Thursday, March 24, 2011

Mh. Lukuvi na Rosemary Nyerere Nao Wapata Kikombe cha Babu

Wadau, naona vigogo wanakimbilia Loliondo kupata 'kikombe cha dawa'. Je, walipanga foleni na wengine au walipata 'bump'? Pia, eti kuna uvumi (au huenda ni kweli) kuwa Mzee Mandela wa Afrika Kusini naye alienda huko kisirisiri kupata kikombe. Kama hiyo dawa kweli inafanya kazi basi huyo babu apatiwe ulinzi mkali hata wa FFU 24/7. Maana wazungu wakipata fununu watamwua. Kisa makampuni ya madawa (Pharmacueticals) watafilisika kwa kukosa wateja.

Dawa ya babu OYEEEEE!


Waziri wa Nchi Ofisi ya Wazri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi (wa pili kulia) na Rosemary Nyerere (kulia) wakipata 'kikombe cha babu' kutoka kwa mchungaji mstaafu wa KKKT , Ambilikile Mwasapila (kushoto) waliopkwenda Loliondo. (Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog)

4 comments:

Anonymous said...

inasemekana inaponesha kuna jirani yangu aanacanser ya mguu ulikuwa unatoa maji unaoza sasa week ya pili amerudi toka loliondo mguu sehemu ya kidonda kimekaukaa anasubiri arudi tena hospital kujua kama na kwa ndani mguu uko vipi.pia ukiangalia kwenye loliondo wonder part 1 and 2 kwenye you tube tv ya kenya ntv wametengeneza documentary nzuri sana wanatushinda watz hatujui kabisa kutengeneza documentary itv na tbc ovyo you yube zao za loliondo.

Anonymous said...

Da Chemi unapointi. Ni kweli wanaweza kumwua. Kama wagonjwa wote watapona hizo dawa za UKIMWI na magonjwa mengine hazitakuwa na soko.

Anonymous said...

Mwl wangu Mama Mkwawa nakuona unapata kikombe. Mungu akulinde, ulinisaidia sana shule

aajnd@comcast.net said...

Nilikuwa siijui hii blog yako dada Chemi..HONGERA! Mola amzidishie miaka mingi kupita ile ya Methusaleem huyu mzee Rev.Mwasapila. Hii ni blessing kwa Taifa letu na wananchi wote. Keep on spreading the good news dada yangu.PEACE!