Tuesday, June 03, 2008

Obama atakuwa Mgombea wa Democrats!!!!


Leo Senator Barack Obama amefanikiwa kupata kura za kutosha kuwa mgombea wa Democrats katika uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani. Ni jambo la kihistoria kwa mtu mweusi kutwaa ugombea. Senator Hillary Clinton, anasema yuko tayari kuwa makamu wake akitaka.

Mungu amlinde maana wabaguzi bado wako wengi hapa Marekani. Naomba Mungu kuwa January 2009 Rais Obama ataapishwa! Huyo McCain anasema ataendeleza hiyo vita vya Iraq hata miaka 100, ana wazimu nini! Kwa heri Bush na Cheney!

5 comments:

Anonymous said...

Dada chemi mimi muzungu huku sweden tumefurahi mno baada ya kupata taarifa hii leo arfajili.mungu amlinde obama ktk historia hii adimu duniani

Anonymous said...

Am proud na Obama!!!Ni black ukizingatia ana ka blood ka East Africa,Ila 2 be honesty dada Chemmy unaniudhi cc huku tunajitahidi soma newz zako ila mbona hutuonyeshi yanayojiri nyumbani Sullivan Summit au wamekukataza mafisadi maana huku USA wana majumba na mitaa ipo kabisaaa

Anonymous said...

kwanza kabisa dada chemi nakubaliana na wewe katika kumpongeza Obama, kwa sababu kwanza, ni mweusi (african background) na pili mimi binafsi nadhani ndiye mgombea aliyekuwa na sifa za kuchukua wadhifa huo mkubwa kabisa duniani.

Lakini pia da-chemi, kwa mtu wa "calibre" yako wewe, hatutegemei uje na matamshi kama, "McCain anataka kuendelea vita ya Iraq hata kwa miaka 100, ana wazimu nini?"; Tunategemea uwe umekomaa kiasi cha kuweza kuheshimu mawazo ya wengine hata kama ukubaliani nayo. Wapo wamarekani ambao wanataka vita vya Iraq viendelee mpaka marekani itakaposhinda na pia wapo ambao wanadhani kuwa vita hiyo ni "pointless". Na ndo uzuri wa democracy, kunapokuwa na opposing views wananchi watasema wanachotaka kwa njia ya kura.

Tunakumbushana tuu.

Anonymous said...

HUYU CHOTARA HANA MAANA YEYOTE SAWA NA BOY WA MAJUMBANI KASHAANZA KWAONA WAYAHUDI MIUNGU WATU WAFRIKA WAKE ANAONA KAMA MAVI MSHAMBA NA HASHINDI NAHUWAKIKA KWA ASILIMIA MIA .MAANA WHITE HOUSE MAANA NI UTAWALA WA WEUPE HATA SIKI MMOJA HAKUNA MWEUSI ATAKAEKUWA RAIS.AMERICA

Anonymous said...

...kusema kweli hatuhitaji matamshi kama haya kuhusu siasa za marekani, ila nampongeza obama kwa kunyakua kura zaidi ili aweze kuwania wadhifa ya rais kwa tiketi ya chama cha democrats. Na huyu fala asiyejua maana ya kutumia CAPS LOCK aachane na kuongea kishenzi na kueneza ujinga wake. Hiyo si busara!

(kutoka...ah! ushanijua tayari...:-D aneishi ng'ambo)