Obama bado ana kura nyingi.

Kwa kweli sijafurahi hizi wiki mbili zilizopita kuona jinsi Mama Clinton alivyochafua jina la Obama. Mara aseme hawezi kuwa na uhakika kuwa si mwislamu. Na alifanya hivyo maksudi kwa vile alijua waMarekani ni waoga na waislamu baada ya mashambulizi ya 9/11. Halafu walifufua ile picha aliyopiga Kenya amevaa nguo za kiSomali mwaka 2006. Na kuna maovu mengine ambayo kampeni yake ilifanya.

Naomba mjue kuwa ubaguzi bado upo hapa Marekani. Hasa katika hizi states za Kaskazini. Sijui kama mlisikia yaliyotokea jana huko Ohio kwenye maeneo ya weusi. Weusi walijitokeza kwa wingi kupiga kura lakini walishindwa. Mfano, sehemu moja walikuwa na kura 50 na watu 300 walijitokeza. Hivyo watu wengi walishindwa kupiga kura. Ilibidi watu wa Obama wamwombe jaji aamuru shemu za kupiga kura zikae wazi kwa saa moja zaidi ili watu wapate nafasi ya kupiga kura. Matatizo kama hayo yalitokea hapa Massachusetts kwenye maeno ya weusi wakati Gavana wetu, Deval Patrick, alivyogombania.

Pia huko Ohio kulikuwa na matatizo kibao, hitilafu za mashine, matishio ya mabomu na mengine.
Halafu washenzi kama Rush Limbaugh, waliomba marepublicans wampigie Senator Clinton kusudi Obama asishinde. Alisema Clinton akishinda basi atazidi kumpaka matope Obama. Siasa bwana!

Leo, Hillary anadokeza kuwa kama atachuguliwa kuwa mgombea wa Democrats atamchagua Obama kuwa running mate, yaani makamu wake. Sijui kama mimi ningekuwa Obama ningekubali maana huyo Mama Clinton ameonyesha ana ukatili ndani yake. Yuko tayari kufanya chochote ili ashinde.

Pia Bush akiondoka January 2009, ataacha nchi na hali mbaya sana ya kiuchumi na kila kitu. Ambaye atashinda atakuwa na kazi kubwa mbele yake. Mungu ambariki atakayeshinda.
Kwa habari zaidi someni:

Tuesday, February 26, 2008

Kampeni ya Hillary wazua Mambo - Eti Obama ni Msomali!

Laura Bush dons Muslim robes and head scarf
President Bush dons foreign attire
This is what Hillary's campaign is using for fear mongering. They claim that Obama really is a Muslim in hiding! By the way, Obama is not a Somali! That is Somali attire he is dressed in!
President Bill Clinton dons African attire
Woops! Hillary and her daughter Chelsea wear Muslim headscarves!
Hillary dons a Head Scarf!
Now we know that Hillary must be affiliated with terrorists!


Hii kampeni ya uchaguzi Marekani safari hii imezidi kuwa chafu mpaka inatia kichefuchefu! Mara kuna 'plants' za kuharibu ofisi za kampeni, mara kuna wengine ambao kazi yao ni ku-twist ukweli.

Leo nimesikitika sana, tena mno, kusikia baadhi ya wazungu wakisema kuwa kumbe ni kweli Obama ni mwislamu. Oh kumbe yuko Al-Qaeda! Oh, kumbe kaelekea zaidi kwenye Uislamu. Kwenye WCVB TV Channel 5 hapa Boston, mtangazaji alisema kuwa kwenye hiyo picha Obama kavaa nguo za Middle East!

Kisa, kampeni ya Hillary wanazungusha picha kwenye neti ya Obama akiwa amevaa nguo za wazee wa kiSomali. Picha ilipigwa alipotembea huko Kenya mwaka 2006. Hivi Obama si MJaLuo?
Hillary anatafuta kura kwa nguzu sasa huko Texas na Ohio. Alishindwa kwenye uchaguzi wa awali kule ndo mwisho wake katika kugombea. Lakini watu wanasema hii tactic ya kutoa picha itamwangusha Hillary haitamsaidia. Wanasema kuwa kumbea huyo mama ni bytch na yuko tayari kufanya kitu chochote ili ashinde!

