Saturday, March 26, 2011

Tiba ya Loliondo - Msimamo wa Mjengwa Blog

(Pichani) Baadhi ya waliofanikiwa kupata kikombe cha 'Dawa ya Babu' huko Sumange Village Loliondo

Nimesikia habari za watu kupona magonjwa yao baada ya kunywa dawa, pia nimesikia habari za watu amabo walizidiwa baada ya kunywa hiyo dawa na kuacha kutumia madawa waliopewa mahospitalini. Pia nimesikia habari za watu kufariki wakiwa wanasubiri kupata dawa ya ya babu.
Ningependa kusikia kutoka kwa watu waliokunywa daw ya babu kabla ya kuaamua kama inafanya kazi au la. Mungu yu Mwema na kweli kama ametupa dawa ya kuponyesha magonjwa yasiyo na dawa basi ingekuwa vizuri dunia nzima wajue habari hiyo.

******************************************************************************
Hii ni tamko rasmi kutoka Mjengwa Blog:

Ndugu Zangu,

Hii ni nchi yetu. Tunayaandika haya kwa mapenzi ya nchi yetu. Yanayotokea Loliondo yanaanza kubeba sura ya kashfa. Taratibu, Loliondo inaonekana kuwa ni aibu ya kitaifa kwenye masuala ya kimsingi ya afya ya watu wake.

Si kawaida, na yawezekana ni mara ya kwanza kutokea, kwa blogu ya jamii kutoa msimamo juu ya jambo la kitaifa. Tunauona umuhimu huo, tunafanya hivyo. Ndio, Hali ni mbaya Loliondo. Kuna Watanzania wenzetu wanakufa kila siku. Wanakufa wakiwa kwenye foleni ya kupata kikombe cha Babu au baada ya kunywa kikombe hicho na kuacha kutumia dawa zao walizokuwa wakitumia kabla.

Asubuhi hii nimepokea simu kutoka Dodoma. Kuna mganga aliyenielezea hali mbaya zinazowapata wagonjwa wake wa kisukari mara baada ya kupata tiba ya Babu na kuacha kutumia dawa zao. Anasema ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kisukari, maana, kisukari kinapanda haraka. Anasema kuna wagonjwa waliokufa baada ya kuacha kutumia dawa zao.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kupigia debe tiba ya Babu bila kufanya uchunguzi yakinifu. Ndio, duniani kuna fikra dhanifu na fikra yakinifu. Ya ‘ Babu’ wa Loliondo ni dhania iliyopaswa kuhojiwa kabla ya kupigiwa debe.

Hivi, wanahabari wetu wanashindwaje mpaka hii leo, kuwahoji madaktari bingwa kwenye maradhi kama UKIMWI, kisukari, na mengineyo. Madaktari hawa wako Agha Khan, wako Bugando, Mount Meru na kwengineko. Hivi, Watanzania wenzetu hawa, katika kazi zao, mpaka hii leo hawana cha kusema, cha kitaalam juu ya Tiba ya Babu? Au media imechagua kuficha ukweli?

Tunajua, kuwa habari za ‘ Babu wa Loliondo’ zinauza magazeti kwa sasa. Lakini, ni dhambi na kutoitendea haki nchi yetu kama tutaamua kufanya biashara na afya za watu wetu. Ni laana kubwa.

Ona sasa, Watanzania kwa maelfu wanakwenda gizani bila kuhoji, au kusaidiwa kuhoji. Katika dunia ya sasa ya Sayansi na Teknolojia hatuwezi kwenda mbele kwa kuendekeza ‘ Abrakadabra’ kama hizi za Loliondo.

Huu ni wakati, kwa Wizara na waziri mwenye dhamana, kutoa tamko rasmi juu ya ukweli kuhusu tiba hiyo ya Babu. Na kama ‘ Babu’ ataruhusiwa aendelee na tiba yake kwa wenye imani, basi, Babu huyu asaidiwe kuhamishia shughuli zake Arusha mjini. Lifanyike hilo ili tunusuru maisha ya Watanzania wenzetu walio katika hatari ya kupata maradhi mapya katika mazingira ya sasa ya Loliondo.

Tunayasema haya kwa mapenzi ya nchi yetu, basi.

Maggid,
Iringa,
Ijumaa, Machi, 25,2011
http://mjengwa.blogspot.com

9 comments:

Anonymous said...

As a Christian I have been wondering whether Loliondo is consistent to the Christian Faith and Theology. Here are some of my personal thoughts and reflections.

Is Loliondo genuine in the Christian Belief and Theology? Does it constitute an eschatological truth that God would intervene at this material time in Tanzania to relieve the sick and the suffering in a special way and save humanity? What is this? Is it a sign of the end of time? where many false prophets, apostles and healers as described in the Holy Bible will arise and draw many people astray? We must wonder after Loliondo what is next?

