Showing posts with label Kubaka. Show all posts
Showing posts with label Kubaka. Show all posts

Wednesday, May 18, 2011

Anayedai Kabakwa na Mkuu Wa IMF Hotelini NY Atajwa

(Pichani - Mkuu wa IMF Dominique Strauss-Kahn Akiwa amefungwa pingu na kupelekwa kwenye gereza ya Rikers Island, New York)


Bila shaka mmesikia habari ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mkuu wa IMF mjini New York. Magazeti ya nje ya Marekani yametaja jina na kutoa picha ya mhudumu wa hoteli anayedai kuwa Bwana Dominique Strauss-Kahn (62) kamfanya mabaya. Inadaiwa kuwa wikiendi iliyopita katika hoteli ya Sofitel mjini New York, Strauss-Kahn alijaribu kumbaka Bi Nafissatou Diallo (32) ambaye anatoka nchi ya Guinea, Afrika Magharibi. Chumba alichofikia ni $3,000 kwa siku!

Habari zinasema kuwa Bi Diallo alienda kusafisha chumba alichofikia Strauss-Kahn. Alidhani hakuna mtu mle. Alipofungua mlango Strauss-Kahn alitoka bafuni na alimkimbiza akiwa uchi na kumfungia chumbani. Hapo Strauss- Kahn alimlazimisha kunyonya ume wake, na baadaye alimwomba Diallo amfanye huko nyuma (kufira). Yule mama alifanikiwa kukimbia na kawaambia wafanyakazi wenzake hotelini ndo wakaita polisi. Inadaiwa kuwa Strauss-Kahn alikimbia baada ya tukio na kuacha simu yake, lakin wakli wa Strauss-Kahn anasema kuwa alienda kula chakula cha mchana na binti yuake halafu baadaye alienda uwanja wa ndege.

Strauss-Kahn alikamatwa kwenye ndege huko JFK Airport ikiwa karibu inaruka kwenda Ufaransa.

Kwa sasa Strauss-Kahn amefungwa bila dhamana katika gereza la Rikers Island huko New York. Duh! Kutoka hoteli ya fahari kwenda Rikers Island ni makubwa. Sidhani kama alitegemea kuona ndani ya jela katika maisha yake. Bi Diallo amefichwa. Tutasikia zaidi mahakamani. Siwezi kujua nani anasema ukweli kwa vile sikuwepo, ila naweza kusema kuwa maisha ya huyo mama yatabadilika. Yeye maskini halafu anachafua jina la tajiri. Nina wasiwasi hata familia yake huko Guinea wako hatarini kuchafuliwa jina.

Lakini jamani, dume zima tena tajiri ilishinda kununua malaya! Wanaomfahamu Bi Diallo wanasema kuwa ni mrefu ana urefu wa futi 6. Hivi Strauss-Kahan alidhani kwa vile mzungu yule mama atakubali kumpa nini?

Mnaweza kuona picha ya Bi Diallo kwa kuBOFYA HAPA:


Kwa habari zaidi someni:


http://www.nydailynews.com/news/world/2011/05/18/2011-05-18_we_want_you_out.html

http://abcnews.go.com/US/dominique-strauss-kahn-sex-case-alleged-victims-lawyer/story?id=13627104

http://www.telegraph.co.uk/finance/dominique-strauss-kahn/8521881/Dominique-Strauss-Kahn-maid-lives-in-apartment-block-for-HIV-sufferers.html

Friday, June 11, 2010

MZimbabwe Abaka Msichana New Jersey

Nyie wanaume kutoka Afrika, mkija Marekani poozeni hizo dhakari zenu. Kuna kijana kutoka Zimbawe mwenye miaka 19 tu ambaye anashitakiwa kwa kubaka huko New Jersey. Ilitokea baada ya Prom, yaani sherehe ya kumaliza Form Four. Hapa Marekani mwanamke akisema basi, manake basi! La sivyo mtafungwa na kuchafuliwa majina na kuitwa sex offender. Kijana huyo ni mwanafunzi na alikuwa ana kaa na host family. Nyege zimemponza. Anashikiliwa kwa dhamana ya $125,000. Huyo ambaye kabakwa lazima atakuwa mzungu, dhamana kuwa kubwa kiasi hicho!

