Showing posts with label Mlimani. Show all posts
Showing posts with label Mlimani. Show all posts

Tuesday, May 06, 2014

Michezo ya EAC Inter-Collegiate 1965

Baba yangu mdogo, marehemu Prof. Crispin Hauli, (mbele) katika mazoezi ya kukimbia pale UDSM Mlimani Campus mwaka 1965.  Alishindana katika michezo ya East African Community Inter-Collegiate Games mwaka 1965, baba mdogo alipata medali ya dhahabu katka mbio za 15,000 meters.

Saturday, June 22, 2013

Mwanafunzi wa UDSM Auwawa na Majambazi



Mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi wanne wa mwaka wa IV wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la Yombo la Chuoni hapo. 
 
Inataarifiwa kuwa waanafunzi hao walikuwa wanajisomea na kuandaa “dissertation” zao kwa mwaka wao wa mwisho wa masomo, na ghafla wakavamiwa na watu waliowaamuru watoe kompyuta zao na pochi za fedha. Wanafunzi hao walikubali shuruti hiyo lakini mmoja wa wanafunzi alipoomba walao wachukue nakala ya documents zao kutoka kwenye computer hizo, ndipo mmoja wa majambazi hayo alipomoiga risasi ya tumbo mwanafunzi huyo, ambaye alianguka chini.

Imeelezwa kuwa wanafunzi wengine kuona hivyo waliwasiliana na uongozi wa Chuo kuomba gari la kumwahisha mwenzao Hospitalini.
Taarifa zaidi za hali ya majeruhi huyo bado hazijawekwa bayana.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kuwavamia wanafunzi vyuoni kwa nia ya kuwapora ama kuwabaka, jambo ambalo limewaacha wengi wakiwa na hofu juu ya usalama wao, baada ya wenzao kupoteza vifaa vyao ama kujeruhiwa na wengine wakipoteza uhai.

Baadhi ya matukio haya yameripotiwa na wanafunzi kuandamana katika vyuo vya St John's Dodoma, IFM Dar, Uhasibu Arusha na sasa Mlimani, Dar.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2WrTyqTKa

Tuesday, April 16, 2013

Msiba Dallas, Texas - Mtoto Zoelle Reeves (Alikuwa na Siku Nne Tu)

Wadau na wana Mlimani,

Nasikitika kutangaza kifo cha mtoto mchanga, Zoelle Imani Nalumansi Reeves.  Alizaliwa 9/4/13 na kufariki dunia 12/4/13. alikuwa duniani siku nne tu.  Wazazi wa Zoelle, ni Catherine Sembajwe-Reeves na Adrian Reeves wa Dallas, Texas. Alizaliwa mzima wa afya, alienda kupimwa kama kawaida ya watoto wachanga hapa USA.  Alifariki usingizini.  Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

Familia ya Prof Sembajwe waliwahi kukaa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Simba Road No. 12 (Mlimani).

Wednesday, December 14, 2011

Hali UDSM Sasa ni Shwari!


Kuna vijana kadhaa huko UDSM ambao walileta fujo hapo Mlimani katika siku chache zilizopita. Hivi, hiyo migomo inasidia kweli au watu wachache ndo wanaumia?  Na wakiharibu mali ya watu inasaidia nini? Hao waliofukuzwa wataenda wapi? Ada zao zimepotea.

Mdau FK ambaye yuko UDSM campus (Mlimani) ameleta taarifa hii:
***********************************************************

Ukweli ni kwamba hapa chuoni kwa sasa ni shwari kabisa. Walimu tunaendelea na ufundishaji kama kawaida ingawa siku kadhaa hivi vipindi vya kuanzia saa 5 vilikuwa havifundishwi kutokana na wanafunzi kugoma. Kimsingi waliokuwa wanasababisha hali kutokuwa shwari ni wanafunzi wachache amabao walikuwa wakiwahimiza wenzao wawaunge mkono kwenye mgomo. Mwanzoni madai yao yalikuwa ni kupewa mikopo kwa wale waliokuwa wamenyimwa na baadaye wakabadili madai kwa kutaka wenzao waliokuwa wamesimamishwa kuachiwa pasipo masharti bila ya kuangalia kama baadhi yao walikuwa na kesi mahakamani.


Kwa tarehe 12, yaani juzi jumatatu, wanafunzi hao waliamua kuleta vurugu hapa chuoni kwa kwenda cafeteria kuwamwagia wenzao chakula, kuweka mchanga kwenye chakula kilichokuwa jikoni na kwenye masufuria na kuvunja majokofu yalioko cafeteria. Pia waliharibu mabasi yanayotoa huduma kati ya hosteli ya mabibo na chuo na kusababisha huduma hiyo kusitishwa mpaka leo. Ila jana Makamu Mkuu wa Chuo ametoa tamko na Baraza la Chuo na kuamua kwamba wanafunzi 8 wanasimamishwa masomo, 35 watasimamishwa kwa miezi 9 na 15 watapewa onyo.

Hata hivyo, bado polisi wanachukua tahadhari kwa kuhofu kuwa huenda wakajipanga tena kuja kuleta vurugu. Kimsingi inasemekana kuwa hao wanafunzi waliosimamishwa wanataka kupanga vurugu ili chuo kifungwe na wote warudi nyumbani. Kwa sasa hapa chuoni kuna landcuiser tatu za FFU lakini hakuna askari wa kutosha na hawana maji ya kuwasha zaidi ya kuwepo tu kwaajili ya tahadhari. Uamuzi wa kutowatawanya jana kwa virungu kumesadia sana kuiweka hali ya chuo kuwa shwari.

Tuesday, November 15, 2011

Picha za Bongo Miaka Ile!

Mdau Dar Millionaire ametuma hizi picha za Bongo miaka ile.  Sehemu zingine hazijabadilika sana.
Oyster Bay

Korogwe Hotel

Maghorofa City Center

Basi Dogo la UDA


Mtaa wa Uhuru 1975


University of Dar es Salaam -Mlimani 1974

Zanzibar Airport 1960's