I ask myself after Loliondo magical healings, will the people be more faithful to God and precisely to Jesus Christ (for Christians) and live a longer life to inherit the Kingdom of God? After Loliondo what next? Here we are confronted by an enigma of a tricky balancing between magical healing and divine healing consistent to the Scriptures.

The whole Nation is groaning as flocks of people stream like sheep without a shepherd towards Loliondo. A healer attracts everyone, regardless of religion, race, and age to seek healing of the body. A dream of which God instructs, the healer provides the magical cup to heal the sick.

Now Loliondo shows a Nation roaring and yelling for healing of the body. People are seeking healing of the body probably with or without spiritual healing. The Loliondo event is a tip of a giant lack of sanctifying and healing Christian Faith hidden under the sea of suffering quiescence among the people of the Nation and of the world who seek complete salvation.

The suffering is an ancient struggle of humankind between faith in the soul and pain in the body. Loliondo shows a Nation hurt by the work of Satan the Lucifer of old, who engineered the fall of man in the Garden of Eden and from then humankind have struggled to bring the body and spirit in harmony.

One would be tempted to provide an answer to this enigma. In the Christian Faith for instance, throughout the ages, God has provided healing powers to selected few Saints to heal the sick in the body for a purpose of saving souls of people; that is to say, body healing would provide a spiritual healing to many so that their souls are saved from eternal condemnation. Body healing from diseases has not been an end to itself but a vehicle to complete spiritual inner healing.

The Christians believe that healing in the name of God must come through Jesus Christ and must aim at total healing that restores Salvation of the body and the spirit from the clutches of sin.

We must watch out, the Christian Faith may be in danger. For now let us enjoy the healing service and pray as we wait in silence for the truth to unfold.

Ngwizukulu Shilinde

Anonymous said...

Da Chemi, mbona hujaandika kuwa Mzee Mandela naye kapelekwa huko kisirisir kupata dawa. Insemekana yuko fiti kabisa sasa anajikisika kama kijana wa miaka 20!

Anonymous said...

Da Chemi comment yako nimeipenda, maana umeiweka very practical, badala ya kuanza ku-debate kuwa dawa ya loliondo ni kweli ya Mungu umeuliza tu simple je watu walioenda huko wamepona au la?
Kwa maoni yangu hiyo ndio the simplest way kujua kama ya Loliondo ni maajabu au la.

Anonymous said...

ni kweli maana mjengwa yuko upande mmoja kuhusu babu anaona kama babu ni tapeli hapo kwa mtu mwenye kuamini atapona na bible imesema watakuja manabii wa aiana nyingi ni kuamini kwako yupi wa kweli na yupi sio lakini yeye kaishaona babu tapeli fulani kama mwandishi anatakiwa ajuekuuliza kama wewe unavyofanya uchagui upande mmoja kama yeye kweli ni mwandishi aenda atafute watu wasiopona na waliopona awahoji ili apate jibu linaloweka.kama wakenya waliotengeneza documentary yao wameuliza pande zote wanaomini na wasioamini ni juu yako wewe na watu wanaokwenda huko sio mgonjwa kwamba wamependa ni matatizo ya mda mrefu ambayo wameangaika hospital bila mafanikio

Anonymous said...

I would like to comment very briefly on Ngwizukulu Shilinde's comments as I am also a Christian and a theologian.

God has always desired to heal man from the time when man fell from grace.
Contrary to most Christian's false belief the devil does not have the power to heal.
The Devil is devoted to threefold mission Kill, Steal and Destroy.

Most so called Christian theology is a confused belief system that is rooted in occult that seems to promote the supremacy of Satan.

Jesus said a Kingdom divided against itself can not stand. This statement was in response to the accusation by Jesus detractors claiming that He (Jesus) used the power of Beelzebub (The prince of demons) to heal and to cast our devils.

There is no such thing as the Devil who heals people.
Jesus said, If you do not believe in me, do believe in the works that I do.

Believer,
Dar es salaam, Tanzania

Anonymous said...

Maggid,

Wewe ni conspiracy theorist mzuri! Naona kwa asili yako una-attach ulrerior motives hata kwenye vitu ambavyo mtu wa kawaida asingejisumbua kusoma mno katikati ya mistari!