Inaelekea kijana alishikwa na nyege mshindo. Binti ambaye kabakwa alikuwa amezimia kwa ulevi. Wenzake walimkuta anafanya mambo yake na kuanza kumpiga! Mnaweza kusoma habari kamili hapa:
http://www.cliffviewpilot.com/bergen/1355-northern-valley-student-charged-with-raping-fellow-senior-at-seaside-heights-motel

Pia,bado kuna mawazo finyu kuwa waafrika wana uume/miboro kubwa kuliko watu wengine. Hivyo wanawake watawashiwishi kutaka kuziona.

****************************************************

N.J. Prom-Party Rape Raises Red Flag


OLD TAPPAN, N.J. (CBS)

It was a nightmare for a teenaged girl celebrating her prom. She was raped during a party that was supposed to be joyous and memorable.

She was part of a group from Bergen County that traveled to the Jersey Shore last week to live it up.

It's a dangerous tradition that has changed the way some schools celebrate their proms.

Could this attack have been prevented? That's what students and parents at Northern Valley Regional High School are asking.

Jackie Finno is an 18-year-old who will be going to her senior prom on Friday night. Then, as the tradition goes, she and her friends will head to the Jersey Shore.

But news an 18-year-old girl was allegedly raped at her after-prom party at the Shore last Friday has Finno on edge.

"When I found out it was terrible. Oh my God. It's very nerve-wracking," Finno said.

But Finno's mother said she's still willing to let her go.

"With much stipulation and we trust. And we trust her and we trust her choices and we have to start letting her go, even through all these tragedies that occur," LeeAnn Finno said.

Police said 19-year-old Matthias Kabette from Zimbabwe and a senior at Northern Valley raped a classmate at a motel in Seaside Heights on June 4. Members of Kabette's host family declined to speak to CBS 2 HD on Thursday night.

"I can't comment I'm sorry," one said.

Students who know the suspect were stunned.

"He's a really nice guy. Like I can't see any bad sides about him," Eugene Kim said.

"I played soccer with him. He was a really nice kid," another student said.

Now parents and students are questioning if the alleged attack could have been prevented.

"I think it's an issue that you are giving teenagers today the freedom to go down to the shore at 16, 17 years old," one parent said. "You're asking for trouble."

Northern Valley junior Christian Mecca said he'd support a midweek prom, like many area high schools already have.

"Because it keeps people out of trouble. It is kind of a tradition to have it on a Friday and you're with your friends for the weekend. But I feel like, just everyone's just gotta be responsible," Mecca said.

Parents said they also bear the responsibility, but feel timing makes no difference.

"Do you think the day of the week probably would've mattered to this kid? Probably not," parent Mike Poole said.

"Is it something that can be completely avoided in our world? Unfortunately not," LeeAnn Finno added.

Kabette, who is studying in the U.S. on a student visa, is being held on $125,000 bail.

Saturday, September 12, 2009

Mzungu Afungwa Kenya kwa Kubaka Wasichana Wadogo!

(Pichani Jon Cardon Wagner na Judy Nyaguthie (kushoto) and Fetha Nyamweru (kulia) ambao kazi yao ilikuwa kumtafutie vibinti!)

Hii imenikumbusha maovu waliofanya wazungu kadhaa Tanzania nikiwa mwandishi wa habari Daily News. Utasikia mzungu kafanya maajabu, halafu kesho yake huyooooo kaenda zake Ulaya au Marekani yaani kawa deported persona non grata. Wengine hata waliua! Nakumbuka moja alitaka kunya kwenye midomo ya maCD! Mwingine alikuwa eti mwalimu lakini anatembea na wanafunzi! Wengine walilazima malaya wafanya ngono na mbwa!

