Showing posts with label Mtoto. Show all posts
Showing posts with label Mtoto. Show all posts

Sunday, June 01, 2014

Mtoto Nasra Afariki Dunia


Marehemu Mtoto Nasra

MTOTO Nasra aliyekuwa akiishi kwenye box kwa miaka minne ikidaiwa kuteswa na mamake mkubwa baada ya mama yake kufariki, huku akikosa uangalizi wa karibu, chakula, tiba na huduma nyingine muhimu AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba, tatizo ni Nimonia (Pneumonia) na homa ilipanda sana.

 R.I.P NASRA wewe mbele sisi nyuma tutakufuata.Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi.


Kwa habari zaidi kuhusu Maisha ya Mtoto Nasra BOFYA HAPA:

Tuesday, April 16, 2013

Msiba Dallas, Texas - Mtoto Zoelle Reeves (Alikuwa na Siku Nne Tu)

Wadau na wana Mlimani,

Nasikitika kutangaza kifo cha mtoto mchanga, Zoelle Imani Nalumansi Reeves.  Alizaliwa 9/4/13 na kufariki dunia 12/4/13. alikuwa duniani siku nne tu.  Wazazi wa Zoelle, ni Catherine Sembajwe-Reeves na Adrian Reeves wa Dallas, Texas. Alizaliwa mzima wa afya, alienda kupimwa kama kawaida ya watoto wachanga hapa USA.  Alifariki usingizini.  Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

Familia ya Prof Sembajwe waliwahi kukaa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Simba Road No. 12 (Mlimani).

Saturday, July 07, 2012

AKrimu Mtoto Halafu Adai Kazaa na Mhindi!

Huko Zimbabwe kuna mambo! Mama moja kakrimu mtoto wake ili aonekane shombe halafu kaenda kwa mhindi kudai yeye ni baba.  Nia yake ilikuwa kumtapeli huyo mhindi ili kupata pesa! Huyo mama kaolewa lakini katembea nje ya ndoa yake na mhindi.

Natoa pole kwa huyo mtoto! Kuwa creamed mwili mzima unaweza kumletea madhara ya afya kama kansa ya ngozi.  

Huyo mama na mue wake wanashitakiwa mahakamani kwa kosa la utapeli.

*******************************************
HARARE, Zimbabwe (AP) - Prosecutors in Zimbabwe say a fraud trial is set to hear claims a black baby was treated with skin-bleaching cream to extort money from a man of Asian descent.

Prosecutor Malvern Nzombe said a court in the second city of Bulawayo on Friday ordered a Zimbabwean woman and her husband to reappear for trial at a date to be set in August.

   He said it is alleged they wanted the baby to appear that it was of mixed race in a plot to "reap financial benefits" from the light-skinned man with whom the woman had an affair.

   Her husband is accused of helping plan the scam, Nzombe said.

   In Zimbabwe's troubled economy, authorities have reported a recent spate of bizarre cons to extract money from unsuspecting victims.