Sunday, June 01, 2014

Mtoto Nasra Afariki Dunia


Marehemu Mtoto Nasra

MTOTO Nasra aliyekuwa akiishi kwenye box kwa miaka minne ikidaiwa kuteswa na mamake mkubwa baada ya mama yake kufariki, huku akikosa uangalizi wa karibu, chakula, tiba na huduma nyingine muhimu AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba, tatizo ni Nimonia (Pneumonia) na homa ilipanda sana.

 R.I.P NASRA wewe mbele sisi nyuma tutakufuata.Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi.


Kwa habari zaidi kuhusu Maisha ya Mtoto Nasra BOFYA HAPA:

9 comments:

Anonymous said...

Hawa nao! Amekaa kwenye box miaka yote hajafariki, wamemtoa ndo amefariki? What the heck is this?

Anonymous said...

Uwezekano wa kuishi ulikuwa mdogo,mi nahisi ushirikina umetawala kama walimfanya ndondocha.Hadi tumbo la uzazi linauma duuuh!

Anonymous said...

Mwenyezi mungu aiweke roho ya mtt mahala pema amina.sheria ifuate mkondo wake na mashtaka ya wakatili wale yabadilishwe kuwa mauaji ya kukusudia.

Anonymous said...

Mazingira ya pande zote mbili yachunguzwe kwa kina na adhabu stahiki kwa uzembe na manyanyaso yoyote ya kijinsia dhidi ya kiumbe hiki cha Mungu kwa kufuata sheria za nchi

Anonymous said...

itakuwa madaktari wamekosea utaratibu, niliwahi kusoma habari moja ya kiukweli kabisa kuwa chizi ambaye anakula majalalani muda mrefu ukimpa chakula kisafi na maji safi ataharisha! Nadhani mwili wa mtoto ungetakiwa kuzoeshwa taratibu mazingira ya kawaida badala ya kumbadilishia kwa ghafla. Kwa mfano mwili wake inawezekana ulikuwa bado haujazoea oxygen nyingi etc.

Anonymous said...

Tukumbuke hiyo homa ya mapafu ilimuanza akiwa kwenye box maana serkali ilipofika pale kumchukua alisikika akikohoa hadi kupaliwa ndani ya box.na hata majirani walimsikia akiwa
Anakohoa sana ndio maana wakaenda kufichua hiyo siri . Pengine angechukuliwa mapema angeweza kupona

Jerry L said...

Mtoto Nasra Said aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka 3 amefariki usiku wa kuamkia leo Muhimbili, Ofisa Ustawi wa jamii athibitisha
Ki ukweli hapa kuna maswali ya msingi ya kujiuliza
1.mbona hakufa kwa miaka yote aliyokaa kwa mateso ndani ya box?
2.ina maana tuanze kuwa na wasiwasi na madr wetu na hospitali?
3.au ni wakati wake ulifika wa kufa?
Ni maswali mepesi kimtazamo lakini yanaitaji majibu mazito na yaliyoshiba ili watz wawe na imani na hospitali zao hususani ya taifa muhimbili.

Anonymous said...

Jambo hili linasikitisha na kuhuzunisha sana, huzuni yangu imerudi tena maana niliposoma habari ya mtoto huyu kuishi ndani ya boksi nilihuzunika sana, sasa kifo chake kimetonesha tena kidonda moyoni mwangu, Mungu wangu na BWANA wangu nimeumizwa sana na mateso na kifo cha mtoto huyu, watu wamekuwa wanyama sana, tabia za watu(kuwa na utu) zimehamia kwa wanyama na unyama umehamia kwa watu, hawa walezi washughulikiwe kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wahuni na wapuuzi wengine wanaofanya makosa kama hayo, aisee ukifa hata wale ndugu yako unaowasaidia sana wanaweza kumnyima mtoto wako maji ya kunywa

MG said...

Nasikitishwa na kisa cha mtoto nasri hadi mauti yake, lakini kuna maswali mengi kuliko majibu. 1. Mtoto alichukuliwa akiwa anaongea na kutabasamu hivyo hakuwa mahututi kama tunavyoaminishwa na vyombo vya habari, kimetokea nini hadi kafa ghafla? 2. Huyu mtoto hakuwahi kunyonya maziwa ya mama kwani mzazi wake alifariki siku chache baada ya kuzaliwa hivyo aliishi kwa maziwa ya ng'ombe hawezi kuwa na siha njema hivyo hao walezi walijitahidi mno, hao wanahabari kutulisha sumu ya habari kuwa mtoto alikuwa kwenye mateso makali sidhani kama wako sahihi nao wachunguzwe na vyombo husika. 3. Kuwakamata walezi wa mtoto naamini kulisababisha madaktari kutopata historia sahihi ya mtoto na kusababisha kutotoa tiba sahihi.Utendaji kazi wa dawati la jinsia nao ufanyiwe tafhmini, kwani wamegeuka babamkwe wa kusuluhisha ndoa. 4. Nachoona mie mtoto alikuwa na utapia mlo kutokana na maisha duni ya walezi, je tunao wataalamu wa lishe katika hospitali zetu? Au ukifika hata kama una malnutrition unaanzishiwa drip za pneumonia? 5. Kuwekwa ndani ya box ni eneo hatarishi? Aliishije miaka minne humo na abaki na tabasamu na ajue kuongea kiswahili kwa ufasaha? ni kawaida mama kumweka mtoto kwenye ''baby walker'' ili mtoto asijikweze hadi eneo hatarishi, sasa kamamzazi hana uwezo wa kununua ''baby walker'' si anaweza tumia box huku akilitandika vizuri kwa baby show na blanket laini?