Hebu na Tanzania muwe waangalifu na hao wazungu wanaokuja nchini kwetu kutafta visichana. Wanajua wakifanya hivyo Marekani/Ulaya watafungwa! Ngono na watoto wadogo ni mwiko kwao!

************************************************************

NAIROBI, Kenya (AP) - A magistrate in Kenya has sentenced an American who founded a popular chain of coffee shops to 15 years' imprisonment for the statutory rape of three teenage Kenyan girls.

Principal Magistrate Teresia Ngugi says Jon Cardon Wagner paid two women $500 to bring the 13-year-old and two 14-year-olds to his house. A Nairobi court convicted and sentenced him on Friday.

Ngugi says his alibi was weak because it relied on the word of his friends.

Wagner's lawyer Mohammed Nyaoga says his client is the victim of an extortion racket and will appeal.'

Nairobi Java House began a culture of gourmet coffee drinking nine years ago and now has eight coffee shops in the capital. It is popular with wealthy Kenyans and expatriates. The chain also exports Kenyan coffee to America and Europe.
Kwa habari zaidi someni:

Wednesday, March 18, 2009

Ubakaji na mauji ya watoto wadogo huko Iringa!

Jamani, hivi huko Iringa kuna nini? Kuna habari kuwa watoto wadogo yaani chini ya miaka sita wanabakwa huko! Sasa huo ni mchezo gani? Najua Afrika Kusini watu wanabaka hao watoto wakidhani eti watapona UKIMWI! Na nashangaa baba zima anataka nini na mtoto mdogo hivyo. Kama hao wahalifu watakamatwa napendekeza wakatwe ume/bolo zao mara moja! Tena mbele ya umati!

********************************************************************

Kutoka Lukwangule Blog:

VITENDO vya ubakaji vimeanza kushamiri mkoani hapa, huku matukio ya hivi karibuni yakionesha wanaokumbwa na sakata hilo wakiwa ni watoto wa kike wenye umri chini ya miaka sita.

Katika matukio mawili yaliyotokea ndani ya wiki tatu, mtoto mmoja amekufa baada ya kufanyiwa unyama huo huku mwingine akiendelea kutibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. Tukio lililopelekea mmoja wa watoto hao kufa lilitokea juzi, baada ya mtoto huyo (jina linahifadhiwa) kubakwa na watu wasiojulikana hadi mauti yake yalipomfika na hatimaye kutupwa kwenye bonde dogo la mlima Tagamenda uliopo mita 600 kutoka stendi ndogo ya mabasi ya mikoani ya Ipogolo ya Iringa mjini.

Polisi waliokuwepo kwenye eneo hilo walifanikiwa kuutoa mwili wa mtoto huyo mwenye miaka mitano kutoka katika bonde hilo lenye miti mingi yenye miba akiwa hana nguo na amelowa damu sehemu zake za siri, huku umati mkubwa wa watu waliokuwepo wakiangua kilio kwa uchungu.

Polisi hao wakiongozana na baadhi ya ndugu wa mtoto huyo waliukimbiza mwili huo katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya uchunguzi zaidi na wakati tukienda mitamboni ulikuwa umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dk Oscar Gabone alisema katika tukio lingine lililohusisha mtoto mwingine wa miaka mitano kubakwa kwamba lilitokea Februari 22 katika milima ya Gangilonga mjini Iringa aliyepokelewa hospitalini hapo Februari 23.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Jamila Mashaka alisema kwa uchungu kwamba siku ya tukio, mtoto wake na wenzake walikuwa wakicheza nje ya nyumba yao baada ya kujipatia chakula cha jioni.

“Ilikuwa majira ya saa moja jioni, baada ya kupata chakula cha jioni mwanangu huyu na wenzake wakawa wanacheza nje, hata hivyo dada yake alikuja chumbani kwangu baadaye akiniambia kwamba mdogo wake haonekani,” alisema.

Alisema jitihada za kumtafuta katika maeneo wanayoishi na kwa marafiki zake aliokuwa akicheza nao hazikuzaa matunda na ndipo ilipofika saa 4.30 usiku wa siku ya tukio walipkwenda kutoa taarifa Polisi.