Nimebandika picha za waheshimwa wakiwemo Hillary wakiwa wamevaa hijab na nguo zinge zi kiutamduni.

Kwa waongea kimombo:

Hey you ignoramuses out there, Mr. Obama's father is from the Luo tribe ofKenya! He is not a Somali. He was just visiting a group of people who live in Kenya and they showed him their respect!

Plus it is a sign of disrespect no to don the attire of the people you are visiting in some foreign lands. Take a look at the photos above!

Kwa habari zaidi someni:

http://youdecide08.foxnews.com/2008/02/25/photo-showing-obama-in-somali-garb-circulated-by-clinton-campaign-source/

http://www.news.com.au/couriermail/story/0,20797,23277403-952,00.html?from=public_rss

http://www.bayoubuzz.com/News/US/Politics/President_Race_2008/Hillary_Clinton_Over_Hill_With_Obama_Somali_Photo__5883.asp

http://bigheaddc.com/2008/02/25/drudge-falsely-accuses-clinton-of-obama-photo-ties/

Wednesday, February 06, 2008

Uchaguzi wa wagombea Rais Marekani - Hakuna mshindi kamili

Mamilioni ya waMarekani walipiga kura zao jana kupata mgombea rais wa upande wa Democrats na Republicans. Hakuna mshindi kamili kwa pande zote.

Hivi kwa Dems, bado tunaye Obama na Clinton. Kwa Republicans bado wapo Huckabee, Romney na McCain.

Kwa habari zaidi soma:

http://www.cnn.com/2008/POLITICS/02/06/super.main/index.html

Tuesday, February 05, 2008

Leo ni Super Tuesday! - Nani atagombea Uraisi wa Marekani!








Leo mamilioni ya waMarekani wanajitokeza kupiga kura. Wanaiita siku ya leo, Super Tuesday. Kura wanaopiga leo zitasaidia kuchagua nani atakuwa mgombea rais kwa upande wa Democrats na upande wa Republican.

Kwa upande wa Republicans waliobaki kugombania nafasi ni Mike Huckabee, John McCain, na huyo mshenzi/mnafiki alikuwa Gavana wetu hapa Massachusetts, Mitt Romney.

Kwa upande wa wa Democrats waliobakia ni Hillary Clinton, na Barack Obama. Kuna mashindano makali sana kati ya hawa wawili. Wote wana wafuasi wengi. Huenda leo hatutajua nani kapita upande wa Democrats na itabidi tusibiri hadi siku ya Convention (mkutano mkuu wao), itakayofanyika mwezi wa nane huko Colorado.
Nadhani kuna chensi kubwa kuwa Democrats watanyakua White House safari hii. Watu wamechoka utawala wa Bush. Wanasema ameharibu nchi na hadi yake, pia kaanzisha vita isiyo na maana huko Iraq. Pia hali ya maisha kwa Marekani umekuwa mbaya, watu wanfukuzwa katika majumba yao, bei ya mafuta umepanda, hata bei ya chakula umepanda mno!
Bush aliwaahidi waMarekani kuwa kama atakuwa Rais bei ya mafuta utashuka. Wakati huyo ni kama $1.80 a gallon. Leo ni $3.10! Wajinga ni nani! Hao waliompigia kura Bush kwa hasira wanaweza kupiga kura zao kwa Democrats! Warudishe hadi ya nchi ilivyokuwa enzi za Rais Clinton!

May the Best Man/Woman win!

Wednesday, January 09, 2008

Hillary Clinton ashinda New Hampshire!


