Showing posts with label Lazarus Mbilinyi. Show all posts
Showing posts with label Lazarus Mbilinyi. Show all posts

Saturday, August 23, 2008

Ukweli Kuhsu Wanaume


Imeandikwa na Kaka Lazarus Mbilinyi

Wanaume viumbe wa ajabu sana, atakupa raha zote na ahadi kedekede, muhimu kutambua je, ni tamaa au upendo wa kweli?

Ni vizuri wanawake wote wakajua kwamba:Kufanya mapenzi kabla ya kuoana (premarital sex) na mwanaume haiwezi kukusaidia yeye ku – fall in love na au wewe kuwa mtu special kwake au kukuhakikisha mahusiano yanayoyumba yasimame vizuri au hata kusaidia mwanaume aji-commit kwako.
Mwanaume akiwa serious na mwanamke anayemtaka kumuoa ataweza kuvumilia sex kwa muda wowote mliokubaliana hadi ndoa.Mwanaume anapokujia kuna mambo mawili kutoka kwake jambo la kwanza inaweza kuwa ni tamaa zake na jambo la pili ni upendo wa kweli.
Pia usichanganye hayo mambo mawili.Kama mwanaume anakutaka kwa ajili ya tamaa zake, kitu cha maana anachokitaka kwako ni kutimiza malengo yake ya kukuchezea kwa ajili ya raha zake (sex). He is just for fun, hata kama atakuahidi mambo makubwa bado anakuwa lengo ni kukuchezea tu.
Kama mwanaume anakutaka kwa ajili ya upendo wa kweli, atakuwa tayari kuvumilia kukusubiri kwa sababu upendo wake ni zaidi ya sex, kwake maisha kwanza na yupo tayari kuvumilia.
Pia mwanamke kuwa bikira au mtakatifu (untouched) ni vitu ambavyo wanaume wanapenda sana, sababu ya msingi ni kwamba mwanaume akimpata mwanamke ambaye hajawahi kuwa na mwanaume mwingine hujisikia vizuri sana, anamwona ni mwanamke special na pia anampa feelings zaidi.
Hii ni kumaanisha kwamba jinsi mwanamke anavyokuwa na wanaume wengi kabla ya kuolewa hupunguza nafasi ya wanaume kujisikia vizuri kumuoa.

Njia nzuri ya kujua mwanaume anakupenda kwa upendo wa kweli uwezo wake wa kuwa serious na wewe ni jinsi anavyovumilia kuhakikisha mnaepuka sex kabla ya ndoa.
Mnaweza kusoma mada zingine za Kaka Mbilinyi kuhusu mapenzi bora huko The Hill of Wealth Blog:

Saturday, August 09, 2008

Tendo la Ndoa Uzeeni




Wadau, niliwahi kuposti mada hapa aliyoandika Kaka Lazarus Mbilinyi inatiwa 'Mawaidha Kuhusu Ndoa'

Sasa ameandikia kuhusu tendo la ndoa uzeeni.

Nadhani wengi tunadhani kuwa ukifikisha umri mkubwa ndo basi unaaga ngono/tendo la ndoa. Hiyo wazo inatia watu kiwewe. Kumbe wala, bado wamo! Asante sana kaka Mbilinyi kwa kuelimisha jamii kuhusu ngono tendo la ndoa. Natumaini watu hawatogopa kuzeeka sasa.

*******************************************************************
Na Lazarus Mbilinyi

Je, wazee wenye umri mkubwa bado huwa hamu kubwa ya tendo la ndoa? Utafiti wa sasa unaonesha kwamba jinsi mtu anavyozidi kuwa mzee uwezo wa kuonja, kunusa, kusikia na kuona hupungua. Pia uwezo wa kusisimuliwa kwa kuguswa hupungua pia.

Kiasili uwezo wa kusisimuliwa kimapenzi na uwezo wa kufanya tendo la ndoa pia hupungua (libido)Pia Utafiti unaonesha kwamba uwezo wa kufanya mapenzi huweza kupunguza kutokana na umri kuwa mkubwa ingawa pia umri kuwa mkubwa hauwezi kuzuia kabisa hamu ya tendo la ndoa (terminate).

Kuna ripoti kwamba wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 50 hadi 80 bado wana hamu kubwa ya kufanya mapenzi (libido) na si kufanya tu bali kufurahia mno tendo lenyewe.

Kuna imani potofu nyingi kuhusiana na tendo la ndoa katika umri mkubwa zifuatazo ni baadhi tu ya hizo imani; Kushindwa kushiriki tendo la ndoa ni matokeo ya umri kuwa mkubwa.Tendo la ndoa ni hatari kwa wazee wenye umri mkubwa. Uwezo au hamu ya tendo la ndoa (libido) hupungua kwa kadri mtu anavyozeeka.

Yote hapo juu si sahihi kabisa. Hizo imani potofu zipo kwa muda mrefu na zimekuwa zikisababisha watu wenye umri mkubwa (wazee) kushindwa kufurahia tendo la ndoa au uumbaji wa Mungu.

Je, mabadiliko ya mwili kwa wanaume wazee huathiri vipi tendo la ndoa?

Kawaida wanaume wazee huhitaji muda mrefu ili kuweza kusisimka.

Kile kilichokuwa kinahitaji sekunde chache hadi dakika chache katika umri wa miaka 19 huhitaji zaidi ya dakika 15 katika umri mkubwa kwa mwanaume.

Wanaume wengi wenye umri mkubwa hupona ugonjwa wa Kukosa uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kujifunza matokeo na athari za umri kwenda sana (Uzee) Katika umri ulioenda wanawake wazee wahahitaji kufahamu kwamba wanaume wazee huhitaji muda mwingi na wakutosha kuuandaa jogoo awike.

Mabadiliko mengine ambayo hutokea kwa mwanaume mzee sana ni kupotea kwa uwezo wa kufika kileleni tofauti na wakati akiwa kijana.

Hii ni kutokana na Kukosa hisia (sensation) za tendo la ndoa. Pia kiwango cha sperms anazotoa hupungua hivyo mwanamke mzee asiwe na mtazamo wa kudhani kuwa uwingi wa sperms ndio uzuri wa tendo la ndoa.

Mnaweza kumtembelea kwenye Blogu yake: http://www.mbilinyi.blogspot.com/