“Kesho yake saa 4.30 asubuhi nililetewa taarifa kwamba kuna mtoto yuko hospitali ya mkoa, na nilipokwenda kumtazama nikabaini kwamba ni wa kwangu. Nawashukuru madaktari wanaomuhudumia kwasababu hivi sasa anaendelea vizuri,” alisema.

habari hii kwa hisani ya Frank wa HabariLeo Iringa

Saturday, June 14, 2008

MKenya abaka mvulana huko Philadelphia

Fred Magondu akisindikizwa kortini na polisi


Asante mdau Subi kwa habari hizi.

Huko Philadelphia, nesi wa kiume ambaye alikuwa anaangalia vijana wenye upungufu wa akili , alimbaka moja wao. Kijana mwenyewe ana miaka 14. Wanasema mtoto ni kipofu, na hajiwezi.

Nesi ametambulika kama MKenya, Fred Magondu, 36. Kwanza nilidhani wamemsingizia lakini wana ushahidi wa DNA. Walipima shahawa zilizokuwa kwa yule kijana. Magondu mwenyewe ana mke na watoto! Jamani! Aibu kweli kwa familia yake.

***************************************************************************

Mwenye kujifunza na ajifunze, mwenye kutoa onyo kwa wengine na atoe.
Subi

Male nurse charged with raping boy

By MATT COUGHLIN Bucks County Courier Times


A nurse caring for a physically and mentally impaired 14-year-old Bucks County boy is accused of raping the teen in April, according to police.

Fred Magondu, 36, a Kenyan national living on King Arthur Road in Philadelphia, was taken into custody at a Philadelphia nursing home Thursday afternoon and later arraigned on charges of molesting a child who was in his care.

Police said they learned of the rape April 30. The boy receives 24-hour nursing care because he is mentally and physically impaired, unable to speak and blind, police said. According to court records, another individual care nurse, who has been caring for the boy for about nine years, discovered injuries to the boy when she attempted to change his diaper after he arrived at school April 30.

The boy was first examined at St. Mary Medical Center in Middletown and then transferred to The Children's Hospital of Philadelphia. Doctors at both hospitals told police the boy was bleeding and bruised.

Police learned that Magondu, a Harleysville Pediatrics employee who has been caring for the boy for several months, was working at the victim's home from April 29 to 30. Magondu was allegedly alone with the boy from 5 a.m. to 7:40 a.m. before putting him on the bus to school, police said.

Investigators interviewed Magondu in early May at an unnamed Philadelphia nursing home where he works, according to court records. Magondu said that on April 30 the boy had been bleeding but the nurse believed it was a physical problem and had changed a set of soiled linens. Police collected a sample of Magondu's DNA and the boy's bed linens and sent them to National Medical Services for analysis.

In a report to police June 6, the laboratory said the linens tested positive for semen that matched Magondu's DNA and that the possibility of it being from another unrelated person was 1 in 7 trillion, according to court records.

Magondu was arraigned on multiple charges of rape, involuntary deviate sexual intercourse, indecent assault, corruption of minors and unlawful contact with minors and sent to Bucks County prison on $250,000 bail. If he is released, the judge ordered that Magondu have no contact with the child and surrender his passport to authorities.

Magondu has been a practical nurse since June 2006 and had renewed his license earlier this month, according to Department of State records. Those records list no prior disciplinary action. He also has an expired graduate permit that lists a prior address in Falls. During his arraignment Magondu told the judge he moved to Philadelphia from Fairless Hills with his wife and three children in January. He has no prior criminal record in Pennsylvania, according to state records.
The newspaper is withholding information about the teen to protect his identity.

Matt Coughlin can be reached at 215-949-4172 or mcoughlin@phillyBurbs.com.

June 13, 2008

Monday, October 22, 2007

Wasichana wadogo wawili wabakwa hadi kufa!