Naheshimu sana maoni yako kuhusu kutoamini kwako yale anayoyafanya babu maana kikweli hauko peke yako kwenye hiyo imani. Mimi pia nina maoni yangu tofauti kuhusu anachokifanya babu na hata watu wengine ambao wanasema wanatibu kwa imani ambao kila siku tunawaona mitaani na kuwasikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. KInachonitofautisha mimi na wewe ni huo uthubutu wa kusema wazi kuwa kinachofanyika ni Abrakadabra. Ili haya madai
yako ya abrakadabra nayo yasiwe ya kiimani kama unavyomtuhumu babu; kwa nini usiweke ushahidi ulio nao wazi? Baadhi ya hoja ulizozitumia naona haziwezi
kusimama zenyewe hasa zinapoangaliwa kwa mtizamo wa kidini. Tazama baadhi ya nukuu hapa chini:

*..."Babu anasema, kuwa Mungu ndiye aliyepanga bei ya tiba ya kikombe iwe shilingi mia tano. Kuwa alimwonyesha mia tano! Na Mungu akamwambia wageni walipe dola moja!"* Mtizamo wangu:

Mambo ya kimungu yanatupa sisi waumini options mbili tu; kuamini au kutoamini! Option ya ku-second guess maelekezo ya mungu haipo!! Kwenye hiyo nukuu sijaelewa ulichomaanisha ni kuwa huamini kama ni kweli babu katokewa na mungu au unaamini kuwa katokewa na mungu ila alichoambiwa hakiingii
akilini kuwa kimesemwa na mungu? Kama una ushahidi kuwa babu hajatokewa na mungu tupatie na sisi wenzio. kama huna fanya kama tunavyofanya sisi wenzio
ambao tuna mashaka yetu lakini hatuna ushahidi wa kunyoosha kidole kama ufanyavyo wewe!

*..."Na kwenye taarifa ya habari iliyofuatia ikaripotiwa, kuwa Serikali imeshindwa kutoa tamko jana juu ya tiba ya Babu kwa vile Babu amesema kamati iliyoundwa iende kwanza Loliondo!"*

Natambua kuwa ni kweli serikali haikutoa tamko jana kama tulivyoahidiwa. NI kweli kutotoka kwake ni kwa sababu ya Babu kuamuru waende kwanza Loliondo?
Ndivyo ilivyosemwa kwenye taarifa ya habari? Kama hiyo ni kweli then
inawezekana kukawa na ukweli kuwa babu alitokewa kweli na mungu maana hizo nguvu alizonazo sasa zitakuwa zimepitiliza!!!!!

Ushauri, epuka sana kutoa hitimisho hasa kwa vitu ambavyo ushahidi wake ni mgumu kupatikana.

Chizi said...

Wakuu, ni kama joke lakini wikiendi hii nilimkuta dogo mmoja amelewa chakari kijiweni, nilipofika tu akaanza kuniambia, "Bro, hivi ikiwa dawa ya babu, wanayosema inatokana na mti wenye sumu, ikawa na madhara (side effects) baada ya muda kama miezi sita au mwaka, hii nchi si itakuwa inaongozwa na ma-mento? machizi kama mimi? maana inasemekana JK kanywa, wakuu wa mikoa, watendaji wakuu wa serikali, mawaziri, maaskofu, wafanya biashara wakubwa, vigogo wanasiasa etc etc." Nilimpuuzia, lakini.....!!!!?????????

Anonymous said...

Ni kitu kisichopingika kwamba serikali inaonekana kukubaliana na tiba ya Babu wa Loliondo kwa kuamua kumpa misaada ya magari, manesi na ulinzi, vitu vinavyogharamiwa na kodi za umma.

Kwa hali hii naipa changamoto serikali hiyo changamoto ya kutoa tamko -- bila kigugumizi kwamba wale wote wanaoishi na VVU na kutumia dawa za ARV, basi:

1. Waache mara moja kutumia dawa hiyo (ARV) baada ya kupata kikombe cha Babu.

AU

2. Waendelee kutumia ARV, pamoja na kupata kikombe cha Babu.

Serikali lazima iwe na msimamo unaoeleweka, siyo kujificha-ficha nyuma ya pazia la dawa ya "imani" kwani sasa hivi ni mapema mno kujua athari (au la) za tiba ya Babu. Sasa basi endapo hapo baadaye Watz waliopata tiba hiyo watadhurika, basi tujuwe kwamba hiyo ilitokana na maelekezo ya serikali yetu ambayo ndiyo pekee yenye dhamana kubwa ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wake.

Pili, ingefaa serikali imlazimishe babu kuweka kumbukumbu za wagonjwa wanaokwenda kwake kupata tiba kwa kuwaorodhesha majina na anuawani zao kwa sababu endapo kutatokea mtu aliyepata kikombe hicho na kudhurika, basi aweze kufungua mashitaka mahakamani dhidi ya Babu.

Bila kumbukumbu itakuwa vigumu kwa babu kukubali kama kweli alimpa mtu huyo kikombe.

Anonymous said...

Hiyo picha ni aibu tupu. Watu wanakunywa vikombe khaa! Waliopona wako wapi mbona waliokunywa wamekufa wengi?