Senator Hillary Clinton ameshinda uchaguzi wa awali huko New Hampshire kwa upande wa Democrats. Senator Barack Obama, amekuwa wa pili. Matokeo yalikuwa karibu. Clinton alipata asimilia 39% ya kura, na Obama alipata asilimia 36%. Clinton sasa ni mwanamke wa kwanza kushinda uchaguzi wa awali New Hampshire.
Watu walitarajia Obama atashinda tena kwa kura nyingi. Watu wengi walishangaa kuona Bi Clinton anaongoza kutoka mwanzo. Watu wanasema huenda alivyoanza kulia juzi ulisaidia watu kuona kuwa Hillary kumbe ni binadamu kama wao. Bi Clinton aliulizwa awali kuhusu nywele zake.
Hali ya hewa New Hampshire ilikuwa nzuri na wazee wengi walitokea kumpigia kura Hillary. Vijana walioahidi kumpigia kura Obama hawakutokea. Mtangazaji moja alisema huenda walikuwa wamelewa au wamechoka kutokana na kusherekea ushindi wa Obama Iowa.
Bado uchaguzi wa awali katika states 48. Tarehe 5 mwezi Februari states 20 watakuwa na uchaguzi wa awali.
Hillary Clinton, ni mke wa Rais Clinton. Kama akishinda urais wa Marekani atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa wa rais wa Marekani, pia atakuwa First Lady wa Kwanza kuwa Rais, na Bill Clinton atakuwa mwanaume wa kwanza kuwa First Gentleman na ambaye aliwahi kuwa rais.

Kwa habari zaidi someni:

Tuesday, January 08, 2008

Inaelekea Obama kashindwa New Hampshire

Inaelekea Senator Hillary Clinton, ni mshindi kwa upande wa Democrats huko New Hampshire kwenye upande wa Democrats. Senator Obama amekuwa wa pili.

Hillary ana 39% na Obama 36% za kura. Kwa upande wa Republicans Senator John McCain ameshinda.

Bado uchaguzi katika jimbo 48 zingine za Marekani.

Saturday, December 01, 2007

Ajisalimisha


Kichaa aliyeteka ofisi ya kampeni ya Senator Hillary Clinton huko Rochester, New Hampshire, Leeland Eisenberg, alijisalimisha jana jioni. Aliachia mateka wote huru kabla ya kujisalimisha kwa polisi.

Eisenberg alisema alifanya hivyo kwa sababu anahitaji matibabu ya ugonjwa wa akili na hana pesa za kulipia. Alisema watu wenye ugonjwa wa akili wanateseka Marekani hasa kama hawana bima au hela za kulipia matibabu.
Senator Clinton anasema kuwa anaelewa kuwa Eisenberg aliteka ofisi yake kwa ajili ya kutoa mwanga kwenye hiyo swala. Alisema pia kuwa anashukuru hakuna mtu aliyeumia au kufa katika tukio hilo.
Kwa habari zaidi someni:

Friday, November 30, 2007

Ofisi ya Hillary Clinton imetekwa nyara New Hampshire

Senator Hillary Clinton
UPDATE: 4:14Pm Eastern - Mateka wote wawili wameachiwa huru
*********************************************************************************

Watu wawili wametekwa katika ofisi ya mgombea rais wa chama ca Democrats wa Marekani, Senator Hillary Clinton. Ofisi enyewe ni ya kampeni yake na iko Rochester, New Hampshire.

Sakata umeanza saa 7 mchana huu na hivyo navyoandika bado inaendelea. Mama moja aliyekuwa ndani ya hiyo ofisi na mtoto wake wa miezi sita aliachiwa huru pamoja na mtoto.

Jamaa aliyeteka nyara ofisi amejifunga mkanda ambayo anasema ina bomu! Ofisi sasa imezungukwa na polisi, SWAT (FFU) na Secret Service. Kama jamaa hajisalimishi msishangae mkisikia kuwa jamaa katunguliwa kwa kupigwa risasi kichwani na FFU.

Pia polisi wameamuru ofisi za wagombea rais wengine maDeomcrats, Barack Obama na John Edwards zifungwe kwa usalama wa raia na wafanyakazi.

Marekani bwana!

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/11/30/clinton.office/index.html