Jamani dunia inaenda wapi? Nawauliza tena mwanaume anakuwa na nyege kiasi gani mpaka kutaka kumbaka mtoto mdogo ambaye nyeti zake hazijakomaa kumudu tendo! Na hata kama ni mkubwa na hajakubali anaweza kuchanwa uke! Si uwongo! Kateni boro za hao wanaume wahalifu maana hawastahili kuwa nazo! Na wanyongwe hadharani!

Na mtasoma chini, wananchi wenye hasira hawakusubiri mkondo wa sheria na hii kesi!

********************************************************************************
Kutoka Freemedia.com

Wanafunzi wawili wafa kwa kubakwa

na Jumbe Ismailly, Singida

MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mrama, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida na mdogo wake aliyekuwa akisoma shule ya awali katika shule hiyo, wamefariki dunia baada ya kubakwa na kulawitiwa na watu wasiojulikana.

Wanafunzi hao wametajwa kuwa ni Twaiba Athumani (13) anayesoma darasa la sita na Zulfa Athumani (7), aliyekuwa akisoma shule ya awali.

Akizungumzia tukio hilo jana, baba wa watoto hao, Athumani Jumanne, alisema tukio hilo lilitokea juzi, kati ya saa 12 jioni na 2 usiku, umbali wa kilomita takriban mbili kutoka nyumbani kwake, kwenye eneo la shamba la viazi la mkazi mmoja wa kijiji hicho.

Alisema kabla ya tukio hilo watoto hao walitoka nyumbani majira ya saa 10:30 jioni kwenda kisimani kuchota maji kwa ajili ya kufulia nguo na kwamba mpaka inafika saa 2 usiku walikuwa hawajarudi.

Alisema, baada ya kuona hali hiyo waliamua kuwafuatilia, lakini hawakuwaona, hali iliyosababisha kwenda kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba 10, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na baadaye Kituo Kidogo cha Polisi Ilongero.

“Mpaka saa mbili asubuhi walikuwa hawajarudi...ilibidi tuwafuatilie hadi kwenye eneo lililokuwa na korongo na ndipo tulipookota kiatu cha tairi cha mtuhumiwa mmoja na tulipoendelea kufuatilia hadi kwenye shamba la viazi ndipo tulipoikuta miili ya marehemu ikiwa imetapakaa vinyesi na damu.

“Tuliweza kutambua viatu vya mmoja wa watuhumiwa baada ya kufuatilia nyayo na tulipofuatilia hadi kwa mmoja wa watuhumiwa, Hamisi Msaghaa, mkazi wa Kijiji cha Mrama tulimkuta akifyatua matofali na kumchukua hadi kituo kidogo cha polisi Ilongero,” alifafanua baba wa watoto hao.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji, Issah Swedi, alisema mtuhumiwa Mile aliyetoroka inasemekana alitoka gerezani hivi karibuni baada ya kumaliza kutumikia kifungo kwa makosa ya ubakaji na kwamba amekuwa na uzoefu wa kuishi gerezani kuliko uraiani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ilongero, Greace Kishindo, alithibitisha kupokea maiti hizo huku zikiwa zimetapaa damu na vinyesi.
Polisi mkoani Singida wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba inamshikilia Msaghaa kwa tuhuma hizo na bado wanamtafuta mtuhumiwa mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Mile aliyetoroka baada ya kufanya tukio hilo.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/17/habari31.php

********************************************************************************
From Ippmedia.com

Wavamia polisi na kuua mtuhumiwa 2007-10-22 08:47:45

Na Elisante John, PST, Singida

Mamia ya wananchi wenye ghadhabu wamevunja mahabusu ya kituo cha polisi cha Ilongero kilichoko wilayani Singida Vijijini, wakamtoa nje na kumpiga hadi kufa mtuhumiwa wa mauaji ya watoto wawili wa familia moja.

Aliyeuawa usiku wa kuamkia juzi ni Mile Nkindwa (20), mkazi wa Ilongelo wilayani hapo, aliyekuwa ametorokea kijiji jirani baada ya kufanya mauaji. Mtuhumiwa huyo alifikishwa kituoni kwa tuhuma za mauaji ya watoto wawili wa kike kwa kuwabaka, kuwalawiti na kuwanyonga kisha kuwatumbukiza ndani ya korongo na miili yao kugundulika ikiwa imetapakaa kinyesi na damu.

Habari kutoka kituo hicho zilisema Nkindwa baada ya mauaji hayo alitoroka na kujificha katika kijiji cha Mughamu. Hata hivyo, mtuhumiwa mwenzake Hamisi Juma Msaghaa (33) amefikishwa mahakamani mjini Singida kujibu mashtaka ya mauaji.

Akielezea tukio hilo, diwani wa Kata ya Ilongelo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Singida, Bw. Ramadhan Samwi, alisema mauaji dhidi ya mtuhumiwa huyo yalifanyika juzi saa 4:00 usiku nje ya kituo hicho. Alisema pamoja na kuwepo askari wa kutosha kutoka Singida mjini waliokwenda kituoni hapo kumchukua, wananchi walivamia kituo hicho kuanzia saa 3:00 usiku na kuwataka askari wamtoe mtuhumiwa aliyehusika na mauaji ya watoto hao.

Bw. Samwi aliongeza kuwa pamoja na askari kugoma kumtoa mtuhumiwa, wananchi walishinikiza atolewe hatua iliyosababisha wapige risasi hewani ili kuwatawanya lakini wananchi waliwazidi nguvu polisi na kuvunja milango na kumburuza nje mtuhumiwa na kumpiga hadi alipokata roho. Aliongeza kuwa wanakijiji hao walimshambulia kwa mawe, marungu, fimbo na kila silaha waliyoiona hadi akaaga dunia.

Akifafanua zaidi, diwani alisema marehemu Mile alikamatwa baada ya baba yake akiongozana na mwenyekiti wa Kijiji cha Itamka Bw. Mamu Mloya, kwenda katika kijiji cha Mughamu ambako mtuhumiwa alijificha kwa jamaa zake baada mauaji hayo. Alieleza kuwa walimnasa na kumfikisha kituo cha polisi cha Ilongelo ambako jioni yake ndipo alipouawa na wananchi hao waliokerwa na mauaji hayo ya kikatili.

Waliokufa katika mkasa huo ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mrama iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida pamoja na mdogo wake aliyekuwa akisoma masomo ya awali shuleni hapo. Watoto hao ni Twaiba Athumani (13) na Zulfa Athumani (7).

Watoto hao wa Bw. Athumani Jumanne, walikumbwa na vifo hivyo vya kikatili Jumatatu iliyopita kati ya saa 12:00 jioni na 2:00 usiku katika shamba la viazi la mwanakijiji mmoja, umbali wa kilomita mbili kutoka nyumbani kwao, wakati walipokwenda kisimani kuchota maji.

Hili ni tukio la tatu katika mwezi huu la wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kuvamia vituo walimowekwa watuhumiwa wa mauaji kwa lengo la kuwaua. Mwanzoni mwa mwezi huu, wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Kagera walivamia makao makuu ya polisi na kuchoma moto kituo kwa lengo la kumuua mtuhumiwa.

Katika tukio hilo, kulikuwa na uvumi kwamba kuna mwanamke kituoni hapo anashikiliwa na polisi baada ya kukutwa akiwa na ngozi ya binadamu. Hata hivyo, habari za kipolisi zinaonyesha kuwa uvumi huo haukuwa wa kweli. Wiki iliyopita, tukio kama hilo lilijiri mkoani Tanga ambapo watu wasiofahamika walivunja ofisi ya kijiji cha Nkogoi wilayani Lushoto na kumuua mtuhumiwa wa mauaji aliyekuwa amefungiwa ofisini humo.

Mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisubiri kupelekwa polisi ni kijana wa miaka 22, Yahaya Omari. Yeye anadaiwa kumuua kwa kumpiga rungu kichwani Muhsin Rashid (15). Marehemu Muhsin alikuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mavumbi.